Msimu mkubwa zaidi wa shamrashamra za kitamaduni katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma sasa upo tayari kurindima kwa mziki wa kusisimua, ofa murwa na mabadikilo makubwa ya kidigitali nchini kote.
Hii inafuatia uzinduzi mkubwa wa makubaliano kati ya Tigo Tanzania – kampuni inayoongoza katika mabadiliko ya kidigitali nchini na Clouds Entertainment Group. Makubaliano haya yanayoipa Tigo haki miliki za jina Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma yatawezesha mzimu huu wa utamaduni ukifikia mikoa 15 nchini.
Wakitangaza makubaliano hayo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugrenzi wa Masoko wa Tigo, William Mpinga aliahidi kuwa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma litakuwa tamasha kubwa na la kusisimua zaidi katika historia ya miaka 16 ya tamasha hilo la kitamaduni katika ukanda huu wa Afrika.
‘Kauli mbiu ya Tigo Fiesta 2017 ni Tumekusoma, ikionesha sifa kuu ya Tigo kama mtandao unaoelewa zaidi mahitaji ya wateja wake nchini kote,’ Mpinga alisema.
‘Ushirikiano huu unamaanisha kuwa pamoja na kuwa mtandao unaoongza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo sasa pia ndio mtandao unaosisimua zaidi nchini. Tutawaletea wasanii wenye hadhi ya kimataifa na waliojizolea sifa ndani na nje ya nchi katika msimu wa miezi mitatu iliyojaa ofa kabambe kutoka Tigo zitakazoendana na shamrashamra za furaha na kumbukumbu za muziki murwa.
‘Kupitia Tigo Fiesta 2017- Tumekusoma, Tigo imejikita kuinua vipaji vya wasanii wa Kitanzania kama njia mojawapo ya kukuza sanaa nchini. Kama tunavyojua, sanaa imekuwa mojawapo ya nafasi kubwa za ajira kwa vijana wetu na baaadhi ya wasanii wetu pia wamepata nafasi ya kuperusha bendera ya nchi katika nchi za kigeni, kwa hiyo kusaidia kuitangaza nchi yetu. Tuna imani kuwa kupitia ushirikiano huu tutaweza kuwakutanisha wasanii wetu na mashabiki wao, kuwajengea uwezo na hivyo kuwasaidia wasanii wengi zaidi kufikia viwango vya kimataifa,’ alisema.
Kwa upande wake, Mratibu Mkuu wa Kamati ya Maandilizi ya Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma, Sebastian Maganga alisema kuwa msimu huu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma utajumuisha mikoa ya Arusha Kahama, Musoma, Mwanza, Tabora na Dodoma. Mikoa mingine itakayohusishwa ni Iringa, Songea na Njombe pamoja na Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Moshi na Mtwara .
‘Kama ilivyokuwa kawaida yetu, hatma ya Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma itafanyika Dar es Salaam,’ Sebastian alisema, huku akibainisha kuwa tarehe za tamasha, maeneo husika pamoja na wasanii na matukio yataoendana na msimu huu yatatangazwa hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment