Hapo sasa.
Watu weweeeee. Hapa vijana hawa ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara
moja wakionyeshana kazi katika harusi ya kijana mwenzao katika kijiji cha
Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Wenyewe wanasema raha zipo kila
mahali. Kama ulikuwa hujui haya hapo kama kawaida.
Saturday, September 07, 2013
Jeshi la Polisi wilayani Handeni kutangaza vita ya bange na gongo
Na Kambi Mbwana,
Handeni
JESHI la Polisi
wilayani Handeni, mkoani Tanga, limesema wilaya hiyo kwa sasa inakabiriwa na
changamoto ya matumizi ya bange na gongo, hivyo wanajipanga vilivyo kulidhibiti
suala hilo.
OCD wilayani Handeni, mkoani Tanga, Zuberi Chembera, akizungumza jambo na Handeni Kwetu Blog wilayani hapa.
Hayo yalisemwa na
Mkuu wa jeshi la Polisi wilayani humo, OCD Zuberi Chembera, alipotakiwa na
Handeni Kwetu Blog aelezee hali ya uhalifu katika maeneo yote ya Handeni.
OCD Chembera alisema
hali ya uhalifu kwa sasa wilayani humo imepungua kwa kasi na kubakia suala la
gongo na bange.
Ili kuchochea kasi ya maendeleo, watendaji wilayani Handeni waapa kufunga mkanda
Na Kambi Mbwana, Handeni
KATIBU Tawala wa
Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Jonh Ticky, amesema kwamba wameamua kufunga
mkanda kuhakikisha kuwa kasi yao inazidi kushika kasi kwa kufanya kazi bila
kuchoka na kuonyesha mfano kwa watendaji wengine wote.
Katibu Tawala wa Wilaya Handeni, mkoani Tanga, Jonh Ticky, pichani.
Akizungumza na
Handeni Kwetu Blog ofisini kwake, Ticky alisema kuwa mara kadhaa wamekuwa
wakifunga mkanda kuhamasisha pia ufanyaji wa kazi za kijamii badala ya
kusubiria kutoa maagizo.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani
Alisema hilo
limechangia kuharakisha maendeleo katika wilaya yao, sambamba na kutoa mwanya
wa kusubiri ‘madudu’ kutoka kwa watendaji wavivu.
MAMBO FULANI MUHIMU:Je, uliyekuwa naye ana mwingine ampendae?
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI wiki nyingine tena
msomaji wangu tunapokutana katika safu hii inayokujia kila Jumamosi, ikiwa na
lengo la kuelezea mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano na maisha.
Wawili wapendanao.
Nashukuru
kama wewe ni mpenzi wa safu hii kiasi cha kuwa pamoja kila Jumamosi. Kwa wewe
ambaye si shabiki zaidi, hivyo nakuombea ili tuwe wadau kwa ajili ya kujadili
mambo haya.
Ndugu
msomaji wangu, ni rahisi mno kujihusisha na mapenzi na waume au wake za watu
bila wewe mwenyewe kujua. Hii ni kutokana na baadhi yao kufanya siri katika
mambo haya.
Wapo
baadhi ya wanaume au wanawake wakiulizwa juu ya uhusiano wao, hukanusha vikali.
Mara kadhaa majibu yao ni kuwa wapo huru. Ati hawana uhusiano na mtu mwingine.
KWEINCHILI (2): Tufunge mkanda kwa maendeleo ya Handeni
Na Adam Seif
Malinda,
WIKI
iliyopita nilizungunzia umuhimu wa kuunganisha fikra za wana Handeni, ikiwa ni
demokrasia ya haki pale inapohitajika kuunganisha watu kutatua jambo fulani, ni
vema kila mtu akapata fursa ya kutoa ya moyoni.
Adam Seif Malinda, mwandishi wa safu hii.
Nilizungunzia
uwepo wa ardhi yenye rutuba, isiyohitaji mbolea ya viwandani, uwepo wa madini
ya dhahabu, uwepo wa misitu ya asili inayoteketezwa kwa kukata mkaa, bila kuwa
na jawabu makini la kutatua kero za umaskini.
Baba wa
taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishawahi kusema enzi ya uhai wake kuwa
hakuna umasikini mkubwa kama umasikini wa fikra.
