Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Mwanza
MAUAJI ya albino yameendelea kushika kasi katika viunga mbalimbali vya nchi yetu, zaidi yakitokea pia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa, kama vile Mwanza, Geita na maeneo ya jirani.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir akizungumza na Ester Jonas, aliyelazwa Hospitali ya Bugando aliyejeruhiwa kufuatia tukio la uporwaji wa mtoto wake Yohana Bahati. Kulia kwa Mbunge ni Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, akiwa na watumishi wengine  wa taasisi hiyo jijini Mwanza.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyri (katikati), akizungumza na binti aliyekutwa nyumbani kwa Ester Jonas, mama wa albino Pendo Bahati aliyeporwa na haijulikani alipokuwa. Kulia kwake ni Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services, Lugano Kasambala, aliyeambatana na mbunge huyo.

Kutokea kwa mauaji hayo si tu yanazua hofu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), bali pia huichafua nchi yetu inayoaminika Tanzania ni kisiwa cha amani kulinganisha na
nchi nyingine Barani Afrika.

Leo hii watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa na wasiwasi mkubwa wa uhai wao, licha ya kuwa na mapenzi makubwa na Taifa lao. Wakati hofu hiyo ikigubika nyuso za watu hao,

mashirika mbalimbali na viongozi wote wa serikali wamekuwa.

Miongoni mwa mashirika hayo ni Bayport Financial Services, taasisi ya kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo nchini Tanzania. Taasisi hii kwa kushirikiana na mbunge wa Viti Maalum, Al Sheimar Kweigyir, walifanya ziara katika Mkoa wa Mwanza, ili kujionea hali ya matukio ya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Katika ziara hiyo, Bayport na Mbunge Shaimar walimtembelea Ester Jonas, mama wa Yohana Bahati anayepata matatibabu katika Hospitali ya Bugando, jijini Mwanza, kufuatia

kujeruhiwa na watu waliompora mtoto wake huyo na kusababisha kifo chake.

Aidha, Bayport pia walimtembelea Sofia Juma, mama wa Pendo Emmanuel, albino aliyetekwa mkoani Geita na hadi leo haijulikani kama yupo hai au amekufa, licha ya Jeshi la

Polisi kutangaza kuwashikilia baadhi ya watu waliodaiwa kuhusika na tukio hilo la uporaji wa mtoto.

Akizungumzia safari hiyo, Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, anasema kwamba wameguswa na kuumizwa na matukio ya mauaji ya albino yanayoendelea kutokea hapa nchini.