https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, September 07, 2013

Jeshi la Polisi wilayani Handeni kutangaza vita ya bange na gongo



Na Kambi Mbwana, Handeni
JESHI la Polisi wilayani Handeni, mkoani Tanga, limesema wilaya hiyo kwa sasa inakabiriwa na changamoto ya matumizi ya bange na gongo, hivyo wanajipanga vilivyo kulidhibiti suala hilo.
OCD wilayani Handeni, mkoani Tanga, Zuberi Chembera, akizungumza jambo na Handeni Kwetu Blog wilayani hapa.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa jeshi la Polisi wilayani humo, OCD Zuberi Chembera, alipotakiwa na Handeni Kwetu Blog aelezee hali ya uhalifu katika maeneo yote ya Handeni.

OCD Chembera alisema hali ya uhalifu kwa sasa wilayani humo imepungua kwa kasi na kubakia suala la gongo na bange.

Ili kuchochea kasi ya maendeleo, watendaji wilayani Handeni waapa kufunga mkanda



Na Kambi Mbwana, Handeni
KATIBU Tawala wa Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Jonh Ticky, amesema kwamba wameamua kufunga mkanda kuhakikisha kuwa kasi yao inazidi kushika kasi kwa kufanya kazi bila kuchoka na kuonyesha mfano kwa watendaji wengine wote.
Katibu Tawala wa Wilaya Handeni, mkoani Tanga, Jonh Ticky, pichani.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog ofisini kwake, Ticky alisema kuwa mara kadhaa wamekuwa wakifunga mkanda kuhamasisha pia ufanyaji wa kazi za kijamii badala ya kusubiria kutoa maagizo.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani
Alisema hilo limechangia kuharakisha maendeleo katika wilaya yao, sambamba na kutoa mwanya wa kusubiri ‘madudu’ kutoka kwa watendaji wavivu.

MAMBO FULANI MUHIMU:Je, uliyekuwa naye ana mwingine ampendae?


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI wiki nyingine tena msomaji wangu tunapokutana katika safu hii inayokujia kila Jumamosi, ikiwa na lengo la kuelezea mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano na maisha.
Wawili wapendanao.
Nashukuru kama wewe ni mpenzi wa safu hii kiasi cha kuwa pamoja kila Jumamosi. Kwa wewe ambaye si shabiki zaidi, hivyo nakuombea ili tuwe wadau kwa ajili ya kujadili mambo haya.

Ndugu msomaji wangu, ni rahisi mno kujihusisha na mapenzi na waume au wake za watu bila wewe mwenyewe kujua. Hii ni kutokana na baadhi yao kufanya siri katika mambo haya.

Wapo baadhi ya wanaume au wanawake wakiulizwa juu ya uhusiano wao, hukanusha vikali. Mara kadhaa majibu yao ni kuwa wapo huru. Ati hawana uhusiano na mtu mwingine.

KWEINCHILI (2): Tufunge mkanda kwa maendeleo ya Handeni



Na Adam Seif Malinda,     
WIKI iliyopita nilizungunzia umuhimu wa kuunganisha fikra za wana Handeni, ikiwa ni demokrasia ya haki pale inapohitajika kuunganisha watu kutatua jambo fulani, ni vema kila mtu akapata fursa ya kutoa ya moyoni.
                Adam Seif Malinda, mwandishi wa safu hii.
Nilizungunzia uwepo wa ardhi yenye rutuba, isiyohitaji mbolea ya viwandani, uwepo wa madini ya dhahabu, uwepo wa misitu ya asili inayoteketezwa kwa kukata mkaa, bila kuwa na jawabu makini la kutatua kero za umaskini.

Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishawahi kusema enzi ya uhai wake kuwa hakuna umasikini mkubwa kama umasikini wa fikra.

Jambo hili ni dhahili tunahitaji kulifikiria mara kadhaa katika vichwa vyetu, kwani naamini wana Handeni hatuna umaskini wa fikra bali tuna umasikini wa kipato ambao tunaweza kupambana nao.