Jambo hili
ni dhahili tunahitaji kulifikiria mara kadhaa katika vichwa vyetu, kwani
naamini wana Handeni hatuna umaskini wa fikra bali tuna umasikini wa kipato
ambao tunaweza kupambana nao.
Wednesday, September 04, 2013
Wabunge wa Upinzani watoka nje ya ukumbi wa Bunge kwa mara nyingine tena
KWA
mara nyingine tena baada ya kuwahi hivyo, wabunge kutoka Vyama vya upinzani leo wametoka nje ya baada
Naibu Spika kushindwa kutolea ufumbuzi hoja za upinzani.
Kwa
mujibu wa wabunge hao wa upinzani, Ndugai alikusudia kuwaburuza zaidi wabunge
hao baada ya baada ya kusimama Tundu Lisu kuuliza muongozo kuhusu kuleta mswaada
bila kuwahusisha Zanzibar huku Tanganyika wakihusishwa!
Sakata
hilo liliibua malalaamiko mengi kutoka bungeni na hatimae wabunge hao kuamua
kutoka nje ya Bunge.
|
JB awapa somo wasanii wa Tanzania
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
NYOTA wa filamu hapa
nchini, Jacob Stephen (JB), amesema ili sanaa ipige hatua ikiwamo ya uigizaji
na uimbaji, inahitaji mipango ya uhakika pamoja na kujituma kwa wasanii wote
kwenye kazi zao.
Msanii wa filamu Tanzania, Jacob Steephen JB.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, JB alisema kuwa wasanii wasiotambua hilo, hawawezi kusonga
mbele na kuendeleza soko lao.
Alisema ingawa muziki
hasa wa kizazi kipya na filamu unachanja mbuga, ila wanapaswa kuongeza bidii
kwa ajili ya kuwa juu zaidi.
Mtunisha misuri awa kivutio uzinduzi wa Simtank mpya
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MTUNISHA misuri
anayefanya vizuri katika sekta hiyo nchini, Mussa Mohamed maarufu kama 50 Cent,
alikuwa kivutio katika uzinduzi wa Simtank mpya, yanayozalishwa na Kampuni ya SILA
AFRICA.
Mtunisha misuri anayejulikana kwa jina la Mussa Mohamed, akipamba uzinduzi wa SimTank jana, jijini Dar es Salaam.Kulia na kushoto kwake ni mabinti waliokuwa wakishiriki nao kwenye hafla hiyo ya aina yake.
Akizungumza katika
uzinduzi huo, mtunisha misuri huyo ambaye pia alishiriki katika mashindano
mbalimbali likiwamo la Dume Condom, alisema kuwa ni fahari yake kuwa kwenye
uzinduzi huo.
Alisema kuwa sekta
yao hiyo ya kutunisha misuri imekuwa kwenye nafasi nzuri kwasababu ya kutumiwa
na makampuni makubwa.
MGODI UNAOTEMBEA:Hoja ya uhamiaji isiishie mkoani Kagera
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UHAMIAJI haramu ni ile hali ya mtu wa Taifa lingine kuingia kwenye
nchi nyingine bila kufuata sheria. Kwa mfano, raia wa Rwanda kuingia Tanzania
kienyeji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Hafuati utaratibu uliowekwa na nchi huru yenye mamlaka zake. Huyo
anavunja sheria, hivyo kwa ujio wake huo, anaweza kufanya vyovyote anavyotaka.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bernard Membe.
Hali hii ya uhamiaji haramu si ngeni duniani. Kumekuwa na
mwingiliano na sababu nyingi zinazowafanya watu watamani kuingia katika nchi
nyingine bila kupiga hodi.
Kila siku wanasikika waliokamatwa baada ya jaribio lao la kuzamia
kushindwa. Wapo wanaorudishwa makwao bila kupenda na wale pia wanaowekwa
kizuizini.
Wakati tunaangalia jambo hilo, lazima tukubali kuwa sheria zetu,
utendaji kazi wetu umewapa urahisi watu wengi kuingia Tanzania soni.
Serikali yazitaka kampuni kutumia njia za kisasa usafirishaji wa fedha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Patrick
Makungu, amezitaka kampuni za kibiashara zilizopo nchini kutumia mbinu za
kisasa za usafirishaji wa fedha ili kuepuka hasara zinazoweza kusababishwa na
matukio ya wizi hususani uporaji.
