https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, March 29, 2013

Kuanguka kwa ghorofa Kariakoo, Kamanda Kova apiga mkwara mzito


 Jengo lililo pembeni mwa msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi katikati ya jiji la Dar es salaam linavyoonekana baada ya kuporomoka asubuhi hii. 

Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Suleiman Kova kawaambia wanahabari kuwa kila aliyehusika na ujenzi, usimamizi na hata utoaji vibali atawajibishwa endapo kutaonekana kumekuwepo uzembe upande wake hadi kusababisha kadhia hiyo.

Inasemekana kuwa, jengo hilo linakisiwa kuua watu wawili na juhudi za kuwaokoa watu waliokuwa kwenye kifusi hicho zinaendelea.
 Watu wakifuatilia kwa karibu hali ya mambo inavyoendelea mara baada ya jengo hilo kuanguka leo asubuhi na kuzua taharuki kubwa.

Simba waivulia kofia Kagera Sugar kwa kuwatoa kamasi



Kukipiga na Toto African kesho Jumamosi Mwanza

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Simba, umesema licha ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya timu ya Kagera Sugar, ila wachezaji wao wamecheza soka la uhakika, ingawa nafasi ndogo zilizotumiwa na kocha wa Kagera, King Abdallah Kibadeni, zilichangia kuwaua katika mchezo huo.
                            Juma Kaseja
Kibadeni ni kocha na mchezaji aliyewahi kuwika na Simba kwa misimu kadhaa, kabla ya kuhamia pia kuinoa klabu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya Patrick Liewing na wasaidizi wake, Jamhuri Kihwelo Julio na Moses Basena, raia wa Uganda, aliyewahi pia kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Nafasi za kazi kibao Serikalini, changamkieni waungwana

Serikali yatangaza nafasi za kazi 1,134
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza nafasi wazi za kazi kama zilivyo katika Tangazo la Lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.

Jengo la ghorofa 14 laangukia Msikiti Kariakoo



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
JENGO jipya linaloendelea kujengwa lenye ghorofa 14 limeangukia Msikiti na eneo la Madrasa mitaa ya Kariakoo wakati watoto wapo ndani yake wanaendelea kujifunza masomo ya Kiislamu.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Seleman Kova
Habari zaidi juu ya tukio hilo zitaendelea kukujia, ingawa watu waliokuwa kwenye eneo la tukio wanasema kuwa jengo hilo lilikuwa kwenye ujenzi.

Kuanguka kwa jengo hilo, kunahisiwa kuwa kutakuwa kumeua, huku tukisubiri taarifa rasmi za kitaalamu na zitakazotoa ushuhuda na maafa yaliyotokea katika kadhia hiyo.



Thursday, March 28, 2013

Juhudi za DC Muhingo wilayani Handeni zazaa matunda suala la mimba shuleni

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni, Zuber Chembera akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu.
Ofisa Elimu wa Wilaya ya Handeni, Mgaza Muchiwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Stori, picha kwa hisani ya Joachim Mushi.
MATUKIO ya kesi za kuwatia mimba/kuwabaka wanafunzi yaliokuwa yameshamiri katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani Handeni sasa yameanza kupungua tofauti na ilivyokuwa awali. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Machi 2012 na Machi 2013 matukio ya mimba yanapungua.

Mbunge wa Chambani, Salim Hemed Khamis afariki Dunia

Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis (CUF),amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Taratibu za kuusafirisha mwili kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika. 

Habari kamili tutaendelea kuzitoa kadri tutakavyokuwa tunazipata kutoka kwa serikali na ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu.