Wednesday, September 04, 2013

Wabunge wa Upinzani watoka nje ya ukumbi wa Bunge kwa mara nyingine tena

PICHA MAKTABA

KWA mara nyingine tena baada ya kuwahi hivyo, wabunge kutoka Vyama vya upinzani leo wametoka nje ya baada Naibu Spika kushindwa kutolea ufumbuzi hoja za upinzani.

Kwa mujibu wa wabunge hao wa upinzani, Ndugai alikusudia kuwaburuza zaidi wabunge hao baada ya baada ya kusimama Tundu Lisu kuuliza muongozo kuhusu kuleta mswaada bila kuwahusisha Zanzibar huku Tanganyika wakihusishwa!

Sakata hilo liliibua malalaamiko mengi kutoka bungeni na hatimae wabunge hao kuamua kutoka nje ya Bunge.

JB awapa somo wasanii wa Tanzania


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NYOTA wa filamu hapa nchini, Jacob Stephen (JB), amesema ili sanaa ipige hatua ikiwamo ya uigizaji na uimbaji, inahitaji mipango ya uhakika pamoja na kujituma kwa wasanii wote kwenye kazi zao.
Msanii wa filamu Tanzania, Jacob Steephen JB.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, JB alisema kuwa wasanii wasiotambua hilo, hawawezi kusonga mbele na kuendeleza soko lao.

Alisema ingawa muziki hasa wa kizazi kipya na filamu unachanja mbuga, ila wanapaswa kuongeza bidii kwa ajili ya kuwa juu zaidi.

Mtunisha misuri awa kivutio uzinduzi wa Simtank mpya


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MTUNISHA misuri anayefanya vizuri katika sekta hiyo nchini, Mussa Mohamed maarufu kama 50 Cent, alikuwa kivutio katika uzinduzi wa Simtank mpya, yanayozalishwa na Kampuni ya SILA AFRICA.
Mtunisha misuri anayejulikana kwa jina la Mussa Mohamed, akipamba uzinduzi wa SimTank jana, jijini Dar es Salaam.Kulia na kushoto kwake ni mabinti waliokuwa wakishiriki nao kwenye hafla hiyo ya aina yake.

Akizungumza katika uzinduzi huo, mtunisha misuri huyo ambaye pia alishiriki katika mashindano mbalimbali likiwamo la Dume Condom, alisema kuwa ni fahari yake kuwa kwenye uzinduzi huo.

Alisema kuwa sekta yao hiyo ya kutunisha misuri imekuwa kwenye nafasi nzuri kwasababu ya kutumiwa na makampuni makubwa.

MGODI UNAOTEMBEA:Hoja ya uhamiaji isiishie mkoani Kagera


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UHAMIAJI haramu ni ile hali ya mtu wa Taifa lingine kuingia kwenye nchi nyingine bila kufuata sheria. Kwa mfano, raia wa Rwanda kuingia Tanzania kienyeji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Hafuati utaratibu uliowekwa na nchi huru yenye mamlaka zake. Huyo anavunja sheria, hivyo kwa ujio wake huo, anaweza kufanya vyovyote anavyotaka.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bernard Membe.

Hali hii ya uhamiaji haramu si ngeni duniani. Kumekuwa na mwingiliano na sababu nyingi zinazowafanya watu watamani kuingia katika nchi nyingine bila kupiga hodi.

Kila siku wanasikika waliokamatwa baada ya jaribio lao la kuzamia kushindwa. Wapo wanaorudishwa makwao bila kupenda na wale pia wanaowekwa kizuizini.

Wakati tunaangalia jambo hilo, lazima tukubali kuwa sheria zetu, utendaji kazi wetu umewapa urahisi watu wengi kuingia Tanzania soni.

Serikali yazitaka kampuni kutumia njia za kisasa usafirishaji wa fedha

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu  wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Patrick Makungu, amezitaka kampuni za kibiashara zilizopo nchini kutumia mbinu za kisasa za usafirishaji wa fedha ili kuepuka hasara zinazoweza kusababishwa na matukio ya wizi hususani uporaji.

