https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, January 06, 2014

SIWEZI KUVUMILIA: Nimeuchoka mgogoro wa Simba usiokwisha

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI mihemko gani isiyokuwa na likizo? Nani yupo nyuma ya wanachama hawa wa Simba? Nini hasa kiini cha mzozo huu? Haya ni baadhi ya maswali ninayojiuliza mara kwa mara.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage.
Ni pale ninapoangalia mgogoro unaoendelea kuwapo miaka nenda rudi kwa klabu ya Simba. Ndio, kuna uwezekano mkubwa mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage hayupo sahihi.
Na inawezekana pia anavunja Katiba hasa kwa kuangalia kuwa Makamu Mwenyekiti wake Godfrey Kaburu alijiuzulu na nafasi yake haijajazwa hadi wakati huu.
Katiba ya Simba inasema Makamu Mwenyekiti anapojiuzulu nafasi yake inatakiwa izibwe ndani ya siku 90. Tangu Kaburu ang’oke, ni zaidi ya siku 200 zimepita.
Haya ni mapungufu makubwa sanjari na ubabe aliokuwa nao Rage katika madaraka yake ndani ya Simba. Pamoja na hayo, Simba inatakiwa kufanya uchaguzi Mkuu Mei mwaka huu.
Hivyo inaonyesha kuwa Rage ana nafasi ndogo ya kuwapo katika nafasi hiyo, hasa kama kweli wanachama hao wamemchoka mwenyekiti wao huyo.
Kama hivyo ndivyo, sioni kwanini wanachama hao wasijipange ili wasubiri Uchaguzi Mkuu wao. Hii siwezi kuvumilia. Siwezi Kuvumilia kwasababu chokochoko hizi hazina tija.
Hata kama Rage akiamua kutangaza kujiuzul leo, nani anaweza kushika nafasi yake kwa nyakati hizi za kuelekea uchaguzi? Binafsi naona huu ni mgogoro wa maslahi.
Kuna mtu au watu wapo nyuma ya wanachama hawa ambao kila mwaka wamekuwa wakijiweka mbele. Baadhi yao ndio walioshiriki kumsumbua Hassan Dalali wakati yupo madarakani.
Muda wake ukaisha na wanachama hawa hawa wakamchagua Rage awe mwenyekiti wao. Ndani ya mwaka mmoja, wakageuka na kumuona Rage si chochote.
Mgogoro huu ulikuwapo tangu mwaka 2011. Kila siku ni maneno na mvutano usiokuwa na maana yoyote. Ndio, naweza kuwa miongoni mwa wadau wa soka wanaotaka Rage ang’oke au akubali kuongoza kwa kufuata katiba yake, ila kwakuwa wakati wake umeshakwisha, sidhani kama kuna haja ya kupambana naye.
Waswahili wamesema kuku wako, manati ya nini? Hata afanye vipi, bado atatakiwa aitishe Mkutano Mkuu wa Simba utakaombatana na Uchaguzi Mkuu ndani ya mwaka huu.
Nafikiri Watanzania wote hususan mashabiki na wanachama wa Simba wangetulia ili mipango ya kiutendaji ifanywe kama ipo na baadaye watakutana katika uchaguzi wao.
Hapo watafanya uamuzi wowote watakaopenda. Kinyume cha hapo tutaendelea kubabaisha kwa kuingiza chokochoko zisizokuwa na maana na kuharibu soka letu.
Hakika siwezi kuvumilia, hivyo kuna haja sasa ya wanachama wote wa Simba kumuacha Rage na badala yake wajiandaye katika Uchaguzi wao utakaotishwa kwa mujibu wa Katiba yao.
Tuonane wiki ijayo.
+255712053949

Sunday, January 05, 2014

Boban aripoti Coastal Union Tanga


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Coastal Union yenye maskani jijini Tanga, Haruna Moshi ‘Boban’, ameripoti mkoani Tanga kwa ajili ya kuanza mazoezi ya kujiandaa na mzunguuko wa pili wa ligi ya Tanzania Bara.

Haruna Moshi Boban pichani.
Kuripoti kwa Boban kunashusha presha kutoka kwa wadau wa timu hiyo wanaosema kuwa kiungo huyo amekuwa mtovu wa nidhamu kwa kuchelewa kuripoti kambini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa timu ya Coastal Union, Hafidh Kido, alisema kuwa Boban aliafiki kujiunga na wenzake mapema wiki hii ili kuendelea na mazoezi ya pamoja.

Alisema kuwa kujiunga na wenzake katika maandalizi ya michuano ya Vodacom ni sehemu ya kujiweka sawa zaidi.

“Baada ya kumaliza ratiba yake kama alivyotoa taarifa kwa viongozi wake, Boban amejiunga na wenzake.

“Tunaamini mambo yatakuwa mazuri kwa kiungo huyo ambaye uwezo wake hapana shaka unajulikana na kuheshimika sana,” alisema.

Boban ni miongoni mwa wachezaji wanaoheshimika katika soka hapa nchini, huku uwezo wake ukiweza kufanya makubwa awapo uwanjani.

Jahazi kukamua Morogoro Januari 31



KUNDI bingwa la miondoko ya mwambao, Jahazi Modern Taarab litaanza kutambulisha nyimbo zake mpya mwishoni mwa mwezi huu ambapo mji wa Morogoro utakuwa wa kwanza kupata uhondo huo.
Wakali wa Jahazi Modern Taarab, pichani.
Jahazi watafanya onyesho maalum mjini humo Ijumaa ya Januari 31 ndani ya ukumbi wa Tanzanite Complex.
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Jahazi kupiga ndani ya ukumbi huo uliofunguliwa kiasi cha mwaka mmoja uliopita.
Kwa mujibu wa mratibu wa onyesho hilo Warda Makongwa wa Planet FM ya mjini humo, wameamua kuandaa onyesho hilo kufuatia maombi ya mashabiki wengi waliotaka Jahazi nayo ibishe hodi ndani ya Tanzanite Complex.
Warda amesema Jahazi halitaenda hivi hivi bali litaandamana na nyimbo mpya kabisa ambazo hazijawahi kusikika hapo kabla.
Amefafanua kuwa nyimbo hizo ni sehemu ya maandalizi ya albam mpya ijayo ya Jahazi Modern Taarab inayoongozwa na Mfalme Mzee Yussuf.


Saturday, January 04, 2014

Waendesha bodaboda wilayani Kilindi waomba kupewa leseni

Na Mwandishi Wetu, Kilindi
WAENDESHA Boda Boda wilayani Kilindi mkoani Tanga wameiomba Mamlaka ya Mapato mkoani Tanga (TRA), kuwapeleka wilayani humo huduma ya upatikanaji wa leseni kutokana na vijana wengine kutokuwa nazo hali inayochangiwa na kutokwepo kwa ofisi inayoshughulika na masuala hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, DC Selemani Liwowa, pichani.
Kilio hicho kilitolewa hivi karibuni na wananchi wa kata ya Kwediboma wilayani hapa wakati wakizungumza ambapo walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiikosa kitendo ambacho kinawalazimu kusafiri mpaka Tanga mjini ili kufuata huduma hiyo.
Evarist Mosha mkazi wa kata hiyo na dereva wa bodaboda alisema kukosekana kwa huduma hiyo wilayani humo serikali inakosa mapato kutokana na waendesha boda boda  wengi kutokuwa na leseni.
Akizungumzia suala hilo, Mkuu wa wilaya ya Kilindi, Suleiman Liwowa alisema ni kweli katika wilaya hiyo hakuna ofisi za mamlaka ya mapato (TRA) na kutaka uwekwe utaratibu ambao utawafikia wananchi na endapo watakubaliana nao wataweka mazingira mazuri ya upatikaji ofisi.

Cheka ashangazwa na sera ya michezo Tanzania



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Francis Cheka, amesema kwamba hakuna bondia anayeweza kupiga hatua kama wadau wa masumbwi wataendelea kuweka akili zao katika mchezo wa mpira wa miguu.
Francis Cheka, pichani.
Hayo yamekuwa malalamiko ya Cheka ya mara kwa mara, jambo linaloonyesha kuwa suala hilo limeshika hatamu katika juhudi zinazoangusha mchezo wa masumbwi.

Akizungumza jana kwa njia ya simu akitokea mkoani Morogoro, Cheka alisema kuwa serikali kwa kupitia wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo imeweka akili zao kwenye soka.

“Unaponiambia mimi najiandaa vipi na ngumi za kimataifa inaniuma kwasababu hakuna anayeweza kusonga mbele kama mfumo wetu utakuwa umeoza kwa kiasi kikubwa.

“Naomba wadau wa masumbwi wote wahakikishe kuwa maendeleo ya michezo ukiwamo wa ngumi unapiga hatua,” alisema Cheka.

Cheka ni miongoni mwa mabondia wanaofanya vizuri katika mchezo wa masumbwi hapa nchini, huku akifanikiwa kuibuka na ushindi kwa mapambano mengi nchini.

APL Mwera yaibuka kidedea Mwidau CUP


Na Mwandishi Wetu, Pangani

TIMU ya Soka la APL kutoka Kata ya Mwera, imetoka kifua mbele huku wakitangazwa mabingwa wapya wa kombe la Mwidau CUP.

Timu hiyo iliibuka na ushindi dhidi ya timu ya Torino ya mjini Pangani, ambayo ilishindwa kufua dafu kwa kufungwa kupitia penati.
Mbunge Amina Mwidau, akimkabidhi kikombe cha ushindi Nahodha wa timu ya APL Mwera Shabani Athuman, baada ya timu hiyo kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi ya Mwidau CUP, mjini Pangani jana.

Hadi dakika tisini za mchezo huo wa fainali hiyo ya Mwidau CUP zinamalizika timu zote zilishindwa kutambiana na kulazimika kutoka suluhu ya bao 1-1.

Kutokana na hali hiyo timu hizo ilizilazimu kuingia katika hatua ya matuta ambap kati ya penati nne zilipingwa kwa kila timu, Torino ilipoteza penati mbili huku APL Mwera ilipoteza moja hali hiyowafanya kuibuka na ushindi na kutawazwa mabigwa wa ligi hiyo.


Timu hizo hadi zinakwenda mapumziko katika kipindi cha kwanza kila timu ilitoka huku ikishindwa kuona nyau ya mwenzake lakini ilipofika dakika ya 57, mchezaji Christopher Gunda wa APL alifanikiwa kuziona nyavu za Torino.


Hata hivyo katika dakika ya 62 Torini ilijibu mapigo na kusawazina bao hilo ambapo hadi dakika 90 timu zote zilishindwa kutambiana na kuamua kupigwa matuta.


Awali akihutubia kabla ya kuanza kwa mchezo huo mgeni rasmi katika mashinda hayo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), aliwataka vijana kuthamini michezo kwani ajira ambayo imekuwa na manufaa kwa Taifa.


“Kwa imani yangu ninaamini hata hapa Pangani tunao wachezaji wazuri kupitia timu zetu hizi zilizoshiriki ligi hii ya Mwidau CUP ambao wana uwezo wa kufanya vizuri katika timu kubwa za ndani na nje ya nchi yetu,” alisema Mwidau.

Friday, January 03, 2014

Ajali yatokea Manzese leo na kutoa roho za watu watatu



HABARI zilizotufikia ambazo bado hazijathibitishwa na jeshi la Polisi zinasema kwamba katika Barabara ya Morogoro, maeneo ya Manzese Argentina, ajali imetokea mapema leo saa sita mchana, ikihusisha gari la mizigo lori na bajaj.

Katika ajali hiyo, watu watatu walikufa papo hapo. Taarifa zaidi za ajali hiyo tunendelea kuzisaka na kuzitoa kadri tutakavyozipata kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari.
 

Kijiji cha Msomela wilayani Handeni mkoani Tanga chapewa cheti cha ardhi yao

Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msomela jana baada ya kukabidhi cheti cha ardhi pamoja na ramani ya kijiji hicho, ikiwa ni hatua ya kuwapa umiliki halali wa eneo hilo. Picha na Rajabu Athumani, Handeni


RSK Kibajaji akamilisha wimbo Mapenzi ya Pesa


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MSANII mwenye maskani yake Handeni, mkoani Tanga, Ramadhan Said Killo, ama RSK, amekamilisha kutengeneza wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Mapenzi Pesa’.
Msanii RSK mwenye maskani yake wilayani Handeni mkoani Tanga.
Msanii huyo anayesaka ufalme wa muziki wa kizazi kipya, akitokea Tanga kwa Wagosi wa Kaya, ni kati ya vijana wanaopigania nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.

Akizungumza jana kwa njia ya simu, msanii huyo alisema kuwa wimbo huo umetengenezwa katika Studio ya EnoBeats chini ya mtayarishaji wake Black Man.

RSK Kibajaj alisema kuwa anaamini wimbo huo utakuwa chachu ya kudhihirisha makali yake katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini.

“Nipo katika harakati za kuonyesha makali yangu katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, hivyo naamini wimbo wangu wa Mapenzi ya Pesa utakuwa njia nzuri.

