https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, December 16, 2015

Kwa hili la shamba la mkonge la Kwamdulu Estate, nakubaliana na wanaosema kwamba masikini hana haki

Na Kambi Mbwana, Handeni
Wakati mwingine viongozi wetu wanashindwa kutumia busara kufanya uamuzi wenye tija kwa Taifa na wananchi wake. Angalia, nimekuja Kata ya Segera, Kitongoji cha Kwedihangala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, nilipopata taarifa kwamba wananchi wamevunjiwa nyumba zao na wawekezaji wa shamba la Mkonge la Kwamdulu Estate, linalopita katika vijiji kadhaa vya Korogwe na Handeni. Wananchi hao waliovunjiwa nyumba zao wameishi hapo tangu mwaka 1982. Shamba lenyewe halilimwi. 

Kampuni yenyewe imevunja mkataba, maana shamba ni la mkonge na wao eti wanataka walime mitiki. Kwa jinsi shamba lilivyokuwa kubwa, kampuni haitaweza kulilima lote hadi walipokuwa wananchi hao. Mwekezaji anaamuru wananchi wahame ndani ya siku 90 kwa madai wanataka kulima mitiki, wakiogopa kauli ya serikali ya kutaifisha mashamba yasiyolimwa na wawekezaji uchwara. Siku 90 zinaisha, wanatumwa vijana kuanza kuvunja nyumba za walalahoi hawa, masikini wanaoishi kwa kutumia jembe la mkono. 

Nimekuja hapa, nimeumia, haswa baada ya kusikia kwamba viongozi wa wilaya ya Handeni wamewataka wananchi hao wahame kama walivyohamia hapo. Huu ni ujinga wa karne. Ningekuwa mimi ni Mkuu wa wilaya ya Handeni, ningezungumza na mwekezaji huyo badala ya kuhamisha wakulima hao, wangewamilikisha heka japo mbili au tatu ili waendelee kulima na kujenga Taifa lao. Kitendo cha kuwataka wahame, wakiwa na mazao yao, mihogo au msimu huu wa kilimo ni kuwasumbua na kuwadhalilisha wananchi hawa. 

Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi, Diwani na viongozi wengine wa chama na serikali wanashindwa kuwa upande wa wananchi badala yao wapo upande wa mwekezaji aliyeshindwa kuilima ardhi yetu. Hii si haki. Serikali iliangalie upya suala hili. Wananchi hawa wapewe japo mwaka mmoja au miwili ili wajiandae kuhama sanjari na kuhamisha rasilimali zao. Wana watoto wanasomesha. Wameshiriki mengi ya kimaendeleo kama michango ya zahanati, shule, maabara za sekondari wakitambuliwa kama wananchi halali katika eneo hilo hilo moja. Je, serikali haikujua udhaifu huo?
Hivi msimu huu wa kilimo, hata kama wananchi hao wakihama, watakwenda wapi? Watalima wapi? Na je mwekezaji anaweza kuwafikia mwaka huu au anataka kulima vibarabara ili waonekane wanalilima shamba lote? Wahanga wananiuliza. Je, ungekuwa ni mwaka wa uchaguzi wangenyanyaswa? Nimewaambia nitawajibu siku nyingine.
By Kambi Mbwana, Mwananchi wa kawaida
0712 053949
kambimbwana@yahoo.com
Mungu ibariki Tanzania.

Wataalamu wajadili mbinu za kupambana na magonjwa ya milipuko jijini Arusha

Dokta Mwele Malecela wa Kituo cha Utafiti wa Madawa (NIMR) Tanzania akifanya mahojiano jana na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoshiriki katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama ukiwemo ugonjwa wa Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani.Warsha hiyoimeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za barani Afrika na Ulaya wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani. Warsha hiyo imeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.

Monday, December 14, 2015

Waziri Januari Makamba amtembelea ofisini kwake Makamu wa Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari Makamba, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari Makamba, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Filamu Nne Kutoka Proin Promotions zaingia kwenye kinyanganyiro cha Africa Magic Viewers Choice Awards 2016

Proin Promotions Ltd imefanikiwa kuingiza filamu zake nne katika Shindano la Africa Magic Viewers Choice Awards 2016 (AMVCA 2016) katika vipengele viwili huku Filamu zote nne zikiingia katika Kipengele Kimoja cha BEST MOVIE - EAST AFRICA filamu zilizoingia katika kipengele hiko ni  MAPENZI YA MUNGU, KITENDAWALI, MPANGO MBAYA, DADDY’S WEDDING huku filamu ya KITENDAWILI ikiingia katika Kipengele kingine cha BEST INDIGENOUS LANGUAGE MOVIE/TV SERIES – SWAHILI.
Filamu zote nne zimeingia katika kipengele kimoja zikichuana zenyewe huku mbili zikitokea nchini nyingine.
 Tunawaomba watanzania kuweza kuzipigia kura filamu hizi ili kuweza kuibuka mshindi. Jinsi ya Kupiga kura fuata tovuti hii www.africamagic.tv
Washindi wa shindano hii wanatarajiwa kutangazwa Mwakani 2016 mwezi wa 3.

Sunday, December 13, 2015

Kozi ya awali ya mafunzo ya zimamoto na uokoaji yafungwa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji, jijini Dar es Salaam

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiwa wamebeba mfano wa majeruhi wa ajali, mara baada ya kumuokoa kutoka eneo la tukio wakati wa maonyesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi hilo,yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakionyesha jinsi ya kuzima moto wakati wa maonyesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya  Sajini na Askari wa Jeshi hilo,yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.
Picha kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Ndani

Ziara za kushtukiza zashika kasi, Waziri wa Afya na Naibu wake wavaa vibwebwe

IMG_8379
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika Hospitali ya rufaa ya Amana iliyopo Ilala, Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza baada ya sherehe za kuapishwa.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Rabi Hume, Modewjiblog
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala ikiwa ni masaa machache tangu kutoka kuapishwa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Wizara hiyo. Mhe. Ummy aliwasili katika hospitali ya Mwananyamala, majira ya saa 8 mchana na kuanza kuzungumza na wananchi mbalimbali waliokuwa wamekaa eneo la hospitali hiyo kuhusu matatizo yanayowakabili pindi wanapofika hospitali hapo kupatiwa huduma ambao wengi wao walionekana kutoridhishwa na huduma wanazopatiwa wanazozihitaji.
Mmoja wa wananchi ambao alielezea kwa masikitiko yaliyomkuta pindi alipofika hospitalini hapo ni, Bi. Khadija Meso ambaye alisema kuwa walikuwa na siku tatu tangu wamefika hospitalini hapo ambapo walikuwa wamempeleka mtoto wao ambae alikuwa anaumwa lakini alikuwa hapatiwi huduma hali imeyopelekea kupoteza maisha kwa mtoto huyo. Mwingine aliyezungumza aliyejitambulisha kwa jina la Mama Madohoro alisema kuwa anashangazwa na hospitali ya rufaa kuwatoza wazee pesa licha ya sera ya afya kusema wazee na watoto chini ya miaka 5 kupatiwa bure huduma za kiafya.