Makungu alitoa rai hiyo hivi karibuni Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa wa mpango wa pamoja katika masuala ya teknohama kwa kampuni za Techno Brain na SAP, wenye lengo la kuboresha utendaji  katika sekta mbalimbali za kibiashara nchini.

Alisema katika kipindi hiki ambacho Taifa linashuhudia ukuaji mkubwa wa masuala ya teknolojia, umefika wakati makampuni ya kibiashara yakaangalia namna yanavyoweza kubadili mfumo wake wa usafirishaji wa fedha ili kuepuka hasara zisizo za lazima wanazoweza kuzipata.

Dkt Elemi alivyoangushiwa sherehe ya kuzaliwa ya aina yake

 Dkt.Elmi na Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura wakiwa wameshikana mikonon kwa pamoja wakioneshana upendo na mapenzi teeele,usiku wa leo kwenye sherehe yao.
 Dkt.Elmi na Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura wakiwa katika picha ya kumbukumbu kabla ya tukio adhimu la kukata keki
 Dkt.Elmi akimlisha keki ya upendo na kwa madaha kabisa,Mkewe almaarufu kwa jina la Anti Ashura  jioni ya leo.

Tuesday, September 03, 2013

Simtank yazindua tenki la aina yake na kushangaza wengi

Tenki linakandamizwa huku watu wakishuhudia. Kushoto ni Meneja Mkuu wa SILA AFRICA, Alpesh Patel.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya SILA AFRICA leo imezindua matenki mapya kutoka SIMTANK yenye kiwango cha juu ubora pamoja na uimara wake.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Alpesh Patel alisema matenki hayo yanaweza kukandamizwa bila kupasuka wala kutoboka.
Meneja Mkuu wa SILA AFRICA, wazalishaji wa Simtank, Alpesh Patel akionyesha tenki lililokandamizwa na baadaye kunyooshwa kwa mikono ya binadamu wa kawaida na kukaa sawa. Picha zote na Kambi Mbwana..

Alisema anaamini wateja wao watapata bidhaa bora kutoka kwenye kampuni yao hiyo iliyokuja na jambo linaloshangaza wengi.

Monday, September 02, 2013

Copa Coca-Cola zaanza kwa sare ya 2-2 kwa Ilala Kaskazini Unguja

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Timu za Ilala na Kaskazini Unguja zimetoka sare ya mabao 3-3 katika moja ya mechi za ufunguzi za michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 iliyoanza leo (Septemba 2 mwaka huu) katika vituo mbalimbali nchini.

Wafungaji wa Ilala katika mechi hiyo iliyochezwa asubuhi Uwanja wa Tamco ulioko Kibaha, Pwani yalifungwa na Ally Shaban (mawili) wakati lingine lilifungwa na Haruni Said. Mabao ya Kaskazini Unguja yalifungwa na Jecha Ally (mawili) na Shehe Ally.

Katika kituo cha Mbeya, Njombe imeanza vizuri baada ya kuifunga Katavi mabao 2-1. Mabao ya washindi yalifungwa na Rackson Mligo dakika ya 13 wakati lingine lilifungwa na Kelvin Gama dakika kumi kabla ya filimbi ya mwisho.

Henry Joseph arudi Tanzania kwa bahati ya kuitwa tena Stars

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemjumuisha mchezaji Henry Joseph wa Simba kwenye kikosi chake kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen, pichani
Tayari Joseph amesharipoti kwenye kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Taifa Stars ambayo iko chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu, na leo jioni itafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Programu ya timu hiyo inaonesha kuwa kesho (Septemba 3 mwaka huu) itafanya mazoezi yake asubuhi na jioni kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Karume.

