Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick moja ya kompyuta sita zilizotolewa na taasisi yao kwa mkoa huo kama msaada wa kuweza kuongeza utendaji kazi mzuri kwa watumishi wa umma, hususan kwa Manispaa ya Moshi, Halmashauri ya Mwanga na Halmashauri ya Same, huku kila moja ikipewa kompyuta mbili. Kushoto kwa RC Sadick ni Katibu Tawala wa Mkoa huo wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Aisha Amour. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
HALMASHAURI
ya Wilaya Same imeanza kupokea faraja za msaada wa kompyuta mbili kati ya sita
zilizofikishwa mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi yao kuungua
moto na kutekeza vifaa mbalimbali vya kiofisi.
Kompyuta
hizo zilipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick,
akiambatana na wakuu wa idara wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watumishi mbalimbali
kutoka kwenye halmashauri za Same na Mwanga.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick wa pili kutoka kushoto, akimkabidhi kompyuta hizo alizopokea kwa Taasisi ya Bayport Financial Services, Katibu Tawala wake wa Mkoa, Mheshimiwa Aisha Amour.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika hafla ya kupokea kompyuta hizo, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema wamekabidhi kompyuta hizo, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Same kuungua moto.
Alisema ingawa msaada wao umekuja kabla ya ofisi hizo kuungua moto, lakini wanaamini kuwa kompyuta hizo zinaweza kupunguza adha ya watumishi wa umma kufanya kazi kwa wakati mgumu, huku zikilengwa kwa Halmashauri ya Same, Mwanga na Manispaa ya Moshi.