Saturday, December 12, 2015

Profesa Muhongo awakalia kooni Tanesco

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Serikali imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuacha mara moja tabia ya kukata umeme bila sababu ya msingi.
Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani walipofanya ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya shirika hilo.
Mara tu baada ya kuapishwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani walifanya ziara hiyo ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuzungumza na Menejimenti ya Shirika hilo.
Profesa Muhongo alisema wananchi wamechoshwa na tabia ya shirika hilo ya kukatakata umeme bila kuwepo na sababu ya msingi ya kufanya hivyo.
“Haiwezekani kila mwaka matatizo ni yaleyale na nyie bado mpo ofisini, hili halikubaliki na halivumiliki. Ninataka tutengeneze historia ya kutatua matatizo ya umeme nchini. Umeme ukiendelea kukatikakatika lazima muondoke,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema wananchi wanahitaji umeme wa bei nafuu ili waweze kujikwamua na umasikini huku akieleza kwamba ni wakati mwafaka suala hilo likatazamwa kwani bei ya huduma ya umeme ikishuka bidhaa nyingine pia zitashuka.
Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliwataka watendaji hao kujieleza ni kwanini umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwataka waeleze wao kama Menejimenti ya Shirika hilo ni hatua zipi ambazo tayari wamezichukua kuhakikisha hali hiyo haijirudii.
Alisema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na hivyo inatakiwa kuwa na umeme wa uhakika.
Vilevile aliwataka waeleze ni kwa nini huwa wanachelewa kufika maeneo ambayo kumetokea hitilafu hali yakuwa wananchi wanatoa taarifa mara tu wanavyoona hitilafu husika.

Dj Bon Love alivyochengua jijini Dar es Salaam

Mkali wa magoma hapa nchini na nje, Dj Bon Love akifanya yake katika Usiku wa Heart & Soul uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye kiota kinachobamba zaidi hapa mjini cha Raphsody, ndani ya Jengo la Viva Towers katikati ya Jiji la Dar. Dj Bon Love na maDJ wengine wakali hukutana pamoja kwenye kiota hicho ili kukonga nyoyo za wapenda Burudani kutoka maeneo mbalimbali.Usiku huo uliwezeswa kwa Udhanimi Mkubwa wa Kilaji ya Heineken.

Baadhi ya Wadua wa Burudani wakiwepo DJ. Venture na Mwanalibeneke Haki Ngowi wakiwakilisha katika Usiku wa Heart & Soul.

Friday, December 11, 2015

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akutana na mabalozi wa Norway na Malawi

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amekutana na Balozi wa Malawi nchini Tanzania na kufanya naye mazungumzo yaliyolenga kukuza uhusiano wa nchi hizi mbili, sambamba na kuongeza tija ya maendeleo huku wakifahamishana nia ya kuwa na miradi ya pamoja itakayolenga kuongeza uhusiano wa pamoja na kupunguza changamoto zinazozikabili nchi hizi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 11, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais leo Desemba 11, 2015 amekutana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne-Marie Kaarstad ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo walizungumzia kuhusu uongezaji wa mahusiani na ushirikiano hasa katika suala la mazingira. Balozi Kaarstad ni mpya nchini Tanzania na ujio wake ameelezea kuwa unalenga katika kuongeza tija kwa nchi hizi mbili na kwamba Norway itabakia kuwa rafiki wa karibu wa Tanzania.

Mwanamuziki Robert Amarula wa Zambia kutumbuiza Dar es Salaam na Dodoma kwenye tamasha la Instagram wikiend hii

Mwanamuziki na mtangazaji wa redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula kutoka nchini Zambia (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana , kuhusu onyesho lake atakalolifanya leo  katika fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam na kesho ukumbi wa Ngalawa Pub mkoani Dodoma katika Tamasha la Instagram Party Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba ambao wamemleta msanii huyo hapa nchini kwa kushirikiana na Kampuni ya C&G Solutions na kulia ni Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.

Thursday, December 10, 2015

Makamu wa Rais Mh Samia Hassan Suluhu afungua maadhimisho ya nne ya siku ya Haki za binadamu duniani

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipunga mkono kupokea maandamano ya wananchi kwenye Viwanja vya Karimjee katika Maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Dec 10, 2015. Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Bahame Nyanduga, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kupokea maandamano ya wananchi wakati wa Maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, wakati wa mapokezi ya maandamano ya wananchi wakati wa Maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.