“Naomba Watanzania wanipe ushirikiano juu ya wimbo wangu na kazi zangu zote ili nifanikiwe katika anga ya muziki huo, ukizingatia kuwa sanaa ndio kazi ninayoipenda,” alisema RSK Mkufu Kibajaj, mwenye maskani yake wilayani Handeni.

Nyimbo alizowahi kuachia msanii huyo ni pamoja na Kibajaji na Usiniache, ambazo bado hazijafanikiwa kutangaza makali yake nje ya wilaya hiyo, likiwamo jiji la Dar es Salaam.

Thursday, January 02, 2014

Minziro: Sitishwi kuachwa kwangu Yanga

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
ALIYEKUWA kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Fredy Minziro, amesema kwamba hatishwi na uamuzi wa kuachwa kwake katika benchi la ufundi la timu hiyo, kwasababu anaamini ujuzi wake atapata sehemu kwa kuupeleka.
Fredy Felix Minziro, aliyekuwa kocha msaidizi wa Yanga
Maneno ya Minziro yamekuja baada ya Yanga kutimua benchi lote la ufundi, ikiwa ni mwendelezo baada ya kumuacha Kocha wao Mkuu, Ernest Brandit.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Minziro, alisema kuwa amekuwa akivunja ujuzi mwingi kutoka kwa makocha mbalimbali waliopita Yanga katika kipindi cha miaka minne, huku akiwa kama kocha msaidizi.
Alisema jambo hilo linampa matumaini makubwa kuwa uwezo wake umekuwa mkubwa na hawezi kukosa timu ya kuifundisha atakapoona inafaa, hivyo hana shaka na uamuzi wa mabosi wake.

Clouds Media Group waadhimisha miaka 14 kwa kuwajulia hali wagonjwa na kuwapa msaada Hospitali ya Temeke




 Mtangazaji wa kipindi cha Clouds FM, Dr Isaac Maro akikabidhi msaada wa vifaa kwa Dr Muzdalifat Abeid, bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali ya Temeke, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
 Mtangazaji wa kipindi cha Clouds FM, Dr Isaac Maro akikabidhi msaada wa vifaa kwa Dr Muzdalifat Abeid, bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali ya Temeke, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.

KITUO cha Redio namba moja hapa nchini, Clouds FM kimefikia kilele cha mwezi wa maadhimisho ya miaka 14 toka kimeanzishwa. Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kwa mwezi mzima sasa, yalianza na watangazaji  wa vipindi tofauti kwenda mikoa mbalimbali ili kuweza kusherekea miaka  hii 14 pamoja na wasikilizaji wao sehemu walipo.

Ikiwa ndio siku ya kilele cha maadhimisho hayo, Clouds FM imetembelea
hospitali ya Temeke na kituo cha kuhudumia vijana wanaotumia madawa ya  kulevya cha Keko Youth, ambapo misaada mbalimbali imetolewa. 
Wakiwa katika hospital ya Temeke, Clouds FM imetoa vifaa mbalimbali vya  hospitali katika wodi ya wanawake na watoto, huku Keko Youth wakipewa  vitendea kazi ambavyo vitawezesha vijana kujiajiri baada ya kumaliza  matibabu.

Akizungumzia maadhimisho hayo ya Clouds FM, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media  Group, Joseph Kusaga alisema sherehe hizi kwa mwaka huu ni za kipekee  kwa Clouds FM hasa kwa kuwa wameweza kufanikisha  mambo mengi makubwa  toka walipoanza. ‘Maadhimisho  haya ya miaka 14 kwa mwaka huu yana lengo moja kubwa, kuwashukuru  wasikilizaji wetu kwa kutufikisha hapa tulipo, na ndio maana tumeanza  kwa kuwapa misaada wanaohitaji, halafu tunamalizia kwa burudani’’  alisema Kusaga.

Wednesday, January 01, 2014

Taswa yawatandika Twanga Pepeta bao 1-0

 Beki wa timu ya Taswa Fc Sufianimafoto (kulia) akiwania mpira na mshambuliaji wa Twanga Fc, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Bonanza la kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014, lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, leo jioni. Katika mchezo huo Taswa ilianza mwaka mpya kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Juma Pinto katika kipindi cha pili.
 Mshambuliaji wa Taswa Fc, Juma Pinto (katikati) akiwatoka mabeki wa Twanga Pepeta Fc, wakati wa mchezo huo.
 Beki wa Taswa Fc, Athuman (kulia) akiwatoka wachezaji wa Twanga Pepeta.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...