https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, June 07, 2013

Mamia wamzika mume wa Khadija Kopa ambaye pia ni diwani mjini Bagamoyo, wakiwapo wasanii, viongozi wa chama na serikali



Na Kambi Mbwana, Bagamoyo
MUME wa mwimbaji wa muziki wa taarabu hapa nchini, Khaidija Kopa, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Magomeni, Jafari Ally, ameszikwa jana katika makaburi yaliyopo mjini Bagamoyo.

 ''Pole mwaya''. Ndivyo anavyoonekana kusema Karima Chichi Mhandeni wa tatu kutoka kulia, akimfariji Khadija Kopa, katika msiba wa mume wake aliyezikwa leo Bagamoyo.
 Waombolezaji wakiwa katika msiba wa mume wa Khadija Kopa, leo mjini Bagamoyo.
Jeneza la Jafary Ally likiswaliwa mbele ya nyumba yake mjini Bagamoyo leo. Wa nne kutoka kulia ni mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Ridhiwan Kikwete, akiungana na waislamu wenzake kuuswalia mwili wa Diwani wa Kata ya Magomeni, mjini Bagamoyo.
 Safari ya kuelekea makaburini ikaanza. Aliyebeba mwenye fulana ya mistari ni Yusuphed Mhandeni, Mchumi wa Kata ya Makumbusho CCM, jijini Dar es Salaam.

Mazishi yake yalidhuhuriwa na watu wengi, wakiwamo viongozi wa vyama vya siuasa, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Serikali pamoja na wasanii wengi waliokwenda kumpa pole Kopa.

Diwani wa CCM na mume wa Khadija Kopa kuzikwa leo saa tisa mjini Bagamoyo



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KADA wa Chama Cha Mapinduzi na Diwani wa Kata ya Magomeni, Bagamoyo mkoani Pwani ambaye pia ni mume wa Khadija Kopa, Jafary Ally anazikwa leo saa tisa mjini Bagamoyo.


Khadija Kopa akimlilia mumewe jana.
Kwa sasa msiba upo kwa wazazi wake Tandale, lakini muda mchache ujao watu wataanza kuelekea Bagamoyo kwa ajili ya mazishi. Jana kulikuwa na mvutano, baada ya baadhi ya watu, wakiwamo viongozi wa CCM kutaka Ally akazikwe Bagamoyo.

Taarifa zaidi ya mazishi ya mume wa Kopa zitaendelea kukujia katika blog yako ya Handeni Kwetu.

Hali ilivyokuwa mazishi ya Albert Mangweha mkoani Morogoro na kuacha picha ya huzuni kwa mashabiki wake



Na Kambi Mbwana, Morogoro
MKOA wa Morogoro, ukiwa chini ya Mkuu wake wa Mkoa, Joel Bendera, jana ulizizima kutokana na kuwapo kwa mazishi ya msanii nguli wa Hip Hop, Albert Mangweha (Ngwair), aliyozikwa katika makaburi ya Kihonda Kanisani, mkoani hapa.
 Afande Sele akizungumza jambo.
Sugu akizungumza na wasanii alipofika kuaga mwili wa Ngwair, Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Tukio la kuzikwa lilitanguliwa na shughuli ya uagaji iliyofanyika pia katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, baada ya kuona mkanyagano wa watu wengi nyumbani, usiku wa Jumatano, ambapo taarifa za kuwasili kwa mwili 
Kamati ya Mazishi, ikiwa chini ya wajumbe wake, akiwamo Adam Juma, ilikubaliana haraka kuwa wapenzi wa muziki nchini wapate fursa ya kuaga katika Uwanja wa Jamhuri na sio nyumbani kwao kutokana na ufinyu wa eneo hilo.
Huyu jamaa alilia sana katika kaburi la Ngwair, akiomboleza mengi, kama vile Ngwair wewe ulisababisha mimi nifeli shule ya Sekondari Mazengo, leo unaniacha peke yangu.
Mwanadada Wema Sepetu, akitafakari jambo katika kuagwa kwa msanii Ngwair.

Mji wa Morogoro ulianza kuzizima tangu asubuhi, baada ya kushuhudia vikundi vya watu wengi vikielekea uwanja wa Jamhuri, sambamba na magari mengi, pikipiki maarufu kama Bodaboda pamoja na baiskeli zilizoenda au kurudi.

Wasanii na viongozi mbalimbali, akiwamo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu nao walikuwapo katika tukio la kuaga mwili wa marehemu Ngwair na baadaye kwenye mazishi yake ambayo yalizua mkanyagano wa aina yake.