Droo ya pili ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" kutoka GAPCO yachezeshwa leo

Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO, Rashid Khalfan (kulia) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya pili ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayoendeshwa na Kampuni hiyo na kusimamiwa na Mkaguzi wa Michezo ya kubahatisha nchini, Abdallah Hemedy (kushoto). katikati ni Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh, Dr John Magufuli atangaza baraza lake la mawaziri, wizara nne zakosa watu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dr John Pombe Magufuli, ametangaza majina ya watu aliowateua kushika nafasi za uwaziri na unaibu waziri, huku nafasi kadhaa za wizara zikiwa bado hazijapata wahusika wake.

Ofisi ya Rais, Tamisemi, utumishi na utawala bora: Mawaziri ni George Simbachawene na Angela Kairuki, Naibu waziri Jaffo Selemani Said

Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira: Makamba na naibu wake ni Mpina
Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma
Ulemavu: Waziri ni Anthony Mavunde
Kilimo, mifugo na uvuvi: Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba, Wiliam Nashe naibu waziri

Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Edwin Ngonyani.

Fedha na mipango: Waziri bado tunamtafuta, naibu waziri ni Kijachi

Nishati na madini: Waziri ni Professa Muhongo, Naibu waziri ni Medadi

Katiba na sheria: Waziri Harisson Mwakyembe

Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Waziri ni Augustino Mahiga ambae nimemteua kuwa mbunge na kisha waziri, Naibu ni Dr Suzan Kolimba.

Ulinzi na kujenga taifa: Waziri ni Dr. Hussein Mwinyi

Wizara ya mambo ya ndani: Charles Kitwamba

Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula

Maliasili na Utalii: Waziri bado, naibu ni Ramo Makala

Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage

Elimu, Sayansi na ufundi: Waziri bado hajapatikana, Naibu ni Stella Manyanya

Afya, maendeleo ya jamii na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Hamis Andrea Kingwangala

Habari, utamaduni, wasanii na michezo: Nape Nnauye, naibu Anastazia Wambura

Wizara ya maji na umwagiliaji: Makame Mbarawa ambae nilimteua kuwa mbunge, Naibu ni Kamwene


Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Edwin Ngonyani.

Fedha na mipango: Waziri bado tunamtafuta, naibu waziri ni Kijachi
Nishati na madini: Waziri ni Professa Muhongo, Naibu waziri ni Medadi
Katiba na sheria: Waziri Harisson Mwakyembe

Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Waziri ni Augustino Mahiga ambae nimemteua kuwa mbunge na kisha waziri, Naibu ni Dr Suzan Kolimba.

Ulinzi na kujenga taifa: Waziri ni Dr. Hussein Mwinyi
Wizara ya mambo ya ndani: Charles Kitwamba
Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula

Maliasili na Utalii: Waziri bado, naibu ni Ramo Makala
Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage
Elimu, Sayansi na ufundi: Waziri bado hajapatikana, Naibu ni Stella Manyanya

Afya, maendeleo ya jamii na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Hamis Andrea Kingwangala

Habari, utamaduni, wasanii na michezo: Nape Nnauye, naibu Anastazia Wambura

Wizara ya maji na umwagiliaji: Makame Mbarawa ambae nilimteua kuwa mbunge, Naibu ni Kamwene

RC Makalla awashukuru wana Kilimanjaro kwa kujitokeza kwa wingi kufanya usafi, ataka kila Jumamosi ya mwanzo wa mwezi iwe maalum kwa usafi

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla, amewapongeza wakazi na wananchi wake katika mkoa huo kwa kuunga mkono agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli la kufanya usafi na kutunza mazingira katika siku ya Uhuru, 9 Desemba iliyoadhimishwa jana nchini kote.  
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mh Amos Makalla juu na chini mwenye miwani akishiriki kufanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru, yaliyoadhimishwa jana nchini kote.
Kwa kupitia siku hiyo, RC Makalla ameagiza wakazi wake na wananchi kuitumia kila siku ya Jumamosi ya mwanzo wa mwezi iwe maalum kwa ajili ya mwendelezo wa kufanya usafi ili kuhakikisha kwamba mkoa wao unakuwa safi.