SIWEZI KUVUMILIA:Hongera Cheka, tunaokuthamini tupo nyuma yako


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WATANZANIA wenye mapenzi mema na mchezo wa ngumi lazima waheshimu mchango wa bondia Francis Cheka. Huyu ni bondia mwenye makali ya kutosha.
Bingwa wa Dunia, Francis Cheka, pichani.
Kila anapoingia ulingoni amekuwa akifanya vitu vya kufurahisha wadau wa ngumi kutokana na kufanikiwa kuibuka na ushindi, hivyo kuzidi kukuza jina lake.

Baada ya kuwapiga mabondia mbalimbali kutoka Tanzania na nchi kadhaa za Afrika, Ijumaa iliyopita, Cheka alifanya tena maajabu kwa kumtandika Phil Williams, bondia kutoka nchini Marekani.

Pambano hilo la Ubingwa wa Dunia mkanda wa (WBF) na kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Cheka alishinda kwa pointi.

roli la mizigo lagongana na hiace na kuua kadhaa, Mkata, wilayani Handeni mkoani Tanga usiku wa kuamkia leo



HABARI zilizotufikia usiku ni kuwa watu kadhaa wanahofiwa kufariki katika ajali ya gari iliyotokea Mkata, wilayani Handeni, mkoani Tanga usiku wa kuamkia leo baada ya gari aina hiace kugongana na roli la mizigo katika barabara hiyo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa walisema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha inaweza kufikia watatu hadi saba.

Juhudi za kupata kwa kirefu ajali hiyo pamoja na kuzungumza na Kamanda wa Polisi mkoani Tanga zinafanyika.


Sunday, September 01, 2013

Simba kuwatambulisha nyota watatu wapya kesho, akiwamo Henry Joseph



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KLABU ya Simba inayodhaminiwa na Bia ya KILIMANJARO inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa vyombo vya habari ili hatimaye taarifa hii iwafikie wapenzi na washabiki wake popote pale walipo.
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga
Mara baada ya safari ya mikoa ya Tabora na Arusha kwenye mechi mbili za awali za Ligi Kuu ya Tanzania, timu ya Simba imerejea salama jijini Dar es Salaam ikiwa na kikosi chake kamili tayari kujiandaa na mechi ijayo ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro iliyopangwa kuchezwa Septemba 14 mwaka huu.
 
Kama sehemu ya maandalizi ya mechi hiyo, kikosi cha Simba kitashuka dimbani katika Uwanja Mkuu wa Taifa siku ya kesho, Jumatatu Septemba 2, kucheza na Mafunzo ya Zanzibar katika mechi ambayo ina faida nyingine zaidi ya kuwa ya kujiandaa na mechi ya Mtibwa.

Kocha Stars amuita Mkude kuivaa Gambia, Ujerumani yaombea ITC watatu Tanzania



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemuongeza mchezaji huyo ili kuimarisha sehemu ya kiungo. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, timu hiyo imefanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wakati kesho Jumatatu (Septemba 2 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mtoto Salha Ibrahim Mabewa akusanya watu katika HAKIKA yake iliyoambatana na kutimiza siku 40 tangu alipozaliwa

 Watoto hawa wa Madrassa wakipata chai katika HAKIKA ya mtoto Salha Ibrahim Mabewa maeneo ya Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Kambi Mbwana.
 Baada ya kisomo kumalizika na mtoto Salha Ibrahim Mabewa kutolewa nje katika shughuli ya HAKIKA yake iliyofanyika leo Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam, watu walianza kugawa chai kama wanavyoonekana hapo waandaazi wakiwa busy kuwalaki wahudhuriaji wao.
Mtoto Salha Ibrahim Mabewa, akitolewa nje katika shughuli ya HAKIKA yake iliyofanyika leo Magomeni Makuti, jijini Dar es Salaam. Aliyembeba ni babu yake aliyejulikana kwa jina la Mzee Rajabu, ambapo pia alitumia fursa hiyo ya kumtembeza kwa wageni waalikwa na wahudhuriaji wa tukio hilo la aina yake kwa mjukuu wake huyo. Handeni  Kwetu Blog inamtakia maisha mema na yenye mafanikio mtoto Salha katika kipindi chote cha uhai wake. Picha zote na Kambi Mbwana.

