Thursday, April 17, 2014
Wednesday, April 16, 2014
Kairuki asimikwa ubosi wa CCM Kilimanjaro
| Katibu mkuu wa Umoja wa Vijana UVCCM Sixtus Mapunda, akimsimika Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki, kuwa Kamanda wa Vijana wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. |
| Katibu mkuu wa umoja wa Vijana UVCCM, Sixtus Mapunda akimsomea , Naibu waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki kiapo cha ukamanda. |
Naibu waziri wa Sheria na
Katiba Angellah Kairuki, akila kiapo cha kusimikwa kuwa kamanda wa
umoja wa vijana UVCCM wilaya
ya Same.
|
| Naibu waziri wa Sheria na Katiba Angellah Kairuki akizindua Shina la wakereketwa wa umoja wa Vijana Uvccm, baada ya kusimikwa kuwa kamanda wa umoja huo wilayani Same. |
Tuesday, April 15, 2014
SIWEZI KUVUMILIA: Siwezi kuwapongeza watoto wa mitaani kamwe
NA KAMBI
MBWANA, DAR ES SALAAM
NASIKIA
eti wale watoto wa mitaani waliokusanywa na kuelekea nchini Brazil wamepongezwa
na serikali baada ya kunyakua Kombe la Dunia kwa watoto wanaoishi katika
mazingira magumu.
Baadhi ya wachezaji wa mitaani waliopata taji nchini Brazil.
Kama hivyo
ndivyo, basi sisi tuna moyo wa ujasiri sana. Kwa maana tumekubali kuwa suala la
watoto wa mitaani Tanzania limemea kiasi cha kukosa mbinu mbadala ya
kupambana nalo.
Hii ni
kazi kubwa. Tanzania nchi yenye wingi wa vipaji, tunahitaji kuwa na sera nzuri
kwa ajili ya kuendeleza michezo, kama kweli tunataka kupiga hatua.
Huo ndio
ukweli. Vinginevyo siwezi kuvumilia, kwasababu naona porojo, siasa, huku tukiwa
wepesi kutafuta maeneo ya kupigia picha.
Kwanini
nasema hivyo? Hata hawa watoto wa mitaani wanaopongezwa leo kwa kuchukua taji
hilo, baada ya mwezi mmoja pengine wakawa wamerudi mtaani kuendelea na maisha
yao magumu.
Mwakani
watachukuliwa wengine, ukizingatia kuwa ni wengi kuliko wale wanaoishi maisha
mazuri. Tukiendelea na mtindo huu, Watanzania hatutakuwa na
mafanikio
katika michezo zaidi ya kusubiria kuokoteza watoto na kuwasafirisha nchi za
wenzetu na kuwatelekeza wakirudi.
DRFA wawapongeza Azam kwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
kimeipongeza timu ya Azam FC kwa kufanikiwa kwa mara ya kwanza kutwaa ubingwa
wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2013/2014.
Nyota wa Azam waliofanikisha ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu.
Azam FC ilijihakikishia kutwaa ubingwa huo Jumapili baada ya
kuifunga timu ya Mbeya City mabao 2-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa
kwenye Uwanja wa Sokoine.
Ofisa Habari wa DRFA Mohamed Mharizo alisema jijini Dar es
Salaam leo mchana kuwa ubingwa huo wa Azam ni kielelzo cha kujituma kwao na kuwa na
ushirikiano na walistahili kutwaa taji hilo.
“Kwa niaba ya DRFA nachukua fursa hii kuwapongeza wachezaji,
benchi la ufundi na viongozi wa timu ya Azam FC kwa ujumla, kwa kufanikiwa
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Ni imani yetu DRFA kuwa timu hiyo itawakilisha vyema nchi
katika michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika, tunawatakia kila la kheri katika
michuano hiyo.
“Lakini pia tunaipongeza Yanga kwa kushika nafasi ya pili
katika ligi hiyo, nao tunawatakia kila la kheri katika michuano ya Kombe la
Shirikisho. Sisi Mkoa tunafarijika sana kuona timu zetu za Mkoa wa Dar es
Salaam zinavyofanya vizuri,” alisema.