Makungu alitoa rai hiyo hivi karibuni Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa wa mpango wa pamoja katika masuala ya teknohama kwa kampuni za Techno Brain na SAP, wenye lengo la kuboresha utendaji katika sekta mbalimbali za kibiashara nchini.
Alisema katika kipindi hiki ambacho Taifa linashuhudia ukuaji mkubwa wa masuala ya teknolojia, umefika wakati makampuni ya kibiashara yakaangalia namna yanavyoweza kubadili mfumo wake wa usafirishaji wa fedha ili kuepuka hasara zisizo za lazima wanazoweza kuzipata.
Makungu alitoa rai hiyo hivi karibuni Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa wa mpango wa pamoja katika masuala ya teknohama kwa kampuni za Techno Brain na SAP, wenye lengo la kuboresha utendaji katika sekta mbalimbali za kibiashara nchini.
Alisema katika kipindi hiki ambacho Taifa linashuhudia ukuaji mkubwa wa masuala ya teknolojia, umefika wakati makampuni ya kibiashara yakaangalia namna yanavyoweza kubadili mfumo wake wa usafirishaji wa fedha ili kuepuka hasara zisizo za lazima wanazoweza kuzipata.
Dkt Elemi alivyoangushiwa sherehe ya kuzaliwa ya aina yake
Dkt.Elmi na Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura wakiwa wameshikana mikonon kwa pamoja wakioneshana upendo na mapenzi teeele,usiku wa leo kwenye sherehe yao.
Dkt.Elmi na Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura wakiwa katika picha ya kumbukumbu kabla ya tukio adhimu la kukata keki
Dkt.Elmi akimlisha keki ya upendo na kwa madaha kabisa,Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura jioni ya leo.
Tuesday, September 03, 2013
Simtank yazindua tenki la aina yake na kushangaza wengi
Tenki linakandamizwa huku watu wakishuhudia. Kushoto ni Meneja Mkuu wa SILA AFRICA, Alpesh Patel.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya SILA AFRICA leo imezindua matenki mapya kutoka
SIMTANK yenye kiwango cha juu ubora pamoja na uimara wake.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Mkuu wa kampuni
hiyo, Alpesh Patel alisema matenki hayo yanaweza kukandamizwa bila kupasuka
wala kutoboka.
Meneja Mkuu wa SILA AFRICA, wazalishaji wa Simtank, Alpesh Patel akionyesha tenki lililokandamizwa na baadaye kunyooshwa kwa mikono ya binadamu wa kawaida na kukaa sawa. Picha zote na Kambi Mbwana..
Alisema anaamini wateja wao watapata bidhaa bora kutoka
kwenye kampuni yao hiyo iliyokuja na jambo linaloshangaza wengi.
Monday, September 02, 2013
Copa Coca-Cola zaanza kwa sare ya 2-2 kwa Ilala Kaskazini Unguja
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Timu
za Ilala na Kaskazini Unguja zimetoka sare ya mabao 3-3 katika moja ya
mechi za ufunguzi za michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 15 iliyoanza leo (Septemba 2 mwaka huu) katika vituo
mbalimbali nchini.
Wafungaji
wa Ilala katika mechi hiyo iliyochezwa asubuhi Uwanja wa Tamco ulioko
Kibaha, Pwani yalifungwa na Ally Shaban (mawili) wakati lingine
lilifungwa na Haruni Said. Mabao ya Kaskazini Unguja yalifungwa na Jecha
Ally (mawili) na Shehe Ally.
Katika
kituo cha Mbeya, Njombe imeanza vizuri baada ya kuifunga Katavi mabao
2-1. Mabao ya washindi yalifungwa na Rackson Mligo dakika ya 13 wakati
lingine lilifungwa na Kelvin Gama dakika kumi kabla ya filimbi ya
mwisho.
Henry Joseph arudi Tanzania kwa bahati ya kuitwa tena Stars
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemjumuisha mchezaji Henry Joseph wa
Simba kwenye kikosi chake kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la
Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen, pichani
Tayari
Joseph amesharipoti kwenye kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya
Accomondia jijini Dar es Salaam. Taifa Stars ambayo iko chini ya
udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29
mwaka huu, na leo jioni itafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume.