Thursday, June 06, 2013

Ngwair autikisa mji wa Morogoro kutokana na maelfu kujipanga barabarani, kujaa makaburini na wale waliokwenda kumuaga Uwanja wa Jamhuri



Na Kambi Mbwana, Morogoro
MAELFU ya watu walijazana leo katika Mkoa huu wa Morogoro kwa ajili ya mazishi ya msanii Albert Mangweha Ngwair, huku aliyepata naye matatizo nchini Afrika Kusini, Mgaza Pembe M to The P naye akiwa miongoni mwa waliohudhuria mazishi ya Ngwair.
 Hapa jeneza la Ngwair linaingizwa karubini, ikiwa ni picha inayoonyesha kuwa hatutaweza tena kukutana na msanii huyu hapa chini ya jua. R.I.P Ngwair.....
 Hapa M to The P akilia baada ya kupita kwenye jeneza la Ngwair katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika Kihonda Kanisani jioni yake.
 Mama wa Ngwair akizungumza na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Joel Bendera, leo mjini Morogoro, kabla ya mazishi ya msanii huyo wa Hip Hop Tanzania
 Mwili wa Ngwair unaingizwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Gwiji wa muziki wa taarabu Khadija Kopa afiwa na mume wake

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HABARI ambazo hazijathibitishwa rasmi zinasema kuwa mume wa mwimbaji mahiri wa taarabu, akiwa ndani ya kundi zima la TOT, Khadija Kopa, Jaffari Ally amefariki Dunia, katika Hospitali ya Lugalo.

Habari ambazo hazijathibitishwa na ndugu wa marehemu, akiwamo mke wake Khadija Kopa, zinasema kuwa marehemu Ally alipelekwa Hospitalini hapo siku ya Jumatatau kwa ajili ya kupata matibabu.

Taarifa za msiba huu zinaendelea kufuatiliwa na kuandikwa kwa urefu zaidi.


Diamond auvuruga msiba wa Albert Mangwea, mwili wake kuzikwa leo hapa mkoani Morogoro, mashabiki wake kila mmoja anasema lake



Na Kambi Mbwana, Morogoro
WAKATI mwili wa Albert Mangwea ukitarajiwa kuzikwa leo hapa mkoani Morogoro, jana katika kuaga viwanja vya Leaders Club, mashabiki wa muziki wa kizazi kipya, walitoa kali baada ya kuacha msiba wa msanii Ngwair na kuanza kumkimbilia nyota mwingine wa muziki huo, Nassib Abdulmalilck, maarufu kama Diamond.
 Ngwair enzi za uhai wake
 Ngwair alivyoletwa juzi
Ngwair alivyoagwa jana.
Hiyo ilitokea jana katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, kulipofanyika tukio la kumuaga msanii Mangwea, aliyefariki nchini Afrika Kusini Jumanne ya wiki iliyopita na kuzua huzuni kubwa katika tasnia hiyo.

Mwili wa Mangwea uliwasili viwanjani hapo saa 2:00 ukitokea Hospitali ya Taifa, Muhimbili, alipohifadhiwa juzi, mara baada ya kuletwa ukitokea nchini Afrika Kusini alipofia.

Hali ya utata katika shughuli hiyo ilianza kuonekana tangu mapema, baada ya wadau na mashabiki kuanza kuzengea katika sehemu waliyokaa wasanii, ikionyesha kuwa walikuwa na shauku ya kuwashika wasanii waliokuwapo uwanjani hapo kwa ajili ya kumuaga mwenzao.

Wednesday, June 05, 2013

Mamia wamuaga Ngwea Leaders Club, wasanii wajazana, mwili wake wasafirishwa Morogoro, kuzikwa kesho



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Marehemu Albert Mangwea ameagwa leo katika Viwanja vya Leaders Club na kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yake yaliyopangwa kufanyika kesho katika Makaburi ya Kihonda.
 Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba kushoto akijadiliana jambo na viongozi wa Kamati ya Mazishi katika shughuli yaa kumuaga marehemu Albert Mangwea, katika viwanja vya Leaders Club leo.

Wasanii wanaaga sasa.

Tuesday, June 04, 2013

Watu washindwa kuzuia vilio vyao katika mapokezi ya Ngwea Uwanja wa Ndege



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WATU wengi walijitokeza leo katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere kuupokea mwili wa marehemu Albert Mangwea, aliyefariki nchini Afrika Kusini, Jumanne ya wiki iliyopita.
Wadau wakijiandaa kuupokea mwili wa Ngwea Uwanja wa Ndege, huku kila mmoja akiwa haamini kinachotokea, huku Polisi nao wakiwa tayari kulinda usalama.
           Msanii Keisha akiwa haamini macho yake.
                           Kalale pema peponi Kamanda Ngwea
 Jeneza la Ngwea likibebwa tayari kupakiwa kwenye gari la kuelekea Hospitali ya Taifa, Muhimbili

Pitia kwa undani rasimu ya Katiba iliyotangazwa na Jaji Joseph Warioba



TAARIFA
_______

Toleo la Rasimu ya Katiba limechapishwa kwenye Gazeti la Serikali kwa
mujibu wa kifungu cha 18(5) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya
83, kwa madhumuni ya kuwepo kwa wananchi kusoma na kutoa maoni zaidi
kwa Tume kuhusu maudhui yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba.
Dar es Salaam, JOSEPH S. WARIOBA,
3 Juni, 2013 Mwenyekiti wa Tume

ii
RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA YA MWAKA 2013

________
YALIYOMO
______

Ibara Kichwa cha Habari

UTANGULIZI

SURA YA KWANZA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEHEMU YA KWANZA
MIPAKA, ALAMA, LUGHA, UTAMADUNI NA TUNU ZA TAIFA
1. Jamhuri ya Muungano
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano
3. Alama na Siku Kuu za Taifa
4. Lugha ya Taifa na lugha za alama
5. Tunu za Taifa

SEHEMU YA PILI
MAMLAKA YA WANANCHI, UTII NA HIFADHI YA KATIBA
6. Mamlaka ya wananchi
7. Watu na Serikali
8. Mamlaka na utii wa Katiba
9. Hifadhi ya Katiba

Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge ' ajifua kwa pambano lake dhidi ya Bahati Mafyela

Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge akiwa katika pozisheni
Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge akifanya mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake

Sipati picha wabongo wataupokeaje mwili wa marehemu Mangwea utakapowasili leo Tanzania kwa ajili ya mazishi yake mkoani Morogoro

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWILI wa marehemu Albert Mangwea, unawasili leo ukitokea nchini Afrika Kusini, Shirikisho la Muziki Tanzania, likitangaza kuwa kila kitu kinakwenda vizuri kwa ajili ya kuuhifadhi kwenye nyumba ya milele.

Mwili wa Ngwea ukiwa tayari kwa kuagwa jana Afrika Kusini

Jeneza la NgweaNgwea alifariki nchini Afrika Kusini Jumanne ya wiki iliyopita na kalenda ya uletwaji wa mwili huo kuanza, hivyo kusababisha ucheleweshwaji wa maziko yake.

                             Marehemu Ngwea enzi za uhai wake.
Mangwea akiletwa leo jioni, basi kesho Jumatano ataagwa katika viwanja vya Leaders Club, wakati saa sita mchana safari ya kuelekea mkoani Morogoro itaanza, huku mazishi yake yakipangwa kufanyika kesho au siku ya Alhamisi.

Monday, June 03, 2013

Ukimya watawala msiba wa Mangwea, mwili wake wadaiwa kufika kesho, wadau wajiuliza maswali 'Kimyakimya'



Na Rahimu Kambi, Dar es Salaam
HALI ya usiri umeendelea kutawala juu ya kifo cha msanii Albert Mangwea na kuanza kuzusha maswali kedekede kutoka kwa wadau wa muziki hapa nchini.
Pamoja na usiri huo kutawala, Kamati ya Mazishi na Shirikisho la Muziki Tanzania, limendelea kuwataka Watanzania kuwa na subira juu ya msiba wa msanii huyo, ambaye sasa mwili wake utafika kesho jioni.
Msemaji wa Kamati ya Mazishi, Adam Juma kushoto, akizungumza jambo akiwa na Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba kulia.

Rais wa Shirikisho hilo, Addo Novemba, aliwahakikishia Watanzania kuwa mwili huo utafika kesho na kuwapa fursa wapenzi wake kuaga siku ya Jumatano, ambapo pia utaelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yake Alhamis, makaburi yaliyopo Kihonda.

Wanakera na usajili wao wa magazetini



SIWEZI KUVUMILIA
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI wazi sasa kila kinachosemwa kwa timu ya Simba na Yanga, basi ni usajili wao, baada ya ligi kumalizika na Yanga kufanikiwa kunyakua Ubingwa kutoka mikononi mwa mtani wao wa jadi.

Picha zikionyesha vikosi vya Simba na Yanga
Baada ya kumalizika ligi hiyo ambayo kwa upande wa Simba kulikuwa na machungu ya aina yake, sasa macho na masikio ya wadau wa soka Tanzania wanaangalia kwenye usajili.

Usajili ambao endapo unatumiwa vyema, basi wachezaji wanaoweza kupatikana ni wale wenye uwezo wa juu na kuzisaidia timu zao na sio wale ambao hata thamani ya mishahara yao haitafanana.

Hapa ndipo ninaposhindwa kuvumilia. Kweli siwezi kuvumilia, maana timu zetu za Tanzania, hasa hizi za Simba na Yanga, mara nyingi usajili wao ni kanyaga twende.

Siasa mkoani Tabora zapamba moto, kada wa CCM akanusha kutuma watu wamzomee mbunge Aden Rage



Na Mwandishi Wetu, Tabora
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tabora na mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wilaya, Emmanuel Mwakasaka, pichani juu, amekanusha vikali tuhuma za baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM kuwa aliwapa vijana fedha ili wamzomee mbunge wa jimbo la Tabora mjini, Ismail Aden Rage.

Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage
Mapema siku ya jumamosi ya mwezi mei 25 mwaka huu,chama cha
mapinduzi,(CCM),mkoa wa Tabora walifanya mkutano wa hadhara kwenye
viwanja vya stendi ya mabasi zamani ambapo kuliibuka zomea zomea toka
kwa wananchi.

Aidha wananchi hao walipokuwa wakizomea walisikika wakitamka kuwa
wamechoka na propaganda wanachotaka ni barabara za
lami,Tabora-Nzega,Tabora-Urambo na ile ya Itigi-Tabora.

Sunday, June 02, 2013

Danadana ya msiba wa Ngwea wazua taharuki, sasa mwili wake kuletwa Jumatatu au Jumanne



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HALI ya utata imeonekana kugusa hisia za watu wengi kutokana na kifo cha msanii Albert Mangwea, huku ripoti yake ikifanywa siri, hivyo kushindwa kuurudisha mwili wa marehemu nchini Tanzania kwa ajili ya mazishi yake.
Marehemu Ngwea, enzi za uhai wake
Kwa siku tatu sasa, mazishi ya Ngwea yamekuwa yakisogezwa mbele kwa madai kuwa ripoti yake haijamilika. Awali, mwili wa Ngwea ulitarajiwa kufika Tanzania Alhamis, lakini danadana ilianza hadi sasa kutarajiwa kuletwa mwili wake siku ya Jumatatu au Jumanne.

Kama hivyo ndivyo, mwili wa Ngwea una dalili za wazi kuzikwa Alhamis, hasa kama utaratibu wa kuagwa katika Viwanja vya Leaders Club utabaki kama ulivyopangwa.

Green Stone wajiandaa na uzinduzi wa tawi lao baadaye mwaka huu


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TAWI la Yanga la Green Stone lenye maskani yake Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, linajipanga kufanya uzinduzi rasmi wa tawi lao baadaye mwaka huu.
Yusuphed Mhandeni, waliosimama wa tatu kutoka kushoto mstari wa nyumba.

Tawi hilo limepatiwa usajili rasmi kutoka Makao Makuu ya klabu yao ya Yanga, huku likishirikisha watu mbalimbali, akiwamo mwimbaji wa muziki wa taarabu nchini, Khadija Kopa.

Saturday, June 01, 2013

Bajaj mpya yenye ubora zaidi yazinduliwa jijini Dar es Salaam leo


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Shinyanga Emporium (1978), leo imezindua Bajaj mpya aina ya Piaggio ambayo haitumii mafuta mengi, hivyo kuwa mkombozi kwa wananchi wote, wakiwamo wafanyabiashara wa Bajaj.
 Nishit Peter, Meneja wa Tawi lililopo karibu na Mlimani City, akitoa maelekezo kwa wateja wake waliotembelea kwenye  uzinduzi wa bajaj aina ya Piaggio, leo jijini Dar es Salaam.

Sudan yaitia hofu Tanzania kupeleka timu zake kushiriki michuano ya Kagame



Na Mwandishi Wetu, Dodoma
SERIKALI imesema italiangalia upya suala la vilabu vya soka vya Tanzania vya Simba, Yanga na Falcon kwenda nchini Sudan kushiriki katika michuano ya Kombe la Kagame ambayo inaandaliwa na Baraza la Michezo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA. 
Bernad Membe, Waziri wa Mambo ya Nje

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernand Membe kuulizwa juu ya usalama wa timu hizo zitakapokwenda jijini Darfur ambako michuano hiyo imeandaliwa. 

Mwili wa Magwea wazuiwa Afrika Kusini, sasa kuwasili kesho Jumapili, huku Baraza la Sanaa Taifa likimlilia nyota huyo na wadau wakijipinda kwa michango



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWILI wa msanii Albert Mangwea, umezuiwa na Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini wakiwa na lengo la kushiriki kumuaga, hivyo kulazimisha kupanguliwa kumleta nchini kesho (leo) na badala yake marehemu atawasili kesho Jumapili.
                   Marehemu Ngwea, enzi za uhai wake
Aidha, wadau mbalimbali wameendelea kushiriki kuchangia msiba wa marehemu Ngwea, wakiwamo Kampuni ya Clouds Media Group, sambamba na Studio za Bongo Records chini ya P-Funk Majani na Push Mobile ambao wote kwa pamoja wamechangia Milioni tano kila mmoja.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba, alisema kuwa wamepata taarifa kutoka Afrika Kusini kuwa mwili huo sasa utawasili kesho Jumapili ya Juni mbili badala ya Jumamosi ya Juni Mosi kama ilivyotangazwa awali.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...