Pages

Pages

Tuesday, May 30, 2017

Waandishi wa Kilimo wakutana jijini Mwanza

 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo Tanzania (TAJF), Gerald Kitabu (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wanachama wa TAJF wakati wa kikao kilichofanyika Ufukwe wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza jana kujadili masuala mbalimbali ya chama hicho.

Mshindi wa Milioni za Biko Arusha apokea fedha zake



Mkurugenzi Mtendaji wa Biko Tanzania Charles Mgeta mwenye miwani akishuhudia katika makabidhiano ya Sh Milioni 10 kwa mshindi wao wa jijini Arusha Leopard Mpande aliyepatikana katika droo ya Jumapili iliyopita. Aliyeshikana mikono na Mpande ni Balozi wa Biko Kajala Masanja.

Na Mwandishi Wetu, Arusha
WAENDESHAJI wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, jana wamemkabidhi zawadi yake jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wao wa jijini Arusha, Leopard Mpande, aliyetangazwa mshindi katika droo ya tisa iliyofanyika Jumapili, jijini Dar  es Salaam.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta, alisema Mpenda ni mshindi akitokea jijini Arusha, baada ya kuamua kucheza bahati nasibu ya Biko.
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko jijini Arusha, Leopard Mpande wa tatu kutoka kushoto akipokea nyaraka na fedha zake baada ya kukabidhiwa kutokana na ushindi wa droo ya nane ya Biko iliyochezeshwa Jumapili. Wengine wanaoshuhudia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja, Msanii Mpoki na maofisa wa NMB jijini Arusha. 

Alisema wanajisikia faraja kubwa kuona watu wanaingia kwa wingi kucheza mchezo wao wa kubahatisha na kuzoa mamilioni ambapo zaidi ya Watanzania 35,000 wameshinda zawadi mbalimbali.


Mgeta anasema hadi sasa wameshafanya droo kubwa tisa huku washindi wote wakiwa wameshakabidhiwa fedha zao hivyo kufanya jumla ya Sh Milioni 90 kuwafikia washindi wa droo kubwa za Sh Milioni 10.

Sunday, May 28, 2017

Maonyesho ya tano ya Kimataifa ya Biashara yafanyika jijini Tanga


Meneja Mkuu Idara ya Masoko Kiwanda cha Saruji cha  Rhino Tanga, William Malonza, akimuonyesha moja ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho, Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, wakati wa maonyesho ya tano ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako Tanga.

Mwijage ameyafungua maonyesho hayo leo katika viwanja ya maonyesho Mwahako ambayo yamezishirikisha mataifa mbalimbali ya Barani Afrika na Asia.

Tanzania yatumia Siku ya Afrika Saudi Arabia kutangaza utamaduni wake

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akifurahia chakula cha asili ya Tanzania na mabalozi wa nchini nyingine katika maadhimisho ya Siku ya Afrika nchini hapa yaliyofanyika hivi karibuni.

Na Mwandishi Wetu, Riyadh
Balozi wa Tanzania UBALOZI wa Tanzania nchini Saudi Arabia, uliungana na ofisi nyingine za balozi za nchi mbalimbali kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Afrika yaliyofanyika hivi karibuni nchini Saudi Arabia.


Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na kutangaza utamaduni, ambapo kwa Tanzania, shamra shamra hizo zilikonga nyoyo za wahudhuriaji wengi, ambapo wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini hapa waliimba nyimbo za kuisifu na kuipamba Tanzania.
Wanafunzi wa kitanzania baada ya kutumbuiza nyimbo za kuisifu Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliuambia Mtandao huu kuwa kusudio la kuungana na mabalozi wengine lilifanikiwa kwa sababu lengo halisi ni kuitangaza Afrika na nchi zao, ambapo anaamini kwa maadhimisho hayo nchi yake imepiga hatua kujitangaza kwa kuonyesha utamaduni wao kwa kupitia, ngoma, nyimbo, ngojera, maonesho ya mavazi na maonesho ya vyakula vya asili vya nchi zilizoshiriki,
Wakati wa Maakuli. Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akiwa ameshika sahani ya chakula katika maadhimisho ya Siku ya Afrika ambapo vyakula vya asili, ngoma na utamaduni wa Tanzania ulionyeshwa katika tukio hilo.

