https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, October 04, 2013

Makamu wa Rais Dkt Bilal aagana na mabalozi waliomaliza muda wao Tanzania na kukutana pia na Balozi wa Tanzania nchini Addis Ababa



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Marekani nchini Tanzania, aliyemaliza muda wake, Alfonso Lenhardt, aliyefika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Okt 3, 2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, aliyemaliza muda wake, Alfonso Lenhardt, aliyefika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Okt 3, 2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Tanzania, nchini Addis Ababa, Ethiopia, Naimi Aziz, aliyefika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Okt 3, 2013 kwa ajili ya mazungumzo. 

Thursday, October 03, 2013

Wadau, kampuni zaombwa kuwezesha tamasha la Utamaduni Handeni

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADAU wa mambo ya utamaduni na michezo wameombwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha kufanyika kwa Tamasha la Utamaduni lililopangwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Mratibu wa Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, Kambi Mbwana, pichani.

Hayo yamesemwa na mratibu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, alipozungumza na mwandishi wa mtandao huu mapema leo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya kutangaza mipango ya kuandaa tamasha hilo la aina yake na lenye mguso wa kuwakutanisha wadau wote kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo, Mbwana alisema endapo wadau wote, wakiwamo wafanyabiashara na wamiliki wa kampuni, taasisi za serikali watashirikiana katika hilo, mambo yatakuwa mazuri.

Alisema hali hiyo inamfanya aone haja ya kuwataka watu hao washirikiane kwa pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tamasha la utamaduni na michezo Handeni linafanyika kwa mafanikio na kuweka historia mpya.

“Watu wote wana umuhimu katika kufanikisha kwa tamasha hili, hivyo kila mmoja kwa nafasi yake tunaomba msaada wake hata wa kimawazo, ukizingatia kuwa kinachofanyika kwa sasa ni kuachiana majukumu tu.

“Tunawaomba wote wenye moyo wa kufanikisha wazo hili tushirikiane nao kwa namna moja ama nyingine, hasa kwa kuona wenye kampuni zao, mashirika na taasisi za serikali pia kutudhamini katika hili,” alisema Mbwana.

Kwa mujibu wa Mbwana, kufanyika kwa tamasha hilo kutakuwa ni sehemu nzuri ya kuwakutanisha wadau, wananchi wa Handeni na Tanzania kwa ujumla kwa ajili ya kujadiliana changamoto zinazowakabili kwa maendeleo yao.

Tamasha hilo la Utamaduni linaandaliwa chini ya Raha Company and Entertainment huku likifanyika kwa mara ya kwanza katika wilaya hiyo inayoongozwa na Mkuu wake wa Wilaya Muhingo Rweyemamu, wakati mbunge ni Dk Abdallah Omari Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara.

Wednesday, October 02, 2013

Lori laigonga treni ya Makyembe inayofanya safari zake za Ubungo na Stesheni



Watu wakiangalia ajali ya lori lililogonga treni inayofanya safari zake Ubungo na Stesheni leo saa 12 za jioni jijini Dar es Salaam na kuzua taharuki ya aina yake. Baaada ya kugonga, lori hilo lilipinduka. Picha na Mpiga Picha wetu.

Ngumi kutifuana katika pambano lingine la masumbwi Oktoba 26 mwaka huu, Ukumbi wa Panandi Panandi

Kocha wa Masumbwi nchini, Super D akitoa neno katika biashara yake ya kuuza cd za masumbwi.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MPAMBANO mwingine wa masumbwi unatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Panandi Panandi Oktoba 26 chini ya uratibu wa Kinyogoli Fondition, huku ukiwakutanisha mabondia mbalimbali.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini kutoka kambi ya ilala Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mpambano huo utawakutanisha bondia Yakubu Maganga atakae zichapa na Ubwa Salumu katika uzito wa kilo 75 huku Seif Ali akipambana na Hassani Labanda pamoja na mipambano mengine ya masumbwi itakayo wakutanisha mabondia mbalimbali

Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi, kuukwaa ubosi wa RECSA

Advera-Senso
                                                                                                                   
JESHI la Polisi kwa kupitia Msemaji wao Advera Senso pichani, limesema kuwa Tanzania inatarajia kupokea Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri kwa Nchi za maziwa makuu na pembe ya Afrika katika mapambano ya kuzuia na kudhibiti uzagaaji wa silaha haramu (RECSA) kutoka nchi ya Rwanda.
 