Akizungumza jana mkoani Kilimanjaro, RC Makalla alisema kwamba wananchi wake walijitokeza kwa wingi kufanya usafi, huku akiwataka waendeleze kasi yao ya kuhakikisha kwamba mkoa wao unakuwa safi. Alisema kwa kufanya hivyo si tu mkoa wao utakuwa safi, ila hata suala la magonjwa ya miripuko linaweza kuwa hadithi kutokana na kutunza mazingira yao. “Jana nilishirikiana kwa pamoja na wananchi wangu kufanya usafi, huku nikifanya usafi soko la Memorial, Hospitali Mawenzi na Soko la Marangu.

“Pamoja na kujitokeza huko kwa wananchi, naomba suala hili liwe jadi yetu kuanzia ngazi ya kaya, mtaa, kitongoji na katika maeneo yote,” alisema. RC Makalla aliagiza Halmashauri zote kuhakikisha masoko yote yanakuwa safi na takataka zinazolewa kwa wakati, bila kusahau mitaro.

Changia damu, okoa maisha


Wednesday, December 09, 2015

Bayport yamuunga mkono Dr Magufuli kwa vitendo, yapaka rangi, yafagia shule ya msingi Hekima

Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akipaka rangi katika ukuta wa shule ya Msingi Hekima, iliyopo Tandale, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo mchana. Picha zote kwa Hisani ya Bayport Financial Services.

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na utoaji wa mikopo, jana imemuunga mkono kwa vitendo Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr John Pombe Magufuli kwa kufanya usafi, kutunza mazingira na kupaka rangi shule ya Msingi Hekima, iliyopo Kata ya Tandale, wilaya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, huku wakianza kwanza kusafisha eneo la Makao Makuu ya ofisi yao, kabla ya kuelekea hapo. 

Tukio hilo liliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bayport, John Mbaga, pamoja na zaidi ya wafanyakazi 80 kwenye taasisi hiyo inayotoa mikopo ya fedha kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, bila kusahau wajasiriamali katika mradi wao wa mikopo ya viwanja vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Shughuli hiyo Ilianza mishale ya saa tatu asubuhi ambapo Mkurugenzi huyo na wafanyakazi wa Bayport walianza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya shule hiyo, pamoja na upakaji wa rangi katika baadhi ya madarasa katika shule hiyo yenye wanafunzi zaidi 1900, ukiacha idadi kubwa ya wanafunzi wa darasa la kwanza watakaonza shule mapema mwakani.

Meneja wa Oparasheni wa Bayport Financial Serviices, Charles Mgeta, akizungumza na waandishi wa habari juu ya taasisi yao kuamua kufanya usafi, kutunza mazingira na kuipaka rangi shule ya msingi Hekima, iliyopo Kata ya Tandale, Wilaya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.



Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema kwamba wamefurahia kushirikiana na walimu na wanafunzi wa shule ya Msingi Hekima kufanya nao usafi na kutunza mazingira ya eneo la shule hiyo inayotumiwa na watoto wengi kutoka kwenye Kata hiyo ya Tandale. “Bayport ni taasisi ya Watanzania wote, wakiwamo watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, hivyo naamini itaendelea kutoa huduma bora zenye kuwakwamua wateja wetu,” alisema Cheyo.

Tuesday, December 08, 2015

UNDP wafurahia uwapo wa miradi ya kusaidia vijana Tanzania

IMG_6094
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya akiongozana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez mara tu baada ya kumpokea alipowasili ofisini kwake akiwa ameongozana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (hawapo pichani).

Na Mwandishi wetu, Kigoma
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ameelezea kufurahishwa kwake na uwapo wa mradi wa kusaidia vijana wa kitanzania kujifunza ujasirimali na kujitegemea.
Akizungumza katika shughuli za uzalishaji mali za vijana wa Shirika lisilo la kiserikali la Nyakitonto Youth Development Tanzania la mjini Kigoma alisema kwamba shughuli wanazofanya vijana hao zinamsisimua sana.  “Tunafurahi sana mimi na  wenzangu kutembelea mradi huu unaofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambao unachochea ujasirimali miongoni mwa vijana. Sote tunajua kwamba vijana wengi wa Kitanzania wanaume kwa wanawake wameelimika lakini hawana ajira rasmi. Na suala la ujasiriamali ni kitu ambachio mtu anaweza kujifunza, na ujasiriamali unatoa fursa  kwa vijana kujiunga katika kundi la wafanyakazi kwa kujiajiri wenyewe.

“Tunajua kwamba kupitia shughuli zinazofadhiliwa na ILO katika ngazi ya jamii na kwa kufuata maelekezo ya serikalai za mtaa vijana wanaanzisha biashara mbalimbali binafsi au na jamii. Kiwanda cha kutengeneza sabuni ni mfano mzuri sana. Tunaona kwamba mradi huu unawaongezea kipato na hivyo kuweza kusaidia familia zao na kupeleka watoto shuleni na kuboresha lishe . Kwa ufupi mradi kama huu unasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokabili kaya maskini Kigoma” alisema Rodriguez
ILO Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na  kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.

Monday, December 07, 2015

Rungu la Dr Magufuli latua tena Bandari, Bodi ya Bandari yavunjwa, mwenyekiti wake atimuliwa, Katibu Mkuu Uchukuzi naye afutwa kazi


HALI imezidi kuwa tete kutokana na joto kali linalozalishwa na utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli, baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusema kuwa Rais Magufuli amevunja bodi ya Bandari na ametengua nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi Profesa Joseph Msamichaka. 
Pia amefukuza kazi watendaji wote waliohusika na kupokea na kutoa makontena kwenye bandari kavu ICD' pamoja na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka baada ya kushindwa kusimamia fedha za TRL kiasi cha Sh Bil 16.

Jamii ya Kimataifa yaombwa kusaidia huduma kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma


IMG_6503
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na ujumbe wake aliombatana nao Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (kushoto) kabla ya kuelekea kambi ya Nyarugusu walipita ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita kumsalimia pamoja na kusaini kitabu cha wageni. Picha zote na Zainul Mzige.

Na  Mwandishi Wetu, Kigoma
JUMUIYA ya Kimataifa imekumbushwa kuisaidia Tanzania katika kuhudumia wakimbizi kutoka Burundi na Kongo ambao wanaishi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kukamilisha ziara yake mkoani Kigoma. Alisema kwamba serikali ya Tanzania kwa miaka mingi imekuwa na moyo wa huruma wa kusaidia majirani zake kwa kuhifadhi wakimbizi na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuona hilo na kusaidia Tanzania kufanikisha  hifadhi ya wakimbizi.

Alisema Umoja wa Mataifa umekuwa ukishuhudia namna ambavyo serikali ya Tanzania inahudumia wakimbizi na kuridhika na hata pale ilipowapatia haki za kuwa Watanzania kwa kuwapa uraia na pia kusaidia kuwarejesha makwao wakati hali ilipokuwa njema.
Hata hivyo amesema kwa sasa hali ya Burundi na Kongo si njema na hivyo Watanzania kupata tena kazi yakuhifadhi wakimbizi. Alisema Tanzania kwa huruma yake imetoa ardhi zaidi ili kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kusaidia kukamilisha makazi hayo mapema kabla ya  mvua za masika ili wananchi hao waweze kuishi kwa amani.
IMG_6505
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita akimsikiliza kwa makini Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.

Alisema kambi ya Nyarugusu ni ya tatu kwa ukubwa duniani  na inahifadhi zaidi ya wakimbizi 150,000 wakiwemo watoto na wanawake na wanahitaji huduma za shule, afya, maji na mengine. Aidha wanahitaji nishati na hali hiyo haiwezi kuwezeshwa na serikali ya Tanzania pekee kwani watakuwa wakielemewa na huruma yake na moyo wa upendo kwa majirani zake.

Chuo Kikuu cha Ushirika MoCU chafanya mahafali ya kwanza mjini Moshi

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi  (MoCU) Pius Msekwa akitunuku Shahada, Stashahada na Astashahada kwa wahitimu wa Chuo hicho wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho.
Wahitimu wa kozi mbalimbali waliohitimu katika Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi,(MoCU).

Friday, December 04, 2015

TRA yawabana wafanyabiashara wakwepa kodi, wafanyakazi 35 watimuliwa

Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Philip Mpango (Kulia)akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa ya upatikanaji wa makontena 43 pamoja na malipo ya kodi ya Zaidi ya shilingi bilioni tano kutoka kwa wakwepa kodi,kushoto kwake ni kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Bw.Lusekelo Mwaseba.
LU2
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Bw.Lusekelo Mwaseba(Kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Philip Mpango.

Thursday, December 03, 2015

RC Makalla akunwa na matokeo mazuri ya darasa la saba wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro

 RC Kilimanjaro awa mgeni rasmi halfa ya walimu Hai, akunwa na ufaulu mzuri wilayani humo

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, akiwa ameshika glasi ya kinywaji kwa ajili ya kufurahia kwa pamoja kwenye hafla ya kuwapongeza walimu wa wilaya ya Hai mkoani humo baada ya kupata matokeo mazuri katika ufaulu wa darasa la saba mwaka huu. Hai imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya mkoani humo na nafasi ya nne kitaifa.

Na Mwandishi Wetu, Hai
MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amehudhuria halfa ya kuwapongeza walimu wilayani Hai, mkoani humo, kwa kufanikisha ufaulu mzuri wa darasa la saba. Wilaya ya Hai imepata nafasi ya kwanza kiwilaya mkoani Kilimanjaro, huku ikishika ikishika nafasi ya nne kitaifa, jambo lililomkuna Mkuu huyo wa Mkoa Kilimanjaro. 
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makalla, mwenye suti nyeusi akiingia katika hafla hiyo, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza katika halfa hiyo akiwa kama mgeni rasmi, RC Makalla, alisema kwamba Hai wanastahili pongezi na wanapaswa kuendelea kufanya bidii ili wazidi kufaulisha kiwilaya na kitaifa. Alisema kuna haja ya sekretarieti ya Mkoa huo na Halmashauri zote kujipanga na kushughulikia kero za walimu, madai ya mishahara, kupandishwa kwa madaraja pamoja na kujibu barua zao kwa wakati ili kuwapa moyo walimu wao hao.

Mabondia Francis Cheka na Thomas Mashali kuzipiga Morogoro Desemba 25

Mabondia Fransic Cheka kushoto na Thomas Mashali wakiangaliana kwa usongo wakati wa kutambulisha mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro. Picha na SUPER D BOXING NEWS


 Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakitambiana mbele ya wandishi wa habari wakati wa kutambulisha mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro. Picha na Suped D

Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Thomas Mashali wa Dar es salaam na Fransic Cheka wa Morogoro wamendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro uzito wa kg 76
akiongea na waandishi wa habari Mashali amesema kuwa hii ni vita ya Dar na Moro  hivyo kawaomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi wa Dar es salaam waweze kuhamia morogoro kwa muda kwa ajili ya kumsapoti
siku hiyo ambayo kwake atakuwa na kibaruwa kigumu ambapo atapigana na Cheka pamoja na wakazi wa Morogoro.

Bondia Chaka alijibu mapigo hayo kwa kusema siku zote anamweshimu bondia anaetaka mpambano wa marudiano hata hivyo dozi ya mashali ipo pale pale na nitampiga katika raundi za awali tu kwa kuwa nipo vizuri na naendelea na mazoezi.

Nae kocha wa Mashali Ramadhani Uhadi amesema kuwa cheka ni bondia wa kawaida sana hivyo wapenzi waje waone mchezo mzuri utakaochezwa na Mashali atakavyo msambalatisha Cheka siku hiyo mjini Morogoro
na kocha wa bondia Cheka Abdallah Salehe amesema Cheka yupo vizuri sana kwa sasa nimempika ameshaiva ata kama mpambano utakuwa leo Mashali atapigwa mapema sana.

Katika mpambano huo kutakuwa na mipambano mingine ya bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atapambana na Twaha Kassimu kg 63 na Vicent Mbilinyi kg 63 atakumbana na Deo Njiku wakati Pius Kazaula kg 66 atamenyana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha mabondia Epson John  kg 57 na Sadiq Momba na wana dada Lulu Kayage kg 51 atapambana na Mwanne Haji kugombania ubingwa wa taifa.





Meli ya MV Mapinduzi II yawasili kwa kishindo Visiwani Zzanzibar

Meli Mpya ya MV Mapinduzi 2 ikiwasili Zanzibar ikitokea Nchini Korea.

Wednesday, December 02, 2015

RC Makalla atembelea kiwanda cha sukari TPC, akerwa na sukari inayoingia kwa wingi kutoka nje

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makalla akiwa kwenye ukaguzi wa kiwanda cha sukari cha TPC kilichopo Moshi, mkoani humo, kama sehemu ya kuangalia hali ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho. Picha na Mpigapicha wetu.

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara katika kiwanda cha Sukari cha TPC kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro ili kujionea hali ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho. RC Makalla alijionea hali halisi ya kiwanda hicho ambacho sasa kinazalisha sukari tani 105,000 baada ya kubinafsishwa, tofauti na uzalishaji wa tani 35,000 tu hapo zamani.
 Ziara inaendelea kiwandani hapo.
Akizungumza katika kiwanda hicho, RC Makalla alisema kwamba amefurahishwa na hali ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho, huku akiahidi kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Tanga kudhibiti sukari inayoingia kutoka nje ya nchi. Alisema atashirikiana na serikali ya Mkoa wa Tanga kudhibiti sukari hiyo ya nje, akiamini kuwa kutasababisha kiwanda hicho kupiga hatua kwa kuuza sukari yao nchini.

UN, Serikali wapongeza wananchi wa Singida kufanya juhudi za kujiletea maendeleo

IMG_4100
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na mmoja wa watendaji wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida mara tu alipowasili kijiji cha Puma kukagua mradi wa ufugaji kuku wa kusaidia watu wanaoishi na VVU unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia TACAIDS. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone.

Na Mwandishi Wetu, Singida
MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja huo (UNDP), Bw.Alvaro Rodriguez ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira yanayofanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo endelevu. Mratibu huyo alitoa wito huo wakati alipofanya ziara ya siku mbili mkoani Singida kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa. Baada ya kuona mafanikio katika miradi hiyo Bw. Rodriguez, alisifu pia jamii ya Singida kwa kujitoa kuhakikisha kwamba wanafanikisha miradi hiyo kwa kuifanya kuwa miradi yao.

Katika ziara hiyo ambapo pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha ushirikiano wa kimataifa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, Bi. Maulidah Hassan walikuwepo, Mratibu alitembelea kituo cha watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi; Kituo cha kutibu kipindupindu na Ushirika wa wajasiriamali vijana.
Miradi hiyo inafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi (UNAIDS). UNAIDS ni mshirika wa karibu wa serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya UKIMWI kupitia mashirika ya TACAIDS na ZAC.

Tuesday, December 01, 2015

Ray Mboya ashinda umeya Manispaa ya Moshi kwa kofia ya Chadema


Msimamizi wa Uchaguzi wa nafasi ya Meya ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Makabayo akizungumza jambo wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Baadhi ya Madiwani walioshiriki zoezi la kumpata Meya wa manispaa ya Moshi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Meya wa Manispaa ya Moshi aliyemaliza muda wake na Mbunge wa sasa wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Hotel ya Umoja.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...