Programu
ya timu hiyo inaonesha kuwa kesho (Septemba 3 mwaka huu) itafanya
mazoezi yake asubuhi na jioni kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya
Karume.
SIWEZI KUVUMILIA:Hongera Cheka, tunaokuthamini tupo nyuma yako
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
WATANZANIA wenye
mapenzi mema na mchezo wa ngumi lazima waheshimu mchango wa bondia Francis
Cheka. Huyu ni bondia mwenye makali ya kutosha.
Bingwa wa Dunia, Francis Cheka, pichani.
Kila anapoingia
ulingoni amekuwa akifanya vitu vya kufurahisha wadau wa ngumi kutokana na
kufanikiwa kuibuka na ushindi, hivyo kuzidi kukuza jina lake.
Baada ya kuwapiga
mabondia mbalimbali kutoka Tanzania na nchi kadhaa za Afrika, Ijumaa iliyopita,
Cheka alifanya tena maajabu kwa kumtandika Phil Williams, bondia kutoka nchini
Marekani.
Pambano hilo la
Ubingwa wa Dunia mkanda wa (WBF) na kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee,
Cheka alishinda kwa pointi.
roli la mizigo lagongana na hiace na kuua kadhaa, Mkata, wilayani Handeni mkoani Tanga usiku wa kuamkia leo
HABARI zilizotufikia usiku ni kuwa watu kadhaa wanahofiwa kufariki
katika ajali ya gari iliyotokea Mkata, wilayani Handeni, mkoani Tanga usiku wa
kuamkia leo baada ya gari aina hiace kugongana na roli la mizigo katika barabara
hiyo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa
walisema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha inaweza kufikia watatu hadi
saba.
Juhudi za kupata kwa kirefu
ajali hiyo pamoja na kuzungumza na Kamanda wa Polisi mkoani Tanga zinafanyika.
Sunday, September 01, 2013
Simba kuwatambulisha nyota watatu wapya kesho, akiwamo Henry Joseph
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KLABU ya Simba inayodhaminiwa na Bia ya KILIMANJARO
inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa vyombo vya habari ili hatimaye taarifa hii
iwafikie wapenzi na washabiki wake popote pale walipo.
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga
Mara baada ya safari ya mikoa ya Tabora na Arusha kwenye mechi mbili za awali
za Ligi Kuu ya Tanzania, timu ya Simba imerejea salama jijini Dar es Salaam
ikiwa na kikosi chake kamili tayari kujiandaa na mechi ijayo ya ligi dhidi ya
Mtibwa Sugar ya Morogoro iliyopangwa kuchezwa Septemba 14 mwaka huu.
Kama sehemu ya maandalizi ya mechi hiyo, kikosi cha Simba kitashuka dimbani
katika Uwanja Mkuu wa Taifa siku ya kesho, Jumatatu Septemba 2, kucheza na
Mafunzo ya Zanzibar katika mechi ambayo ina faida nyingine zaidi ya kuwa ya
kujiandaa na mechi ya Mtibwa.
Kocha Stars amuita Mkude kuivaa Gambia, Ujerumani yaombea ITC watatu Tanzania
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars
kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia
itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen
amemuongeza mchezaji huyo ili kuimarisha sehemu ya kiungo. Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29
mwaka huu kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, timu hiyo imefanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu
ya Karume wakati kesho Jumatatu (Septemba 2 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya
mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mtoto Salha Ibrahim Mabewa akusanya watu katika HAKIKA yake iliyoambatana na kutimiza siku 40 tangu alipozaliwa
Watoto hawa wa Madrassa wakipata chai katika HAKIKA ya mtoto Salha Ibrahim Mabewa maeneo ya Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Kambi Mbwana.
Baada ya kisomo kumalizika na mtoto Salha Ibrahim Mabewa kutolewa nje katika shughuli ya HAKIKA yake iliyofanyika leo Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam, watu walianza kugawa chai kama wanavyoonekana hapo waandaazi wakiwa busy kuwalaki wahudhuriaji wao.
Baada ya kisomo kumalizika na mtoto Salha Ibrahim Mabewa kutolewa nje katika shughuli ya HAKIKA yake iliyofanyika leo Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam, watu walianza kugawa chai kama wanavyoonekana hapo waandaazi wakiwa busy kuwalaki wahudhuriaji wao.