Pitia maoni ya Rasimu ya Katiba ya Chama cha siasa NRA

MAONI YA NRA NI KAMA IFUATAVYO;
SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
1(1)Tunakubaliana na SERIKALI TATU .

 
Naibu Katibu Mkuu wa NRA
SASABU:Imekuwa ni kilio cha muda mrefu cha washiriki wa Muungano huu kila mmoja juu ya serikalai yake yenye mamlaka kwa watu wake na hata ukizingatia nchi hizi zilikuwa na historia zake, na kila moja ilikuwa chini ya utawala mwingine wa kikoloni, zilipata Uhuru wao kwa njia tofauti na tarehe tofauti, hivyo ili kuufanya Muungano wenye nguvu na uhalali ni kuwa na serikali hizi tatu zitakazokuwa na mabunge matatu.

NA Ili kuleta maana sahihi ya matumizi wa Maneno, Katika Rasimu hii ya Katiba,Kila panaposomeka ‘TANZANIA BARA’ ,badala yake isomeke ‘JAMHURI YA WATU WA TANGANYIKA’, na Kila panaposomeka ‘TANZANIA ZANZIBAR ’ badala yake isomeka ‘JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR’
Sababu 1:Majina haya mawili ndio yatakayotoa jina la Tanzania, na hivyo kuwa na ‘JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA’
 
Sababu 2:Kuleta maana halisi ya muungano huu ni kuwa kuna wananchi wa pande mbili walioungana na kupata Neno ’JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA’ hivyo maneno ‘WATU WA’ katika upande wa Tanganyika na Zanzibar linawawakilisha wananchi moja kwa moja , kwa kuwa , wao ndio walengwa katika Muungano huu.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NRA
Pia tunapendekeza ‘KUONGEZWA ANNEX PAGE’ mwisho wa Katiba hii, iweke wazi eneo litakalotiwa saini na viongozi wa nchi hizi mbili.
Sababu:Suala la hati ya Muungano limekuwa ni tatizo,watanzania kwa vipindi tofauti wamekuwa wakihoji suala la makubaliano ya muungano,hivyo kurasa hii ya nyongeza ikionyeshe Nani anawakilisha upande mmoja ,lini wanasaini,na kama kuna makubaliano yoyote yaanishwe katika kurasa hii ili kujenga imani kwa wananchi wa nchi hizi mbili.

Kigi Makasi kuwaaga Simba kesho tayari kuelekea nchini India


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSAKATA kabumbu wa Simba, Kigi Makasi, anatarajia kuwaaga mashabiki wao katika mechi ya kesho dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar, mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Simba, Kigi Makasi, pichani.
Makasi anatarajiwa kuondoka Tanzania kuelekea nchini India kwa matibabu yake ya goti baada ya kuumia katika mechi za mzunguuko wa pili msimu uliopita.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa mchezaji wao huyo atatumia mechi hiyo kuwaaga mashabiki na wanachama ili wamuombee dua katika safari yake hiyo ya nchini India.

Saturday, August 31, 2013

MAMBO FULANI MUHIMU:Umegundua nini kwa umpendae, chukua hatua

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KUNA watu ambao wanaendelea kuingia kwenye wasiwasi mkubwa kwasababu ya kutofurahia uhusiano wao au ndoa yao kwa wale waliofanikiwa.
Mambo Fulani Muhimu kwa watu muhimu.
Hawa ni wale wanaoshi bila hata kugundua namna gani ya kuwafurahisha watu wao.

Ni wale ambao licha ya kutarajia makubwa kutoka kwa wapenzi wao, ila wametumbukia katika wasiwasi wa aina yake.

Ndugu msomaji wangu, katika uhusiano wa kimapenzi, kuna wale ambao wapo pamoja lakini wanapokuwa kwenye tendo la ndoa, mmoja wapo haridhiki.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...