Biko kutoa Milioni 20 jumatano hii, mwingine aibuka na 10M Arusha


Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja kulia akizungumza jambo wakati wa kuchezesha droo ya tisa ambapo mkazi wa Arusha, Leopard Mpande aliibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi hivyo atajinyakulia Sh Milioni 10 kutoka Biko. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAHATI Nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku, sasa imezidi kuchanja mbuga baada ya kuongeza donge nono la washindi wa droo zao kubwa, ambapo sasa mshindi wa droo ya Jumatano hii anatarajiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 20.

Mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa, tayari imempata mshindi wake wa droo ya tisa ya Jumapili ambaye ni Leopard Mpande wa jijini Arusha, aliyenyakua Sh Milioni 10 huku pia Biko ikiwa imeshapata washindi zaidi ya 35,000 wa papo kwa hapo.
Kajala Masanja akizungumza na Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.

Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo kushoto akiandika dondoo za mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko aliyetangazwa leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Arusha, Leopard Mpande aliibuka kidedea katika droo hiyo.


Akizungumza leo katika droo iliyompata Mpande, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema kwamba wameamua kuongeza zawadi ya droo kubwa ya jumatano hii kutoka Sh Milioni 10 hadi 20 ili kuwawesha washiriki nafasi ya kujikwamua kimaisha kwa zawadi za BIKO, "Changamkieni fursa hii" alisema.
  
Alisema droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 itafanyika Jumatano, huku akiwataka watu wacheze mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za MPESA, TIGOPESA na AIRTEL Money kwa kuingia kwenye kipengele cha lipa bili au lipa kwa MPESA ambapo watatakiwa waingize namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kuweka pia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456.

Friday, May 26, 2017

Mwakaboko: Milioni 10 za Biko zinanikomboa kiuchumi


Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wa droo ya nane ya Biko, Daniel Dancan Mwakaboko aliyetangwa Jumatano ambapo jana alikabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kushoto ni afisa wa NMB aliyesimamia zoezi la kuingiza fedha hizo katika akaunti ya mshindi huyo wa Milioni 10 na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko Grace Kaijage.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MSHINDI wa droo ya nane ya Bahati Nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Daniel Mwakaboko, jana amepokea fedha zake jumla ya Sh Milioni 10, huku akisema kuwa zawadi aliyoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko itamkomboa kiuchumi na kumuondoa kwenye hatari ya umasikini inayowakumba vijana wengi.


Akizungumza jana katika makabidhiano ya fedha zake, Mwakaboko alisema kwamba zawadi ya fedha taslimu Sh Milioni 10 ni nyingi kwa wakati huu anaposaka maisha bora kwa kutafuta mtaji mara kadhaa bila mafanikio.
Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wa droo ya nane ya Biko, Daniel Dancan Mwakaboko aliyetangwa Jumatano ambapo jana alikabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa sasa anafanya kazi ya kuchapisha majarida na vitu tofauti tofauti vya kiofisi katika ofisi ya mtu mwingine, hivyo ni wakati wake wa kuangalia namna gani atazitumia vizuri fedha za ushindi alizokabidhiwa baada ya kuibuka na ushindi kartika droo ya nane ya Biko iliyochezeshwa Jumatano.


“Biko ni mchezo mzuri usiochosha na unaoweza kumpa kila mmoja wake ushindi kwa sababu hata uchezaji wake wa kuweka muamala kwa simu za Tigo Pesa, MPESA na Airtel Money kwa kuanzia Sh 1000 na kuendelea ni rahisi maana unachotakiwa ni kuingiza namba ya kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 tayari kusubiri zawadi ya papo kwa hapo au droo kubwa ya Sh Milioni 10.

Wednesday, May 24, 2017

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akizungumza na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) pamoja na wanahabari walipofika ofisini kwake wakiwa katika ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani wa mkoa huo leo.
Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon akitoa maelezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba kabla ya kuanza ziara ya mafunzo hayo.

