https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, August 20, 2015

Rais Kikwete aagwa, Magufuli atambulishwa Diamond Jubilee

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahma Kinana alipokuwa anawasili kwenye hafla ya kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Jumatano Agosti 19, 2015
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg Philip Mangula alipowasili kwenye hafla ya kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Jumatano Agosti 19, 2015.
  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Mhe Saidi Meck Sadick alipowasili kwenye hafla ya kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Jumatano Agosti 19, 2015
  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova  alipowasili kwenye hafla ya kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Jumatano Agosti 19, 2015
  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli. 
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mgombea mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan  
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT Mhe Sophia Simba
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Masaburi
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa jiji la Dar es salaam Dkt Masaburi
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wana CCM
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkereketwa wa CCM
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wakereketwa wa CCM
 Sehemu ya umati wa maelfu ya wananchi wa Dar es salaam kwenye hafla ya kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Jumatano Agosti 19, 2015
  Sehemu ya umati wa maelfu ya wananchi wa Dar es salaam kwenye hafla ya kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Jumatano Agosti 19, 2015
 Kila mtu alikuwa na kamera yake ya simu kurekodi hafla ya kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Jumatano Agosti 19, 2015
 Wabunge watarajiwa wa Dar es salaam 
 Sehemu ya umati
 Sehemu ya umati

 Sehemu ya umati

 Sehemu ya umati

 Nyomi ya wana CCM wa Dar es salaam
 Nyomi ya wana CCM wa Dar es salaam
 Nyomi ya wana CCM wa Dar es salaam
 Nyomi ya wana CCM wa Dar es salaam
 Mikono juu
 Nyomi ya wana CCM wa Dar es salaam
 Nyomi ya wana CCM wa Dar es salaam
 Nyomi ya wana CCM wa Dar es salaam
 Wanahabari kazini
 Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM Ndg Ramadhani Madabida akisalimia umati
  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimia umati
  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea
 Msanii nyota wa Bongo Fleva Inspekta Haroun alikuwepo pia
Nyomi
 Wana CCM kila pembe ya ukumbi
 Diwani Kitwana Manara Popat na wajumbe wenzie
 Wabunge wa Dar es salaam
  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kuongea
  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo
  Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha mgombea mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan
 Mgombea mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan akisalima wananchi
 Mgombea mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan akiongea
 Pongezi kwa Mgombea mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan 
 JK akimualika Dkt Magufuli
 Mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisalimia umati
 Mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisalimia umati
 Mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiongea
 Mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisalimia umati
 Mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisalimia umati
 Pongezi kwa mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli baada ya kuogea 
 Meza kuu
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Dkt Magufuli  na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana 
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Dkt Magufuli  na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana 
 Mwenyekiti wa wazee wa Dar es salaam akiongea 
 Mwenyekiti wa wazee wa Dar es salaam akiongea 

 Mwenyekiti wa wazee wa Dar es salaam akipongezwa na Dkt Magufuli
 Mwenyekiti wa wazee wa Dar es salaam akipongezwa na mgombea mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan
 Meza kuu
Kwaherini na asante sana

Tuesday, August 18, 2015

Bayport yaanzisha huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj

Mratibu wa Bima kutoka Bayport Financial Services, Ruth Bura, katikati akizungumza katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari, pikipiki na Bajaj kwa kushirikiana na Kampuni ya NIKO Insurance. Kulia ni  Meneja Uendelezaji wa Biashara wa  NIKO Insurance, Jabir Kigoda na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Niko, Mannaseh Kawoloka.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo, imezindua huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj, ikiwa na lengo la kurahisisha masuala ya usafiri kwa wateja wao ili kukwamua zaidi. Kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya kumetajwa kuwa kutachangia kwa kiasi kikubwa wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri waliokuwa wakishindwa kulipa bima kwa wakati na wakati mwingine mteja kupata ajali hali ya kuwa hana huduma ya bima inayoweza kumlinda.
Oparesheni Meneja wa Bayport Financial Services, Charles Mgeta, kushoto akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari, pikipiki na bajaj. Anayefuata ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance, Mannaseh Kawoloka.
Afisa Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance, Mannaseh Kawoloka katikati akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj inayoendeshwa na Taasisi ya Bayport Financial Services. Kulia kwake ni Mratibu wa bima hiyo, Ruth Buran a kushoto kwake ni Meneja Oparesheni wa Bayport, Charles Mgeta. Picha zote na Mpiga Picha Wetu. 

Friday, August 14, 2015

NHIF wawapa somo wadau wa blog juu ya masuala ya bima ya afya

 
 MKURUGENZI wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti, akifafanua jambo wakati alipokuwa akiwasilisha mada juu ya mpango wa uchangiaji binafsi, KIKOA, wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NHIF, na Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN).Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Bloggers wakimsikiliza  Mkurugenzi wa huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti, alipokuwa akiwasisilisha mada iliyohusu mpango wa uchangiaji binafsi, KIKOA kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NHIF na Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN).Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini Dar es Salaam.

