https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, April 24, 2014

Serikali yapiga marufuku wnasiasa kwa timu ya Mbeya City



Na Pendo Fundisha, Mbeya.
SERIKALI Mkoani Mbeya imepiga marufuku itikadi za kisiasa katika uendeshaji wa timu ya soka ya Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ili kulinda uhai wa timu hiyo.

Uamuzi huo umefikiwa  kufuatia baadhi ya wanasiasa kuanza tabia ya kujinadi kuwa mafanikio ya timu ya Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya yametokana na juhudi zao na vyama vyao vya siasa.

 Katibu Tawala wa mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja, aliyasema hayo kwenye hafla ya kuwapongeza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu ya Mbeya City iliyoambatana na kuivunja rasmi kambi ya timu hiyo baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara huku timu hiyo ikifanikiwa kushika nafasi ya tatu.

Mtunguja, alisema tayari baadhi ya wanasiasa mkoani hapa wameanza kuyahusisha mafanikio ya timu hiyo na harakati zao za kisiasa za vyama vyao hali ambayo ni hatari kwa uhai wa Mbeya City katika ulimwengu wa soka nchini.

Alisema, tabia hiyo inaweza kuwagawa mashabiki wa timu hiyo kutokana na kwamba kila mmoja ana mapenzi na chama chake cha siasa hivyo kuingiza itikadi kwenye uendeshaji kutasababisha ubaguzi baina yao.

“Wanasiasa watuache, wasituvuruge baada ya kuona mafanikio yaliyopatikana sasa wanataka kujiingiza katika timu, watatuulia timu yetu.” alisema Mtunguja.

Kufuatia mafanikio ya timu hiyo, Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, alisema Halmashauri ya jiji hilo imeamua kuboresha mishahara ya wachezaji ili kuzuia uwezekano wa kurubuniwa na timu kubwa kwa kigezo cha maslahi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mbeya City, Musa Mapunda, alisema baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya tatu msimu huu, sasa wanaweka mikakati ya kuhakikisha timu hiyo inachukua ubingwa wa ligi Kuu ya Soka Tanzania bara msimu ujao.

Naye kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi, alisema katika usajili wao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi hiyo hawatachukua wachezaji wenye majina kutoka timu zinazoshiriki ligi hiyo bali bali ataangalia zaidi wachezaji chipukizi wasio na majina kutoka ndani ya mkoa wa Mbeya.

Mbeya City ilianzishwa Julai mwaka 2011 na huu ni msimu wake wa kwanza kushiriki ligi hiyo na kupata mafanikio yak upigiwa mfano.

Wednesday, April 23, 2014

Jackline Wolper: Wasanii wanaambukizana Ukimwi

Na Rhobi Chacha, Dar es Salaam
STAA wa filamu Bongo,  Jackline Wolper, ameibuka na kusema kuwa baadhi ya wasanii wanaambukizana ugonjwa hatari wa Ukimwi ‘Ngoma,’ wenyewe kwa wenyewe kutokana na kukacha matumizi ya kondomu.
Jackline Wolper, msanii wa Bongo Movie, Tanzania
Akizungumzia hilo, Wolper alisema baadhi ya mastaa wengi wa kibongo wapo wanaoambukizana ‘Ngoma,’ kwa sababu ya kuendekeza ngono zembe hali ambayo ni hatari kwa ustawi wa sanaa hiyo.

“Ni kweli wala siongopi baadhi ya wasanii hatujali matumizi ya kondomu, wito wangu watu wawe waaminifu na wakishindwa basi watumie kinga kwa usalama wa afya zao na ustawi wa tasnia ya filamu.

NYUMBA INAUZWA: IPO MBEZI KWA YUSUPH JIJINI DAR ES SALAAM

 Nyumba hii inauzwa. Ipo Mbezi kwa Yusuph, jijini Dar es Salaam. Ipo katika hali nzuri na imezunguukwa na miti kwa ajili ya kivuli cha kupumzikia. Ina eneo kubwa na tulivu. Bei ni maelewano. Mawasiliano ni 0713611878.....

 Sehemu ya nyumba hii inavyoonekana pichani.
 Nyumba hii jinsi ilivyo.
 Ni nzuri sana.
 Karibu uione kwa maelewano ya kuuziana.
 Nyumba hii inauzwa.
Karibu sana. Nyumba hii inauzwa na ni nzuri kwa ajili ya makazi. Ina eneo kubwa na zuri.

SIWEZI KUVUMILIA: Azam FC imewaumbua ‘Doto na Kulwa’

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NITAUMIA kama kuna mtu atashindwa kuipongeza timu ya Azam iliyofanikiwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu.

Ndio, maana timu hii imeweza kunyakua ubingwa mbele ya timu za Doto na mwenzake Kulwa zinazoaminika ni timu vigogo vya soka vya Tanzania Bara. Kwa wasiojua, timu za Doto na Kulwa, basi ni Simba na Yanga, zilizoanzishwa miaka ya 1935 kwa Yanga na 1936 kwa mwenzake Simba SC.