Mkazi Tabata Daniel Mwakaboko aibuka na mkwanja wa Biko

Picha tofauti tofauti Balozi wa Biko Kajala Masanja akimkaribisha mgeni wake mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe katika droo ya nane ya Sh Milioni inayoondeshwa na Biko Tanzania ambapo mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Daniel Dancan Mwakaboko alifanikiwa kutangazwa mshindi katika droo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha wetu. 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya nane iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam na waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ imefanyika huku mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Daniel Dancan Mwakaboko akifanikiwa kuibuka na mkwanja wa Sh Milioni 10. 
 
Hiyo ni siku chache baada ya wakazi wa Ubungo, Sospeter Muchunguzi na Stanley Kapondo, mfanyakazi wa TANESCO nao kuibuka na mamilioni ya Biko kwa siku tofauti ndani ya wiki moja.


Akizungumza katika droo hiyo, Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema kwamba siri kubwa ya ushindi ni kucheza Biko mara nyingi zaidi, akiamini kuwa kila anayecheza ana nafasi kubwa ya kuibuka kidedea na ushindi huo.

Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe kushoto akiwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja wakati wanamtafuta mshindi wa droo ya nane wa Biko ambaye mkazi wa Tabata, Daniel Mwakaboko alitangazwa mshindi na kuzoa jumla ya Sh Milioni 10 atakazokabidhiwa jijini Dar es Salaam.

Alisema mchezo wa Biko ni mzuri na rahisi kucheza kwake, hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kutumia nafasi yake vizuri kwa kucheza bahati nasibu hiyo iliyojizolea umaarufu katika kipindi kifupi baada ya kuanzishwa kwake.


“Hakuna njia ya mkato ya kuweza kushinda donge nono la Biko badala yake dawa ni kucheza kwa wingi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Kajala.


Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka Watanzania kuingia kwa wingi katika mchezo wa Biko hususan wakazi wa mikoa mbalimbali ya Tanzania nao wakiwa kwenye nafasi kubwa ya ushindi.

Tuesday, May 23, 2017

Maofisa ugani wapewa somo

 Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus (kulia), akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa hilo. 

Picha mbalimbali za Bonanza la kwaya jijini Dar es Salaam

Kikosi cha kwaya ya Usharika wa Mabibo (waliovaa jezi za Dark Blue) na kwaya ya Usharika wa Kinondoni (waliovaa jezi nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi kuanza
Mpira ukiwa unaendelea ambapo kwaya ya Kinondoni waliibuka kuwa washindi

Muchunguzi: Kuogopa kucheza Biko ni dalili ya kukaribisha umasikini

Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, kulia akimkabidhi nyaraka halali za Benki ya NMB zinazoonyesha kuingizwa kwa fedha za mshindi wao Sospeter Muchunguzi pichani kushoto jumla ya Sh Milioni 10 alizoshinda katika Bahati Nasibu yao ya Ijue Nguvu ya Buku, droo iliyochezeshwa Jumapili. Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MSHINDI wa droo ya saba ya Sh Milioni 10 kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Sospeter Muchunguzi, amekabidhiwa fedha zake huku akisema kuwa kuogopa kucheza Biko ni dalili ya kukaribisha umasikini.



Muchunguzi aliyasema hayo jana katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam wakati anakabidhiwa fedha zake na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage.



Akizungumza kwa msisitizo mkubwa, Muchunguzi mwenye ndoto za ujasiriamali alisema kwamba watu wote waliofanikiwa katika maisha yao walithubutu katika mambo waliyokusudia kuyafanya, hivyo ni budi kila mmoja kupita njia hiyo.
Sospeter Muchunguzi katikati akisaini nyaraka za benki ya NMB kwa ajili ya fedha zake kuingizwa kwenye akaunti yake katika benki hiyo jana baada ya kuibuka kidedea katika droo ya Biko ya Sh Milioni 10. Kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko Grace Kaijage na kushoto ni Afisa wa NMB.


Alisema uhakika wa kushinda ni mkubwa ikiwa mtu ameamua kweli kuingia katika sekta ya michezo ya kubahatisha, hususan mchezo wa Biko ambao hata uchezaji wake upo wazi na hakuna dalili zozote za kudanganya washindi.