Makabidhiano hayo yatafanyika kesho tarehe 03/10/2013 katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ya Rwanda atamkabidhi uenyekiti huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania Mh.Dk Emmanuel Nchimbi.
 
Uenyekiti huo utadumu kwa muda wa miaka miwili ambapo katika kipindi hicho mikutano yote ya kukabiliana na uzagaaji wa silaha haramu itaratibiwa na Nchi ya Tanzania kupitia Jeshi la Polisi.

Umoja huo ulianzishwa mwaka 2005 kwa madhumuni ya kudhibiti uzagaaji wa silaha haramu kwa nchi za maziwa makuu na pembe ya Afrika ambazo ni pamoja na Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania.

   

Mbunge wa Kilwa Kaskazini akerwa na magari kufungwa minyororo jijini Dar es Salaam



Kadhia hii hapana
Moja kati ya sifa ya mwanadamu mwenye busara ni kukubali kujifunza kwa makosa aliyotenda na kuomba radhi aliowakosea.Mwalim Julius Nyerere aliwahi kuandika kwenye kitabu chake, Tujisahihishe, kuwa ni: ‘upumbavu mtu kuamini kuwa anajua kila kitu’’.
Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu.
Naandika kwa kuona kuwa hali mbaya inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam bila hatua stahiki kuchukuliwa. Pia kuwaomba wenzangu wanaokerwa, kuathirika na kuichukia tabia ya ufungaji magari ambayo yanapaki mitaani haswa katikati ya Jiji la Dar es salaam. 

Makundi ya mgambo na kampuni binafsi za ulinzi wamekuwa wanafunga magari kwa minyororo na kudai malipo kutoka kwa wamiliki wa magari husika kwa kusingizia kuwa umepaki ‘mahala pasiporuhusiwa’. Ajabu ni kwamba hakuna alama za katazo.
 
Jambo la kustaajabisha ni kuwa ramani ya mji wa Dar es salaam haijabadilika tangu kuchorwa na kubuniwa kwake na wajerumani miaka ya 1800+ na 1900 mwanzoni. 

Kumbukumbu ya kifo cha mama Betseba Lupembe Balandya

Mama B Photo - 17x22.jpg
IN THE LOVING MEMORY OF OUR BELOVED MOTHER
THE LATE MAMA BETSEBA LUPEMBE BALANDYA
(05 OCTOBER 2012 – 05 OCTOBER 2013)
The 1st Death Anniversary

Dear Mama Betseba Lupembe Balandya

It has been one year now,
Since God called you away.
Oh how the Angels rejoiced as you walked
Through those Pearly Gates that day

We can never say goodbye to you,
Because we could never bear the pain.
Instead we say we love you
Until we meet again in Heaven.
Days ran, months flew, one year passed ,
Praying, you left us saying good bye
A lovely wife and a mom you have been
Many troubles you have seen

To teach each of us you have done your best
God grant you an eternal rest

Offering to your soul today an Anniversary Mass
Always we remember you in our hearts
Send us praying a rain of Grace
Your example in our life a relief of peace

A Tribute of Love

Your beloved Husband Dr. Cornelius Lugata Balandya
Children: Patrick, William, George, Emmanuel, Belinda, Edward
Grandchildren: Dorice, Kenneth, Angela, Consolata, Kesheni, Betty, Anitha, Violet, Benny, Yolanda, Christian and Malcom
We would also take this opportunity to thank and extend our gratitude to each and every one of you for your support at what was very difficult time for us as a family.
May our good Lord extend his love and care to all of you.