Wakati inanyakua ubingwa wa Tanzania Bara, wapo baadhi ya watu wanaoshikwa na machungu kiasi cha kufikiria kuwa Azam wameshinda kwa kubebwa, jambo ambalo si kweli hata kidogo.

Hapa siwezi kuvumilia kamwe. Siku moja baada ya kushinda mbele ya Mbeya City kwa bao 2-1 jijini Mbeya, Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi aliibuka akisema kuwa Azam wanabebwa.

Hapa unaweza kushangaa kauli hii. Tujiulize. Vipi Mbeya City wangefungwa na timu za kina Doto na Kulwa yani Simba na Yanga?
Vipi timu hizi zingeendelea kutawala soka la Tanzania kwa kuibuka mabingwa kila mwaka? Hapana. Hii si njia nzuri.

Kwa timu kama Azam FC, nathubutu kusema kuwa imestahili kunyakua ubingwa wa Tanzania Bara. Na inastahili pia kushiriki michuano mikubwa, ikiwamo Ligi ya Mabingwa Afrika, msimu ujao.

Wasimamizi wa soka la Tanzania, Shirikisho la Soka nchini (TFF) iwe makini katika hili. Azam ni miongoni mwa timu zenye wachezaji mahiri mno.
Hata hivyo haitoshi, pia imewekeza vizuri, hivyo sioni ajabu ikichukua ubingwa wa Tanzania Bara au hata taji lolote barani Afrika.

Huu ni wakati wa kujivunia matunda ya uwekezaji mzuri wa soka na kuachwa kubabaishwa na timu zinazojiita vigogo.

Tangu kuibuka kwa timu ya Mbeya City, nilipenda aina ya soka lake. Kuna uwezekano mkubwa soka letu likapanda chati kwa kuzalishwa wachezaji wazuri kutoka katika timu za kawaida huko mikoani, maana soka halipo Simba na Yanga tu.

Huu ndio ukweli hivyo ni wakati wetu kujivunia na kuwaunga mkono mabingwa wapya, timu ya Azam FC, huku nikishindwa kuvumilia kama yupo anayeumizwa na matokeo haya.

Ndio maana nasema, hizi timu za kina Doto na Kulwa zifikie wakati zithaminiwe kwa ukongwe wao ila si kwa soka lao. Hazina kitu kabisa hizi.
Zimechoka, zimeishiwa. Ni Baraka ya majina tu, ila uwanjani ni sifuri.
Tuonane wiki ijayo.
+255712053949

Tuesday, April 22, 2014

Kitambi noma bingwa bonanza la Pasaka Arusha

Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga akiwa anasalimiana na wachezaji wa timu   Mango Garden ya jijini Dar es salaam wakati walivyokuja kushiriki bonanza la kitambi noma lililofanyika katika kiwanja cha kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid ya jijini Arusha

Katika bonanza hili la kitambi noma kuliuzuriwa na watu wengi akiwemo mbunge wa jimbo Meatu  kupitia CHADEMA Aliyevaa tisheti ya blue Mh. Meshack Opulukwa
Kulikuwepo pia na mashindano ya kukimbia na magunia  ambapo katika mashindano haya mchezaji kutoka timu ya Mango Garden alishinda
Washabiki wa timu ya kitambi noma ya jijini Arusha wakishabikia ushindi mara baada ya kushinda kukimbiza kuku.

Mwenyekiti wa BungeMaalum la Katiba, Samuel Sitta atinga Ikulu Zanzibar kumpa rais Shein mwenendo wa Bunge la Katiba

 
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta kulia, akimpatia taarifa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Dk Ali Mohammed Shein juu ya mwenendo Bunge hilo na ulipofikia alipomtembelea Ikulu ya Migombani Zanzibar. Picha na Owen Mwandumbya 

Wakati viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiweka kambi Zanzibar, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta jana naye alitumia siku nzima visiwani humo akikutana na baadhi ya viongozi wa Serikali, katika kile kinachotafsiriwa kuwa kulinusuru Bunge hilo.

Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka Zanzibar zinasema Sitta alikutana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Rais Mstaafu, Aman Karume na mwanasiasa wa siku nyingi wa CCM, Mzee Hassan Nassor Moyo.