“Nilipoona utaratibu wa Biko ni mzuri nikathubutu kucheza huku nikiamini kwamba endapo naweza kuibuka na ushindi naweza kusogea katika hatua moja kwenda nyingine hivyo Watanzania wenzangu hakuna haja ya kuogopa ili tusonge mbele.

Sunday, May 21, 2017

Sospeter Muchunguzi naye azoa mkwanja wa Biko

Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akizungumza jambo wakati wa kuchezesha droo ya saba ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10 ambapo bwana Sospeter Muchunguzi wa Ubungo, jijini Dar es Salaam alitangazwa mshindi.



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

DROO ya saba ya mchezo wa Kubahatisha wa Biko, Ijue Nguvu ya Buku imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam, huku Sospeter Muchunguzi akifanikiwa kuibuka kidedea na kuzoa Sh Milioni 10.



Mkazi huyo wa jiji alifanikiwa kujinyakulia zawadi hiyo ya juu ya Sh Milioni 10 kutoka Biko, katika droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa ushirikiano na Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.



Akizungumza katika droo hiyo ya saba, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba Watanzania wameendelea kupata hamasa kubwa na kujitokeza kwa wingi kuwania zawadi mbalimbali za fedha taslimu kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni 1,000,000.

 Kajala Masanja akionyesha namba ya mshindi.
“Ni furaha kwetu kuona idadi kubwa ya Watanzania inajitokeza kwa wingi kucheza Biko na kupata zawadi mbalimbali kutoka kwetu kwa kucheza bahati nasibu yetu kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1000 ambapo kwenye namba ya kampuni wataingiza 505050 na namba ya kumbukumbu ni 2456.


“Biko bado inaendelea kuchanja mbuga ambapo sasa tutakuwa tunachezesha droo kwa siku ya Jumatano na Jumapili kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kila mtu anaibuka na ushindi wa Biko na kuzoa mamilioni kutoka kwenye bahati nasibu yetu,” Alisema Heaven.



Naye Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe, aliwataka Watanzania kuendelea kuchangakia zawadi za Biko kwa kucheza kwa wingi kutokana na utaratibu mzuri na urahisi wa mchezo wa Biko.

Friday, May 19, 2017

Kapondo: Mshiko wa Biko umekuja wakati nina uhitaji mkubwa wa pesa


Mfanyakazi wa Shirika na Umeme TANESCO Stanley Kapondo, katikati akipokea fedha zake jumla ya Sh Milioni 10 alizoshinda katika bahati nasibu ya Biko katika droo ya Jumatano. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven na kushoto ni afisa wa NMB aliyesimamia uingizaji wa fedha hizo katika akaunti ya Kapondo.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MSHINDI wa Droo ya Bahati Nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku iliyochezeshwa juzi Jumatano, Stanley Kapondo, amekabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 10, huku akisema kuwa pesa hizo zimekuja wakati muafaka ili kuondoa changamoto zinazomkabili katika maisha yake.


Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam kwa kusimamiwa na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, ikiwa ni siku moja baada ya kumpata mshindi wao wa droo ya Jumatano.

Mfanyakazi wa Shirika na Umeme TANESCO Stanley Kapondo kushoto akifurahia fedha zake za ushindi wa droo ya Biko alizoshinda katika droo ya Jumatano. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kapondo alisema alikuwa na uhitaji mkubwa wa pesa, hivyo aliamua kucheza Biko kama sehemu ya kutafuta suluhu ya matatizo yake.
Alisema pamoja na kuamua kucheza Biko, hakuamini kwamba angeshinda Sh Milioni 10, badala yake alikuwa anawazia ushindi wa Sh Milioni moja aliyoona ni rahisi.

Sunday, May 14, 2017

Mbunge wa Lushoto akagua barabara ya Mombo

Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akikagua athari za mafuriko kwenye barabara ya Soni hadi Mombo ambapo imefungwa kutokana na vifusi,mawe kudondoka barabarani na hivyo kusababisha adha hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia akiangalia athari za barabara ya Mombo hadi Soni ambayo imefungwa kutokana na kushuka kwa mawe makubwa na vifusi.

