Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HATUA ya kwanza ya usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2013/2014 imefungwa
rasmi jana (Agosti 5 mwaka huu) ambapo klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) zimewasilisha usajili wa vikosi vyao ndani ya wakati.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, pichani
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa baadhi
ya klabu zimefanya makosa madogo madogo katika usajili ambapo zimepewa
siku ya leo (Agosti 6 mwaka huu) kufanyia marekebisho kasoro hizo. Hivyo
kesho (Agosti 7 mwaka huu) majina ya vikosi vyote yatabandikwa kwenye
mbao za matangazo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa
ajili ya kipindi cha pingamizi kitakachomalizika Agosti 12 mwaka huu.




