Mpira Pesa kukutana Oktoba 6 mwaka huu


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WANACHAMA wa klabu ya Simba wa tawi la Mpira Pesa, wanatarajia kufanya mkutano Mkuu Oktoba sita mwaka huu katika Ukumbi wa Anex Magomeni Mikumi, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
Mkutano huo unafanyika kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayoihusu klabu yao wakiwa na lengo la kuhakikisha kuwa timu yao inafanya vizuri katika mechi za Ligi Kuu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tawi hilo la Mpira Pesa, Ustadh Masoud, alisema kuwa maandalizi ya mkutano huo yanaendelea kwa ajili ya kuufanikisha kwa vitendo.

Alisema aidha pia watajaribu kuangalia namna gani tawi lao linaendelea kuwa na nguvu katika tasnia ya mpira wa miguu hapa nchini ili mambo yao yaende vizuri.

MGODI UNAOTEMBEA: Chadema, leo mmeisahau ndoa ya CUF na CCM?



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WASWAHILI wana msemo wao, siku zote mla ndizi usahau, ila anayetupa maganda ni ngumu kusahau. Siku zote jambo hilo litakuwa kichwani mwake, akiwaza na kuwazua.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Huenda chuki ikawa ndani yake kwa kuangalia tukio hilo, ila yule aliyekula ndizi si ajabu akawa ameshasahau na kuendelea na maisha yake ya kila siku.

Nimejikuta nikianza hivi baada ya kuangalia muungano wa mashaka wa vyama vya upinzani Tanzania, kama vile Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama Cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi, inayoongozwa na James Mbatia.

Kabla sijaenda mbali zaidi, naomba niseme kuwa sina chuki na uamuzi wa muungano huo kwa wapinzani wala chuki ya viongozi wanaongoza vyama hivyo vya siasa vyenye hamu siku moja vishike dola.

Kwa wale wanaofuatilia siasa za Tanzania, watakumbuka jinsi CUF walivyotukanwa na kudhalilishwa na Chadema, ambao leo wamejirudi na kuunda muungano. Mara kadhaa CUF waliitwa sehemu ya CCM na kila walichohitaji kutenda, kilibezwa.

Tuesday, October 01, 2013

Extra Bongo wamlilia marehemu Watuguru


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya Extra Bongo, imestushwa na kifo cha mpiga gitaa wa bendi ya WK sound, Joseph Watuguru, aliyefariki juzi na kupangwa kuzikwa leo Kongowe jijini Dar es Salaam.
Marehemu Jose Watuguru kushoto enzi za uhai wake.
Watuguru aliwahi kutamba na bendi kadhaa hapa nchini, ikiwamo ile Mchinga Sound akiwa na wakali mbalimbali, hasa Mwinjuma Muumini maarufu kama kocha wa Dunia.
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, alisema kuwa kifo cha Watuguru ni pengo katika tasnia ya muziki wa dansi nchini.

Alisema marehemu alifariki kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya TB, huku akiacha mke na watoto wawili na msiba wake upo nyumbani kwa kaka yake Kongowe.

Khamis Tambwe mabao aumwa tumbo ghalfa


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
DAKTARI wa timu ya Simba, Yasin Gembe, amesema mshambuliaji wao Khamis Tambwe, amepata mvurugiko wa tumbo hivyo kukosa kufanya mazoezi ya asubuhi na wenzake.

Muda wote wa mazoezi, Tambwe alikuwa nje ya uwanja, hivyo kuzua hofu kwa wadau na mashabiki wa timu ya Simba wanaokoshwa na kasi ya mshambuliaji huo ndani ya uwanja.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Gembe alisema kuwa mshambuliaji wao Tambwe aliamka vibaya kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya ghafla ya tumbo.

Wakazi wa Kikuyu Kusini walivyoandamana kupinga bomoa bomoa mkoani Dodoma

 Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu  [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
  Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu  (CDA) wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akipaza sauti ya matumaini kwa wakazi wa Kata ya kikuyu kusini walioandamana kupinga Bomoabomoa ya CDA waliokuwa wamepanga kubomoa nyumba na misingi katika eneo hilo, ambapo aliwataka wakae chini na Mkurugenzi kutatua mgogoro huo kabla ya kubomoa.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...