https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, July 05, 2014

Mbeya City: Tumeanza mazozi rasmi



NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa timu ya Mbeya City, Juma Mwambusi, amesema kwamba wameanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na Ligi ya Tanzania Bara msimu ujao utakaoanza baadaye mwezi ujao.

Jana jijini Mbeya, timu hiyo iliyomaliza ligi kwa kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi inaingia uwanjani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Prisons, zote za jijini humo.
Akizungumzia mazoezi hayo, Mwambusi alisema kwamba ameanza rasmi patashika ya kuandaa timu yao kwa ajili ya kujiandaa na Ligi ijayo.

Alisema wanaamini mazoezi yao yatakuwa na tija juu ya kuiweka sawa Mbeya City ili ijiweke katika mazingira mazuri ya kiushindani. "Naamini huu ni wakati wa kuiandaa vyema Mbeya City ili msimu ujao uanze kwa mafanikio na hatimae vijana kufanya vizuri uwanjani.

“Tumeanza rasmi mazoezi, huku tukijipanga kuwapatia burudani kamili ya soka wakazi wa Mbeya na Tanzania kwa ujumla,” alisema Mwambusi.
Mkoa wa Mbeya sasa umepata ushindani wa kisoka, huku timu za Mbeya City na Prisons zikiingia katika ushindani wa aina yake, kama timu pinzani.

Dickson Samwel Mbiling'i anatafutwa na Ndugu zake

Jina: Dickson Samwel Mbiling'i

Umri miaka 27

Kabila: Mkinga

Dini: Mkristo

Maeneo anayopenda kutembelea:

Iringa, Mbeya, Dar es Salaam na Bagamoyo.

Mtajwa hapo juu anatafutwa na ndugu zake. 
Kwa mara ya mwisho alionekana nyumbani kwake Mwananyamala Mchangani jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano ya  Julai 2, 2014.

Wajihi wake ni maji ya kunde mrefu kiasi mwembamba wa wastani. Msamaria mwema yeyote mwenye taarifa zake au atakayemuona popote anaombwa kuwasiliana na ndugu zake kwa namba:-

0754 477226-Moses Mbiling'i

0754 301095-Adrew Mwilingu

0757 000014-Bartholomew Mbiling'i

0784 890389-Ahadi Kakore.

Wadau waaswa kujifunza huduma za Twiga Bancorp kwenye maonyesho ya sabasaba

Pichani ni  Meneja wa Tawi lililopo ndani ya  maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar,Bi. Upendo Tendewa akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki hiyo.Bi.Upendo amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kukidhi mahitaji ya wateja ya kibenki na ya kifedha kwa kuhakikisha upatikanaji wa bidha na huduma bora kabisa katika soko  kwa bei inayowezekana kulipa na viwango  vyenye manufaa yanayolingana na gharama na faida ya kurudhisha kwa mwanahisa.

Amesma benki hiyo inatumia kadi yako iitwayo Twiga ExpressCard ambayo mteja anaweza kuitumia kupata huduma za kibenki katika ATM yoyote iliyounganishwa na mtandano wa UMOJA SWITCH,ambapo zaidi ya ATM 180 na mabenki ishirini nna nne nchini yameunganishwa.
 Afisa Masoko wa Benki ya Twiga Bancorp Bwa.Adalbert Alchard akizungumza na Wanahabari nje ya banda lao kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kwa wateja wao, kwenye maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar.Pichani kushoto ni  Afisa wa Benki hiyo,Bi Tuddy Lutengan.

Friday, July 04, 2014

Msikiti wa Bakheressa wazinduliwa

 Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akikata utepe kuzindua rasmi Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliojengwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Said Salim Bakhresa  katika eneo la Uwanja wa Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti huyo wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa, ambapo pia uzinduzi huo uliofanyika leo Julai 4, 2014, ulihudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Kiserikali akiwemo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wengineo. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokelewa na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa, wakati alipowasili Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa msikiti huo uliofanyika leo Julai 4, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ( wa pili kuli) Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa (katikati) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto) wakijumuika na waumini wa dini ya Kiislam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkititi wa ‘Masjidil Huda’ na Swala ya Ijumaa uliofanyika leo Julai 4, 2014, Chamaz jijini Dar es Salaam.

DRFA yaipongeza Simba, Aveva kuchaguliwa kwa kishindo


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimeipongeza klabu ya Simba kwa kufanya uchaguzi wa amani na kupata viongozi wake wapya watakaoingoza kwa miaka minne.



Mwenyekiti wa DRFA Almas Kassongo, amema kuwa wana imani na uongozi huo mpya wa Rais Evans Aveva, Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na Kamati yake ya utendaji.



“Sisi DRFA tunawapongeza viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza klabu ya Simba kwa kipindi cha miaka minne, katika uchaguzi uliofanyika Juni 29 mwaka huu katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Pilisi, Osterbay.



“Tunaamini kuwa wanachama waliowachagua viongozi hao wana imani nao na wataweza kuiongoza klabu hiyo kufikia mafanikio,” alisema Kassongo.



Alisema DRFA itakuwa tayari kufanya kazi na kushirikiana kwa karibu na uongozi huo katika kipindi chote cha uongozi wao na kuwataka kudumisha amani na utulivu ndani ya klabu hiyo.



Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Colin Fish, Jasmine Sudi, Said Tuli, Idd Kajuna na Ally Sum.

Safari ya Humud Sopafaka yapata baraka



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KIUNGO wa zamani wa Simba aliyekatisha mkataba wake Abdulhalim Humud, ataanza rasmi kuitumikia klabu yake mpya ya Sofapaka ya nchini Kenya keshokutwa, baada ya kupata hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC).

Humud ambaye kipaji chake soka kilianza kuonekana akiwa na timu ya Mtibwa ya Sugar ya Morogoro, yupo tayari kwa ajili ya kuanza rasmi maisha mapya ya kutumikia Sofapaka ya nchini Kenya, baada ya kumalizana na klabu hiyo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Humud alisema amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuichezea Sofapaka, baada ya timu hiyo kuonyesha nia ya kumuhitaji  kwa muda mrefu ili kutumikia klabu hiyo nchini Kenya.

Alisema kuwa Sofapaka kwa sasa ipo katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Kenya, huku akiamini klabu hiyo itamuwekea mazingira mazuri ya kuonyesha soka la aina yake ndani ya timu hiyo.

“Mimi nashukuru mungu kwa kila jambo nimekuwa nikikutana na mitihani mingi, lakini mungu amenipa ujasiri na kuishinda sasa hivi nimesajili na Sofapaka, nimekuja kuaga kwa ajili ya kurudi nchini Kenya kuanza kuitumikia klabu yangu hii.

Uhondo wa Skylight Band kuendelea jijini Dar es Salaam

1
Kijana Machachari wa Skylight Band Hashim Donode (kushoto) akilianzisha taratibuuuu Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village akipewa Sapoti na Sony Masamba. Sasa mashabiki na wapenzi wa Skylight Band kila wiki wanashindanishwa kucheza staili yao matata ya "Kikuku na washindi hupewa ofa ya kulipiwa vinywaji, kiingilio na usafiri. Mwanzo ilikuwa Ijumaa iliyopita ambapo washindi walipewa ofa hiyo pamoja na kuhudhuria show yao kali iliyopigwa ndani ya Dar Live.
2
Meneja her self ...Aneth Kushaba akiimba kwa hisia kali Ijumaa iliyopita. 3 Chezea Meneja weweeee ni kazi na furaha ya kutosha ndani ya Skyligt Band hapo akifurahia sauti yake tamuuuuu ya wapigaji vyombo wa bendi hiyo.

Thursday, July 03, 2014

Mwanamichezo Sean Garnier aatua Tanzania

 Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn's John Ntuli (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo. Pembeni ni Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo akifafanua machache mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa. Pembeni yake kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn's John Ntuli na Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi.

Wednesday, July 02, 2014

Aveva kukabidhiwa ofisi Julai 8

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KLABU ya Simba, inatarajia kumkabidhi ofisi rais mpya wa klabu hiyo, Evans Aveva, Julai nane mwaka huu, sambamba na kuanika mambo yote, ikiwamo Milioni 420 zilizotajwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage.

Siku ya Uchaguzi Mkuu, Rage alitangaza kwa waandishi wa habari kuwa anaondojka madarakani huku akimuachia rais mpya Sh Milioni 420, jambo ambalo limepokewa kwa hisia tofauti na wadau na mashabiki wa soka.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kwamba kwa sasa taratibu za ofisi hiyo zinaandaliwa kwa ajili ya kumkabidhi Rais huyo ofisi kw ajili ya kuongoza baada ya kuchaguliwa kwa kishindo na wanachama wake.

Alisema kuwa anaamini pamoja na Milioni 420 zilizotajwa na mwenyekiti Rage, Simba pia ina mambo mengi ambayo kisheria lazima yaandaliwe kwa ajili ya kumpa mwanga wa utendaji wake kwa maendeleo ya klabu yao.

“Makabidhiano rasmi ya ofisi yamepangwa kufanyika Julai nane ambapo taratibu zote zitawekwa hadharani ili kuongoza kwa miaka minne baada ya kuchaguliwa na wanachama wake Juni 29.

“Kuhusu hizo Milioni 420, ni vyema pia wadau wakasubiria siku hiyo ya makabidhiano kwasababu kila kitu kitawekwa hadharani ili kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda sawa na kuiletea maendeleo klabu yao,” alisema Kamwaga.

Aveva ndio rais wa kwanza wa klabu hiyo tangu Katiba ya Simba iliposajiliwa na kuondoa neno mwenyekiti na kutambulika kama Rais, akirithi mikoba ya Rage, huku wanachama wengi wakiwa na imani naye.

Lowassa aliposhiriki Jubilei ya miaka 25 ya Uaskofu wa Tarcisius Ngalalekumtwa

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,Mhashamu Severini Niwemugizi  wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.

Tuesday, July 01, 2014

Shindano la urembo la Qs lawekewa mikakati


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Qs Mhonda J  Entertainment, imesema inaweka mikakati kabambe ili shindano lao la urembo la Qs Queen linafanyika kwa mafanikio.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Joseph Mhonda, alisema kwamba mipango hiyo inakwenda sambamba na hamu ya kuona tasnia hiyo ya urembo inapiga hatua.

Alisema lengo la kuanzisha kwa shindano hilo ni kutafuta fursa za ajira mpya kwa mabinti watakaoshiriki shindano hilo lenye tija kwa watu wote.

“Shindano la Qs Queen lilifanyika mwaka jana, lakini likasimama kwa muda, hivyo nia yetu ni kujipanga ili lifanyike tena kwa mafanikio makubwa.

“Naamini wadau wote wanatumia wakati huu kuweka mikakati ya aina yake ili shindano lifanyike kwa mafanikio makubwa, licha ya changamoto mbalimbali kujitokeza,” alisema Mhonda.

Kampuni hiyo inajihusisha na kazi mbalimbali, ikiwamo kuwasimamia wasanii nyota, akiwamo Ney wa Mitego, H Baba na wengineo wanaotamba Tanzania.


Simba wanahitaji maendeleo, si malumbano tena



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Juzi Juni 29, klabu ya soka ya Simba ilifanya uchaguzi wake mkuu baada ya mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage, kumaliza muda wake wa miaka minne wa kuongoza.
Evans Aveva, pichani
Katika uchaguzi huo watu mbalimbali walijitokeza kuchukua fomu za kugombea uongozi kwenye klabu hiyo. Nafasi za juu za uongozi zilikuwa ni rais ambapo Evans Aveva alikuwa akichuana na Andrew Tupa na makamu wa rais ilikuwa ikigombewa na Geofrey Nyange Kaburu, Jamhuli Kihwelo ‘Julio’ na Swed Mkwabi. 

Sitaki kusema nani aliibuka kidedea katika kinyang’anyiro hicho ila kuwakumbusha wanachama wote na viongozi wapya walioingia madarakani kusimama kwenye ukweli, kuwa Simba haina maendeleo licha ya kuasisiwa miaka 1936.

 Hii ni aibu kubwa kwa klabu kama hii. Nilibahatika kutembelea maeneo mbalimbali kusikiliza kampeni za wagombea, hususan Temeke, Ilala na Kinondoni, ambapo kampeni zilifanyika katika Ukumbi wa Urafiki na kuhudhuriwa na watu wengi sana. 

Kila mmoja alikuwa akijaribu kuonyesha cheche zake juu ya nafasi anayogombea. Wote walionyesha wana kitu cha kufanya. Hata hivyo, mara nyingi mtu anapotaka jambo lake hutumia ufundi mwingi kuomba kura ikiwezekana hata kuongopa. 

Kamishina wa Polisi jamii atembelea wilaya ya Same

Kmishana wa Polisi Jamii nchini Musa Ali Musa akikaribishwa wilaya ya Same ambako ametembelea na kufanya ukaguzi kujionea hali ikoje ya namna asakari wanaposhirikiana na jamii pamoja na dawati la jinsia.
Kamishna Musa akikaribishwa kufanya ukaguzi katika Gwaride lililoandaliwa na sakari Polisi wilaya ya Same.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...