James Peter wa Bunju jijini Dar es Salaam ashinda Milioni za Biko

Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja akifurahia namba ya ushindi ambapo mkazi wa Bunju, jijini Dar es Salaam, James Peter amejinyakulia jumla ya Sh Milioni 10 katika droo iliyochezeshwa leo  jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Emmanuel Ndaki. Picha na Mpiga picha wetu. 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKAZI wa Bunju jijini Dar es Salaam, James Peter amefanikiwa kuibuka kidedea katika droo ya tano ya wiki ya kuwania Sh Milioni 10 baada ya kutangazwa mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho.
Droo hiyo ya tano ya wiki imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Emmanuel Ndaki. Akizungumza katika droo hiyo ya tano, Kajala Masanja alisema mshindi wa Milioni 10 wa wiki hii alibahatika kutangazwa mshindi baada ya kupigiwa simu mara tatu, huku mara mbili akishindwa kupokea simu kwa haraka.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akiagana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Emmanuel Ndaki baada ya kumaliza kuchezesha droo ya tano ya Sh Milioni 10 ambapo mkazi wa Bunju, jijini Dar es Salaam, James Peter kutangazwa mshindi wa droo hiyo ambapo amejishindia jumla ya Sh Milioni 10.

Kajala Masanja akifurahia namba ya ushindi ya bwana James Peter
Alisema hata hivyo baadaye alipokea simu hali inayoonyesha kwamba alikuwa na bahati kubwa kwa kunyakua fedha hizo zinazotolewa kwa mshindi mmoja kila mwisho wa wiki, huku washindi wengine zaidi ya 20,000 wa zawadi za papo kwa hapo wakijishindia zawadi kem kem.
“Tumefanikiwa kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 ambaye anatokea jijini Dar es Salaam, akiongeza idadi ya washindi wanne kutokea jijini hapa, huku

Bia ya Serengeti kuidhamini Taifa Stars kwa Sh Bilioni 2.1

Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (kulia ) akipeana mkono na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) mara baada ya kukabidhiana mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 2.1,ambao ni udhamini  kwa timu ya Taifa kwa miaka mitatu .Pichani kati anaeshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

Thursday, May 11, 2017

DC Iringa afungua warsha ya siku tatu ya kujenga uelewa kwa wadau

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Meya wa Manispaa ya kinondoni Mheshimiwa Benjamini Sitta ambaye pia ni mwenyekiti wa warsha akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa

Serikali kujenga nyumba za askari magereza 9500 nchini



Na Mwandishi Wetu, MOHA
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Benki ya Exim inatarajia kujenga nyumba 9500 za askari magereza ili kukabiliana na changamoto za makazi ya askari  wa jeshi hilo hapanchini.

Naibu Waziri wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akishirikiana na Viongozi wengine kufungua Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa. Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma. Picha na Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi



Akizungumzia changamoto za makazi ya askari wa Jeshi la  Magereza Nchini, wakati wa uzinduzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alisema Serikali inatambua changamoto za makazi kwa askari magereza na tayari iko katika mazungumzo na benki ya Exim ili iweze kujenga nyumba hizo.

“Nawaomba  askari wetu nchi nzima  wawe na subira  Serikali inatambua na  inashughulikia changamoto ya makazi ya  askari na tayari tuko katika mazungumzo na wadau ikiwemo benki ya Exim kuanza mradi wa ujenzi wa nyumba takribani 9500, lengo ni kukidhi kiu ya makazi ya askari na familia zao,” alisema Masauni.

Awali akitoa maelezo ya ujenzi wa Gereza hilo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa alisema ujenzi wa Gereza hilo umefanywa na wataalamu ambao ni askari Magereza kwa  kushirikiana na wafungwa kama sehemu ya utekelezaji wa  amri ya Mh. Rais Dk. John Magufuli ya kutaka wafungwa watumike katika kazi za uzalishaji ikiwemo kilimo,ujenzi na ufundi mbalimbali.

Ujenzi wa Gereza hilo umegharimu jumla ya shilingi milioni 65 na litasaidia pia kuhifadhi wafungwa 148 na hivyo kupunguza msongamano wa wafungwa katika Gereza la Kongwa mkoani Dodoma pamoja na kuepuka usumbufu wa  ndugu wa wafungwa kusafiri mpaka wilayani Kongwa kwenda kuwaona ndugu zao.