Mtoto Salha Ibrahim Mabewa, akitolewa nje katika shughuli ya
HAKIKA yake iliyofanyika leo Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam. Aliyembeba
ni babu yake aliyejulikana kwa jina la Mzee Rajabu, ambapo pia alitumia fursa
hiyo ya kumtembeza kwa wageni waalikwa na wahudhuriaji wa tukio hilo la aina
yake kwa mjukuu wake huyo. Handeni Kwetu
Blog inamtakia maisha mema na yenye mafanikio mtoto Salha katika kipindi chote
cha uhai wake. Picha zote na Kambi Mbwana.
Pitia maoni ya Rasimu ya Katiba ya Chama cha siasa NRA
MAONI YA NRA
NI KAMA IFUATAVYO;
SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
1(1)Tunakubaliana na SERIKALI TATU .
SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
1(1)Tunakubaliana na SERIKALI TATU .
Naibu Katibu Mkuu wa NRA
SASABU:Imekuwa ni kilio cha muda mrefu cha washiriki wa Muungano huu kila mmoja juu ya serikalai yake yenye mamlaka kwa watu wake na hata ukizingatia nchi hizi zilikuwa na historia zake, na kila moja ilikuwa chini ya utawala mwingine wa kikoloni, zilipata Uhuru wao kwa njia tofauti na tarehe tofauti, hivyo ili kuufanya Muungano wenye nguvu na uhalali ni kuwa na serikali hizi tatu zitakazokuwa na mabunge matatu.
NA Ili kuleta maana sahihi ya matumizi wa Maneno, Katika Rasimu hii ya
Katiba,Kila panaposomeka ‘TANZANIA BARA’ ,badala yake isomeke ‘JAMHURI YA WATU
WA TANGANYIKA’, na Kila panaposomeka ‘TANZANIA ZANZIBAR ’ badala yake isomeka
‘JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR’
Sababu 1:Majina haya mawili ndio yatakayotoa jina la Tanzania, na hivyo kuwa na ‘JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA’
Sababu 1:Majina haya mawili ndio yatakayotoa jina la Tanzania, na hivyo kuwa na ‘JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA’
Sababu 2:Kuleta maana halisi ya muungano huu ni kuwa kuna wananchi wa pande
mbili walioungana na kupata Neno ’JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA’ hivyo maneno
‘WATU WA’ katika upande wa Tanganyika na Zanzibar linawawakilisha wananchi moja
kwa moja , kwa kuwa , wao ndio walengwa katika Muungano huu.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NRA
Pia tunapendekeza ‘KUONGEZWA ANNEX PAGE’ mwisho wa Katiba hii, iweke wazi eneo
litakalotiwa saini na viongozi wa nchi hizi mbili.
Sababu:Suala la hati ya Muungano limekuwa ni tatizo,watanzania kwa vipindi tofauti wamekuwa wakihoji suala la makubaliano ya muungano,hivyo kurasa hii ya nyongeza ikionyeshe Nani anawakilisha upande mmoja ,lini wanasaini,na kama kuna makubaliano yoyote yaanishwe katika kurasa hii ili kujenga imani kwa wananchi wa nchi hizi mbili.
Sababu:Suala la hati ya Muungano limekuwa ni tatizo,watanzania kwa vipindi tofauti wamekuwa wakihoji suala la makubaliano ya muungano,hivyo kurasa hii ya nyongeza ikionyeshe Nani anawakilisha upande mmoja ,lini wanasaini,na kama kuna makubaliano yoyote yaanishwe katika kurasa hii ili kujenga imani kwa wananchi wa nchi hizi mbili.
Kigi Makasi kuwaaga Simba kesho tayari kuelekea nchini India
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSAKATA kabumbu wa Simba, Kigi Makasi, anatarajia kuwaaga mashabiki wao katika mechi ya kesho
dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar, mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini
Dar es Salaam.
Mchezaji wa Simba, Kigi Makasi, pichani.
Makasi anatarajiwa
kuondoka Tanzania kuelekea nchini India kwa matibabu yake ya goti baada ya
kuumia katika mechi za mzunguuko wa pili msimu uliopita.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa mchezaji
wao huyo atatumia mechi hiyo kuwaaga mashabiki na wanachama ili wamuombee dua
katika safari yake hiyo ya nchini India.
Subscribe to:
Posts (Atom)