Yatosha ya Airtel yapangwa kutia timu kila Mkoa Tanzania

Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea wakati akitangaza kwamba Airtel  kufanya Matamasha ya Airtel Yatosha katika mikoa mbalimbali ya Tanzania yenye lengo lan kutoa burudani sambamba na kuelimisha Jamii na wateja  wake kuhusu huduma za Airtel ikiwemo kuitambulisha huduma mpya ya Airtel Yatosha. Kulia Meneja Mauzo Airtel  Kanda ya Pwani  Raphael Daudi
Kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee  ni moja ya kikundi kitakachotumbuiza katika Matamasha ya Airtel Yatosha akiongea wakati wa uzinduzi wa Matamasha hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel morocco, Matamasha haya yatawashirikisha wasanii wengine wakiwemo Fid Q,   Juma Nature,   Ney wa Mitego  na Stamina.Kulia Meneja Mauzo Airtel  Kanda ya Pwani  Raphael Daudi
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Airtel Tanzania leo imetangaza mpango wake wa kufanya matamasha ya Airtel Yatosha yenye lengo la kutoa burudani na kuwaelimisha jamii na wateja wake  juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Airtel ikiwemo huduma mpya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa gharama nafuu zaidi.
Akiongea wakati wa kutambulisha matamasha hayo, meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeamua kutoa burudani wakati wa msimu huu wa sikukuu ikiwa ni pamoja na kuitambulisha huduma yetu ya Airtel yatosha kwa watanzania,  tunaamini kwa kupitia matamasha yatakayofanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania wateja wetu na watanzania kwa ujumla watapata burudani na kupata nafasi ya kupata elimu juu ya huduma zetu Nyingi
“Safari yetu ya burudani za Airtel yatosha itaanza katika Mkoa wa Morogoro katika siku ya  Jumapili na Jumatatu ya Tarehe 31/3 na 01/04/2013,  Kuanzia Saa Tatu kamili Asubuhi mpaka saa Kumi na Mbili Jioni, pale katika viwanja vya Sabasaba.
Tutakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Fid Q,   Juma Nature,   Ney wa Mitego  na    Tip Top Connection. Kiingilio ni BURE , tunapenda kukukualika wewe na washikaji zako wote kuhudhuria katika tamasha hili la kwanza kabisa pale morogoro na utape burudani kabambe. Njoo na Kitambulisho chako ili uunganishwe na ufurahie ofa nyingi toka Airtel” aliongeza Mmbando
Naye kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee  alisema” kama kawaida tumejipanga kuwapa wateja wa Airtel na watanzania burudani ya Ukweli katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, tunaomba watanzania wajitokeze kwa wingi katika matamasha haya ya Airtel Yatosha. Mbali na sisi kutoa burudani itakuwa nafasi pia kwetu kuona vipaji mbalimbali vya mashabiki wetu ambao ndio wasanii nyota wa kesho hivyo tuwapa hamasa ya kujitokeza kwa wingi ili tuweze kuburudika pamoja.
Wasanii watakaoshiriki katika Matamasha maalumu ya Airtel yatosha watatumbuiza kwa vibao vyao mahiri kama vile Fid Q na kibao chake cha Sihitaji Marafiki na  Ney wa Mitego na kibao chake cha Nasema Nao huku Tip Top Connection wakiwakilisha na kibao chao cha Nani kamwaga pombe yangu

Airtel hivi karibuni imezindua huduma ya Airtel Yatosha inayomuwezesha  mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.  Mteja anajiunga kwenye huduma hii kwa kupiga *149*99#

Masanja Mkandamizaji apania Tamasha la Tumaini Jipya

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MCHEKESHAJI maarufu na mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Emmanuel Mgaya, Masanja Mkandamizaji, amesema kuwa amejipanga imara kuhakikisha kuwa anafanya vitu vya aina yake katika onyesho la Tumaini Jipya, linalotarajiwa kufanyika mkoani Morogoro Machi 31, katika Uwanja wa Jamhuri na kushirikisha pia wakali mbalimbali.


Masanja Mkandamizaji

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Masanja alisema kuwa amejiandaa vyema kutangaza neon la Mungu kwa kupitia kipaji chake cha uimbaji wa muziki wa Injili, akiamini kuwa afya yake itakuwa njema na kuimba pamoja na wadau wao katika onyesho hilo la Tumaini Jipya.
Masanja Mkandamizaji
Alisema ingawa anatamba sana katika ulingo wa uchekeshaji kwa kuwa na aina ya uzungumzaji na kufurahisha watu wengi, lakini makali yake hayaelezeki katika uimbaji wa muziki wa injili.

“Nipo sawa kiafya na naamini Mungu atanibariki kila zuri kwa ajili ya kuimba pamoja kwenye tamasha hilo la Tumaini Jipya nikiwa na waimbaji wengine wenye makali ya aina yake.

“Itakuwa ni siku nzuri kwa siku ya Jumapili ya Machi 31 katika uwanja huo wa Jamhuri, hivyo naamini watu watakuja kwa wingi kulishuhudia neno likipenya masikioni mwao,” alisema Masanja Mkandamizaji.

Mbali na Masanja, wengine watakaofanya onyesho hilo ni pamoja na Martha Mwaipaja, Stara Thomas, Bahati Bukuku, Sifa John, Joseph Nyuki pamoja na vikundi mbalimbali vya kwaya vikitajwa kuwapo kwenye tamasha hilo la Tumaini Jipya litakaloanzia mkoani Morogoro.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...