https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, July 03, 2013

Mhuburi wa nchini Uganda akamatwa mjini Iringa kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu

Mhubiri Raia  wa Uganda Richard Mwangusi, akiwa  chini ya ulinzi wa polisi  usiku  huu baada  ya kutuhumiwa kujipatia  fedha kwa njia ya udanganyifu.
Kamanda  wa  Polisi  Mkoa  wa Iringa (RPC) Ramadhan Mungi akitoka  Kituo  Cha  Polisi mjini Iringa, anaposhikiliwa mhubiri huyo wa nchini Uganda, akituhumiwa kuwa amejipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Askari Polisi  Mkoa  wa Iringa,  wakiwa nje ya  Kituo Cha  Polisi anaposhikiliwa mhubiri  huyo mwenye asili ya nchini Uganda kwa madai kuwa amejipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

MGODI UNAOTEMBEA: Sugu amesafishwa kwa tuhuma za kumtusi Waziri Mkuu Mizengo Pinda?


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KILA mtu anajua kuwa sheria na haki ni vitu viwili tofauti. Usilazimishe kupata haki, kwasababu sheria imeonyesha juu ya madai yako.
Kufanya hivyo ni kujipotezea muda wako unaoweza kuutumia katika kazi nyingine za maendeleo yako.
 Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu'


Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Pamoja n ayote hayo, lakini wakati mwingine si sahihi kujificha kwenye mhimili wa kisheria kwa kufanya mambo ambayo ni tofauti katika jamii.
Kila mmoja anapaswa kuishi kwa upendo bila kuweka u-mimi, vyama vyetu na mengineyo pia.

Nasema haya baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama ‘Sugu’kutoka (CHADEMA)kuachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Mkoa wa Dodoma, kwa madai kuwa hati ya mashitaka ina mapungufu kisheria.

Tuesday, July 02, 2013

Wasanii Tamasha la Filamu Grand Malt watoa msaada jijini Mwanza

Picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Sehemu ya vyandarua vilivyotolewa msaada vikiwa tayari vimefungwa na wasanii wa filamu hapa nchini,mara baada ya kutoa msaada wa vyandarua hivyo ndani ya wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Mkoa wa jiji la Mwanza-Sekou-toure mapema leo asubuhi kwa udhamini mkubwa wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grandmalt.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
WASANII maarufu wa Bongo Movie hapa nchini, ambao wapo hapa kwa ajili ya Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ jana walikabidhi vyandarua kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure.

Akizungumza na wasanii hao, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hassan Hida, aliwashukuru wasanii hao kwa msaada huo na kuwataka wawasaidie pia wasanii wachanga wa jijini hapa ili nao waweze kutoka.

Tanzania yamuaga kwa shangwe Rais Barack Obama wakati anaondoka leo kuelekea nchini kwao Marekani

Na Rahimu Kambi, Dar es Salaam
RAIS wa Marekani, Barack Obama, ameondoka muda mchache kuelekea nyumbani kwao, huku akiacha historia katika mataifa haya mawili, Tanzania na Marekani.
  8E9U8107 8E9U8109 8E9U8112

Kwaheri na karibu tena Tanzania Rais Barack Obama.
8E9U8188
Rais Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Barack Obama wa Marekani aliyeondoka leo kurudi nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku za mbili nchini hapa.
Akiwa Uwanja wa Ndege, Obama ameagwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwetee, ambaye ndio mwenyeji wake na kuacha ardhi ya Tanzania iliyomlaki kwa furaha za aina yake.

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal aiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Umoja wa Afrika

IMG_9822
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal pichani, ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Umoja wa Afrika unaojadili namna ya kumaliza Baa la Njaa katika nchi za Afrika. Mkutano huo wa siku moja umefanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia Jumatatu Julai Mosi, 2013 ambapo nchi washiriki wamekumbusha kuhusu Azimio la Maputo walilolitoa miaka 10 iliyopita yaani mwaka 2003, azimio lililolenga kukabiliana na Njaa na Utapiamlo.

Monday, July 01, 2013

Wakati Rais Barack Obama akiingia leo Tanzania, fahamu kidogo alipotokea kabla ya kupata mafanikio ya kuongoza Taifa la Marekani

WAKATI Rais wa Marekani, Barack Obama anawasili leo akitokea nchini Afrika Kusini katika ziara yake ya nchi tatu za Afrika ikiwamo Senegal, Afrika Kusini na Tanzania akiingia leo mchana, rais huyo amekula msoto kabla ya kufikia mafanikio yake.
Rais Barack Obama wakati huu.
Wachache wanaweza kusema rais huyo amepata raha kuanzia mwanzo hadi leo anaishi akiwa na mafanikio makubwa, hususan ya kuongoza Taifa kubwa la Marekani.

Obama anasema,  " Wakati tukiendelea na masomo yetu ya Sheria mimi na Michelle tulifanya kazi katika kampuni ya Uwakili ya Sidley na Austin jijini Chicago.
 
Binafsi nilikuwa na wasi wasi kuhusu ujana wangu na hasa changamoto kuwa maisha ya sasa ni fedha. Hofu yangu ilikuwa ni lini nitaanza kukamata fedha nyingi ili zisaidie mawazo na fikra zangu kufikia mahala ninapotaka.

Obama enzi hizo.
Lakini, kutokana na kupanda kwa gharama na mkopo niliyochukua Serikalini kwa ajili ya masomo, niliamua kuendelea kuwatumikia mabwana wawili; chuo na kampuni ya sheria.

Nilijitahidi kadiri nilivyoweza kundunduliza sehemu ya kipato changu . Hatimaye nilifanikiwa kuwa na chumba. Nilinunua suti zangu tatu na pia jozi moja ya viatu.

Hata hivyo, wakati nanunua viatu sikuwa makini, kwani vilionekana vidogo; vilivyonibana na kunifanya nionekane mshamba. Siku niliyopiga ripoti ofisini, kila mmoja aliniangalia.
Ingawa sikujua ni kwa nini, lakini nilihisi walifanya hivyo kutokana na viatu vyangu!"- Barack Obama.

SIWEZI KUVUMILIA: Kwa Simba hii haiwezi kumheshimu Juma Kaseja

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KATIKA mfululizo wa makala zangu, niliwahi kuelezea kasumba wanazokutana nazo wasemaji wa klabu za Tanzania, hasa za Simba na Yanga.
 Juma Kaseja akichupa kuudaka mpira katika moja ya mechi za mpira wa miguu Tanzania.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
Msemaji wa Simba alikuwa ni Ezekiel Kamwaga na yule wa Yanga akiwa ni Louis Sendeu, ambao wote wameondoka kwenye timu hizo, tena kwa matatizo makubwa.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...