Wagosi wa Kaya kuja na 'Bao na Gahawa'
Na Asifiwe George, Dar es Salaam
BAADA
ya kimya cha muda mrefu wasanii wanaounda kundi la muziki wa kizazi kipya la
Wagosi wa Kaya, limetoa vitu vipya vinavyokwenda kwa jina la 'Bao' na Gahawa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, mmoja wa wanaounda kundi hilo
Fred Maliki 'Mkoloni' alisema kutokana na deni kubwa walilonalo kwa mashabiki
wao wameamua kurudi upya katika tasnia hiyo.
"Kuthibitisha kuwa ujio wetu sio wa kubahatisha tumejiandaa vizuri
kukabiliana na soko gumu la muziki hata upande wa albamu ambao unakimbiwa na
wasanii wengi kwa sasa," alisema.
Alisema nyimbo zote mbili zimerekodiwa katika studio ya Tongwe Records na video
zake zimeshootiwa Tanga na kampuni ya Ngome video chini ya muongozaji Mecky
Kaloka.
"Ujio wa kazi hizo mbili ni wa moja kwa moja na video bila ya
kuwachelewesha wasanii kupata ladha tuliyoamua kuirudisha katika tasnia baada
ya kimya cha muda mrefu," alisema.
Sunday, April 06, 2014
Yanga yaikandamiza JKT Ruvu bao 5-1 Uwanja wa Taifa
Timu ya Yanga SC leo imezinduka tena kwa kuwachabanga kwa
jumla ya mabao 5-1 timu ya JKT Ruvu, mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa,
jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Yanga wakionekana kuwa wachache zaidi katika mchezo wa leo dhidi ya JKT Ruvu ambapo walishinda bao 5-1.
Katika mchezo huo, winga wa Yanga, Mrisho Ngassa alifunga
bao tatu kwa dakika ya 8, 15 na 48, wakati goli la nne la Yanga lilifungwa na
Didier Kavumbagu dakika ya 40, huku lile la tano likifungwa dakika ya 51 na Hussein
Javu, wakati bao la kufutia machozi la JKT likifungwa na Idd Mbaga dakika ya
83.
Mechi ilianza kwa kasi, ila JKT walipunguza umakini na kuwapa
nafasi Yanga kulishambulia lango lao mara nyingi na kufanikiwa kuibuka na
ushindi mnono ambao pia umeibua matumaini ya kutetea ubingwa wao.
Super D apongeza pambano la ngumi Chalinze
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA wa mchezo wa masumbwi wa klabu
ya Ashanti Boxing, yenye maskani yake Ilala, jijini Dar es Salaam, Rajabu
Mhamila ‘Super D’, amesema kwamba kufanyika kwa pambano la Erick Magana na
Mwaite Juma wilayani Chalinze ni sehemu ya kuendeleza mchezo huo na kuupatia
mafanikio.
Pambano hilo limepangwa kufanyika Aprili
15 katika Ukumbi wa Ndelema Inn, mjini Chalinze, ambalo halitakuwa la ubingwa,
huku ikiwa ni njia za kuweka harakati ya kuutangaza vizuri na kuurudisha kwenye
hadhi yake ya siku zote.
Akizungumza jijini Dar
es Salaam juzi, Super D alisema kwamba wadau wa ngumi wamekuwa wakishirikiana
kwa mambo mengi, ikiwamo mbinu nzuri za kuuletea mafanikio makubwa mchezo wa
masumbwi.
Alisema mapambano kadhaa
ya utangulizi yatakuwapo likiwapo la Biglee Juma, Godfrey Sadick, Hussein
Pendeza nao wakitarajiwa kupanda ulingoni kwenye patashika hiyo itakayokuwa na
faida kubwa kwa wakazi wa Chalinze na Tanzania kwa ujumla.
“Tuna mipango kabambe ya
kutangaza mchezo wa masumbwi katika nchi yetu, hivyo tunaamini kwa pamoja
Chalinze watapata burudani kamili kutoka kwa vijana wao,” alisema.
Pambano limeandaliwa kwa
ajili ya kuhamasisha mchezo huo nchini, ambapo kwa siku hivi karibuni
unaonekana kusua sua, hivyo hizi ni juhudi za kuuweka juu,” alisema.
Mchezo wa masumbwi
umeendelea kuwekewa mikakati ya kuuweka kileleni baada ya kuonekana kuwa
umeanza kusua sua katika kona ya ngumi nchini.