Wednesday, August 12, 2015

Kura za maoni jimbo la Handeni zazidi kuwaka moto

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HALI imezidi kuwa tete katika Uchaguzi wa kuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea Ubunge, Jimbo la Handeni, wilayani Handeni, mkoani Tanga, baada ya kubainika mapendekezo yaliyofikiwa na Kamati ya Siasa na Maadili hayajafikishwa kwenye Kamati Kuu, kwa sababu ya kuwabeba baadhi ya wagombea waliokuwa kwenye mchakato huo.
Wagombea wa Ubunge CCM jimbo la Handeni, Dr Seif Mhina, John Salu, Chifu Msopa, Mboni Mhita, Ahmed Bwanguzo, Ramadhan Mahiza na Kambi Mbwana mwenye koti, walipokuwa kwenye kampeni hizo Handeni.

Katika matokeo yaliyotangazwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Handeni, Salehe Kikweo, yalionyesha kuwa mgombea John Salu, aliongoza, lakini alikiri kuwa hayo si matokeo halisi kwa sababu kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa kanuni pamoja na wagombea watano kupita njia za panya, vikiwamo vitendo vya rushwa kwenye mchakato huo wa Ubunge Handeni.

Akizungumza kwa hisia kali, mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, Ramadhan Mahiza, aliuambia mtandao huu kuwa ofisi ya CCM Handeni, imeidanganya Kamati Kuu, chini ya mwenyekiti wake wa CCM Taifa, Mh Jakaya Mrisho Kikwete, kutokana na ripoti na mapendekezo ya vikao halali kutofika mezani kwa ajili ya kujadiliana juu ya kumpata mtu anayekubalika kwa wananchi wote.

Alisema katika mchakato huo wa ubunge Handeni, wapo wagombea walioguswa moja kwa moja kutoa rushwa na kugawa madera ambayo waliokamatwa walikiri, hivyo suala hilo kumalizwa kwa kutoa mapendekezo ya kuwaengua wagombea watano wa nafasi hiyo ya ubunge Handeni.

Saturday, August 08, 2015

Picha mbalimbali za sherehe za wasanii wakimuaga Rais Kikwete

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  Mhe Paul Makonda alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. John Pombe Magufuli alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe January Makamba  alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Ruge Mutahaba, mratibu mkuu wa hafla  alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na wasanii  alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambako Wasani wa fani mbalimbali waliandaa hafla rasmi ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015

UTT-PID wakifanya yao kwenye maonyesho ya nane nane mkoani Lindi

Maafisa Masoko wa UTT-PID, Bi Kilave Atenaka (katikati) na  Bi. Mary Minja (kwanza kulia) wakiongea na mteja aliyefika banda lao lililo chini ya wizara ya Fedha katika Maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

Global Link Education watoa semina ya wanaokwenda kusoma India na China

Mkurugenzi wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Abdulmaliki Mollel akitoa maelezo katika semina ya kuwajengea uwezo wazazi na wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya India na China leo katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, David Nsimba akitoa semina ya kuwajengea uwezo wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya India na China leo katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Thursday, August 06, 2015

Zoezi la uandikishaji wapiga kura BVR lakamilika

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kukamilika kwa zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu kwa kutumia mfumo wa BVR Mkoani Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani zoezi hilio limefanikiwa kwa kiasi kikubwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizojitokeza.

Wednesday, August 05, 2015

Wakazi na wananchi wa Mbweni JKT wilayani Kinondoni wamuomba DC Paulo Makonda apige jicho mradi wa daraja uliokwama

 
Licha ya mtaa wa Mbweni JKT, jijini Dar es Salaam kujengwa majumba ya kifahari na kupatikana pia nyumba za viongozi mbalimbali wa serikali, miundo mbinu yake, hususan daraja linalojengwa katika eneo hilo ili kuwafanya wananchi wapite kwa urahisi kusua sua. Kwa miaka kadhaa sasa ujenzi wa daraja hilo umesimama. 

Pichani ni gari la mwananchi na mkazi wa eneo hilo akipta kwenye maji ambayo mara kadhaa hujikuta wamesimama kwa saa kadhaa, hususan kama eneo hilo litajaa baada ya eneo hilo kujaa maji yanayotoka baharini.

 Hali hiyo si tu inakwamisha maendeleo, pia ni hatari kwa usalama wa wananchi kwenye eneo hilo. Wananchi wengi wameonekana kuichoka hali hiyo na kuiomba serikali kulifanyia kazi daraja hilo ili kuwafanya wananchi waingie na kutoka bila usumbufu wowote kama unaotokea wakati huu.
Kambi ya JKT Mbweni ikiwa tulii. Ujenzi wa daraja hilo umekwama. Wananchi hawajui ujenzi huo umekwamia wapi. Baadhi ya wananchi waliozungumza na mtandao huu walimuomba Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paulo Makonda na Mkurugenzi wake kuangalia namna gani mradi huo umesimama kwa miaka mitatu sasa.
Linaloonekana nyuma ya kibao cha tangazo la Halmashauri ni daraja linalojengwa kwenye eneo la Mbweni JKT ambalo hata hivyo limesimama na kuleta adha kubwa kwa wakazi na wananchi wa eneo hilo kwa miaka mitatu sasa. Wananchi hao wameendelea kutaabika hasa sehemu hiyo inavyopokea maji mengi kutoka baharini kila wakati. Picha zote za Mpiga Picha Wetu.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...