Pitia kwa urefu tamko la UVCCM dhidi ya UKAWA

Leo Nitatumia maneno makali kidogo ili tuelewane kiurahisi. Wapinzani wa Nchi hii ni "BAPHOON". Maana ya BAPHOON ni Watu au Kundi la Watu linalotumika Kwa Maslahi ya Mataifa Mengine Kuangamiza Taifa Lao. Wako Tayari Hata Kuchukua Mabomu na kulipua Nchi yao Wenyewe. Hawa ndio wanaojiita UKAWA (THE BAPHOON)
Imani namba Tano na namba nane za Chama Cha Mapinduzi kwa pamoja zinasema:
Cheo ni Dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu na Nitasema Kweli Daima Fitna kwangu Mwiko.
Paul C. Makonda, Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM ambaye pia ni Mjumbe Bunge Maalum la Katiba
Kwa tafsiri ya Imani ya Chama tunakubaliana na maneno ya Mwanahistoria wa zamani wa Uingereza Lord Acton aliyewahi kusema; “Power tends to Corrupt, and absolute power corrupts absolutely. Great men are almost always bad men” Yakimaanisha kuwa; “Madaraka yana tabia ya kuwaharibu walio nayo, na wenye madaraka makubwa Zaidi huharibika Zaidi kwa kuwa hata watu wema hugeuka kuwa wabaya wakishakuwa na madaraka”

Na sisi Vijana Wazalendo tunasema; “Watu wenye Madaraka Makubwa Wakiharibiwa na hayo madaraka hulewa hayo madaraka na kuanza hata kutukana kudharau waliowapa madaraka hayo. Lakini wenye madaraka makubwa wanaojua kuwa madaraka yao ni dhamana, kwanza huwa wapore na wanyenyekevu na hubeba dhamana kubwa ambayo wao huona madaraka hayo ni Mzigo wala si zawadi.”

Wapo wanaodhani kuwa Vyama vya Upinzani vipo kwa ajili ya Maslahi ya Taifa. Wapo wanaodhani Vyama vya Upinzani ndio mkombozi wao. Na wapo wanaodhani muarobaini wa matatizo ya taifa hili ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ni vyama vya Upinzani. Ukweli halisi wamepotoka sana. Vyama vya Upinzani vipo kwa maslahi yao tu na vimekuwa ni dhaifu kiasi haviwezi kuaminiwa kupewa dhamana ya Uongozi wa Taifa hili.

Uhakiki yachomoza mashindano ya nyama choma jijini Dar es Salaam



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAA ya Uwakiki iliyopo Kijichi, imeibuka kidedea  kwa kuwa baa inayochoma nyama bora katika shindano la Safar Lager Nyama Choma mkoa wa Dar es Salaam.
Iliibuka juzi katika fainali za shindano hilo zilizofanyika katika Viwanja vyaLeaders, Kinondoni Dar es Salaam na kujinyakulia kitita cha  sh.milioni moja, kombe na cheti.

Jumla ya baa sita kutoka wilaya zote Dar es Salaam, ziliingia fainali ambapo nafasi ya pili ilinyakuliwa na baa ya Meedakutoka Sinza, ambayo iliondoka na sh.800,000 , ikifuatiwa na Dar Safari Park iliyopata
600,00, Soccer City,400,000, Fyatanga 200,000 na Blue Fish, 100,00.

Pamoja na  zawadi za fedha, pia baa hizo zilipata vyetivya ushiriki, ambapo bendi  ya Twanga Pepeta na disko la DJ John Dilinga 'JD', viliongoza burudani katika fainali  hizo.

Awali akizungumza katika shamrashamra hizo, Meya wa Manispaa Kinondoni, Yusuf Mwenda alisema shindano hilo likitumika vizuri, linaleta afya bora na kuongeza ajira kwa vijana.

"Shindano hililinasaidia kuweka afya yamlaji nyama salama, nahivyo kuongezaidadu yawalaji,kupanuasoko la biashara ya nyamana hatimayemfugaji kufaidika na ajira kuongezeka,"alisema.

Meneja  wa Bia ya Safari, OScar Shelukindo alisema wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha maendeleo kwenye jamii kupitia udhamini wa michezo pamoja na uwezeshaji wa wafanyabiashara.

Kiingilio cha chini Taifa Stars na Burundi Sh 5000



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KIINGILIO cha chini katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu Rugamba) itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa mechi hiyo itakuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa wa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari ipo kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach kujiandaa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka nchini Kenya.

Burundi inatarajia kuwasili nchini keshokutwa (Aprili 22 mwaka huu) tayari kwa ajili ya mechi hiyo inayotajiwa kuwa ya kusisimua. Mechi hiyo imepangwa kuanza saa 10 jioni.

Wachezaji wa Taifa Stars waliopo kambini ni Deogratias Munishi, Mwadili Ali, Aidan Michael, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Hassan Mwasapili, Kelvin Yondani, Said Moradi, Amri Kiemba, Frank Domayo, Himid Mao, Jonas Mkude, Athanas Mdamu, Haruna Chanongo, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Ramadhan Singano na Simon Msuva.

Wengine ni Benedicto Mlekwa, Emma Simwanda, Joram Mgeveje, Omari Kindamba, Edward Mayunga, Shiraz Sozigwa, Yusuf Mlipili, Said Ally, Abubakar Mohamed, Hashim Magona, Omari Nyenje, Chunga Zito, Mohammed Saidi, Ayoub Lipati, Abdurahman Ally na Paul Bundara.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...