Somo la ufugaji wa kuku
MCHANGANUO WA KUANZA KUFUGA KUKU, KWA WALE WENYE MTAJI MDOGO NA WA KATI KUANZIA LAKI MBILI ( 200,000/=)..
Kwa hisani ya Mtaalam wa fedha wa Tanuri Media, Chuwa Freddie
Kwa mtaji mdogo kama laki na 60 mtu anaweza kuanza kwa kufuga kuku wa kienyeji na hawa lazima uwe na eneo ambalo utajenga banda kubwa liwe na banda la ndani na eneo la wavu na vieneo vya kutagia anaweza kununua vifaranga vya mayai 15 ambavyo ni elf 45 na majogoo 5 ambayo ni elf 12 na 500.
hapo imebaki laki 1na elf 5 hizi bati laini zinauzwa 11,000/- mpaka 12000/- kwa bati 3 zinatosha ambapo ni 33,000/- hapo imebaki
72,000/- mabanzi 8 ni kama elf 40 hapa atanunua ya bei nafuu hapo imebaki elf 32,000/- hiyo inatosha misumari na waya/wavu hapo kale ka 160,00/- inakua imeisha inabaki gharama za fundi na chakula cha kuanzia
fundi ni kama 30,000/-
chakula cha kuanzia kwa kuku 20 wa kienyeji ni debe la pumba ambalo ni kama 10,000/-
vifaa kama vya kuwekea maji unaweza.hata kukata makopo ya maji ya kilimanjaro ukaweja maana hawa kuku ni wakubwa hawawez kuzama ili kuepusha gharama.
Sasa hiyo loss ya kama elf 40 tukadirie 50 itatoka wapi? hapa ndipo pakufata ndugu jamaa na marafiki sasa ukimpelekea mtu mchanganuo wako na ukamweleza nia yako na upungufu wako yupo atakaekuchangia elf 5 wengine 10 hatimae zinatimia.
hayo ndo mawazo yangu mimi ni mjasiriamali jamani anaehitaji ushauri nipo nimejaa tele kila la kheri vijana....
Kwa hisani ya Mtaalam wa fedha wa Tanuri Media, Chuwa Freddie
Kwa mtaji mdogo kama laki na 60 mtu anaweza kuanza kwa kufuga kuku wa kienyeji na hawa lazima uwe na eneo ambalo utajenga banda kubwa liwe na banda la ndani na eneo la wavu na vieneo vya kutagia anaweza kununua vifaranga vya mayai 15 ambavyo ni elf 45 na majogoo 5 ambayo ni elf 12 na 500.
Mfugaji wa kuku akionekana pichani.
Kwani.vifaranga hivi.no.vikubwa na vinakua.tayar.vimefukuzwa na.mama yao so kufa ni ngumu...jumla hapo ni kama 57,500/-hapo imebaki laki 1na elf 5 hizi bati laini zinauzwa 11,000/- mpaka 12000/- kwa bati 3 zinatosha ambapo ni 33,000/- hapo imebaki
72,000/- mabanzi 8 ni kama elf 40 hapa atanunua ya bei nafuu hapo imebaki elf 32,000/- hiyo inatosha misumari na waya/wavu hapo kale ka 160,00/- inakua imeisha inabaki gharama za fundi na chakula cha kuanzia
fundi ni kama 30,000/-
chakula cha kuanzia kwa kuku 20 wa kienyeji ni debe la pumba ambalo ni kama 10,000/-
vifaa kama vya kuwekea maji unaweza.hata kukata makopo ya maji ya kilimanjaro ukaweja maana hawa kuku ni wakubwa hawawez kuzama ili kuepusha gharama.
Sasa hiyo loss ya kama elf 40 tukadirie 50 itatoka wapi? hapa ndipo pakufata ndugu jamaa na marafiki sasa ukimpelekea mtu mchanganuo wako na ukamweleza nia yako na upungufu wako yupo atakaekuchangia elf 5 wengine 10 hatimae zinatimia.
hayo ndo mawazo yangu mimi ni mjasiriamali jamani anaehitaji ushauri nipo nimejaa tele kila la kheri vijana....
Subscribe to:
Posts (Atom)






