Pages

Pages

Tuesday, May 30, 2017

Mshindi wa Milioni za Biko Arusha apokea fedha zake



Mkurugenzi Mtendaji wa Biko Tanzania Charles Mgeta mwenye miwani akishuhudia katika makabidhiano ya Sh Milioni 10 kwa mshindi wao wa jijini Arusha Leopard Mpande aliyepatikana katika droo ya Jumapili iliyopita. Aliyeshikana mikono na Mpande ni Balozi wa Biko Kajala Masanja.

Na Mwandishi Wetu, Arusha
WAENDESHAJI wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, jana wamemkabidhi zawadi yake jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wao wa jijini Arusha, Leopard Mpande, aliyetangazwa mshindi katika droo ya tisa iliyofanyika Jumapili, jijini Dar  es Salaam.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta, alisema Mpenda ni mshindi akitokea jijini Arusha, baada ya kuamua kucheza bahati nasibu ya Biko.
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko jijini Arusha, Leopard Mpande wa tatu kutoka kushoto akipokea nyaraka na fedha zake baada ya kukabidhiwa kutokana na ushindi wa droo ya nane ya Biko iliyochezeshwa Jumapili. Wengine wanaoshuhudia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja, Msanii Mpoki na maofisa wa NMB jijini Arusha. 

Alisema wanajisikia faraja kubwa kuona watu wanaingia kwa wingi kucheza mchezo wao wa kubahatisha na kuzoa mamilioni ambapo zaidi ya Watanzania 35,000 wameshinda zawadi mbalimbali.


Mgeta anasema hadi sasa wameshafanya droo kubwa tisa huku washindi wote wakiwa wameshakabidhiwa fedha zao hivyo kufanya jumla ya Sh Milioni 90 kuwafikia washindi wa droo kubwa za Sh Milioni 10.
 Mshindi wa Biko jijini Arusha akisikiliza ushauri wa kifedha kutoka kwa afisa wa NMB Jijini Arusha jana.


“Huku Jumatano ya kesho tukitoa Sh Milioni 20 kwa mshindi wetu wa droo kubwa, tunajivunia kuona idadi ya wanaovuna mamilioni kutoka Biko inaongezeka kwa kucheza kwa kupitia M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money ambapo jinsi ya kucheza ni kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumbukumbu namba ikiwa ni 2456.


“Mtu anaweza kucheza kuanzia Sh 1000 au zaidi huku kila tiketi moja inayopatikana kwa Sh 1000 ikiwa na nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 10, huku kwa Jumatano hii dau likipanda hadi Sh Milioni 20,” alisema Mgeta.


Mgeta aliongeza kuwa zawadi za papo kwa hapo zinazopatikana katika bahati nasibu yao ni kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja ambayo hulipwa kwa mshindi kwa kupitia simu yake aliyotumia kuchezea bahati nasibu yao.


Naye Mpande aliishukuru Biko kwa kumpa zawadi yake, akiamini kuwa kupokea kwa haraka kumemfanya aamini kuwa Biko ni waendeshaji wa bahati nasibu za kisasa na zenye uhakika mkubwa wa kushinda.

Nimepokea zawadi yangu ya Sh Milioni 10 kwa furaha kwa sababu sikuamini kabisa kama nimeshinda, lakini pia kama napokea fedha zangu kwa haraka kiasi hiki, ikiwa ni siku moja baada ya kushinda kwenye droo ya Jumapili.


“Nawaomba Watanzania wenzangu wasilaze damu, tuendelee kucheza Biko ili tuweze kuvuna mamilioni kwa sababu njia ya ushindi ni kucheza mara nyingi zaidi na tusikate tamaa, ukizingatia kuwa hata mimi sikuamini kama naweza kutangazwa mshindi,” Alisema.


Bahati Nasibu ya Biko ni moja kati ya michezo iliyoibuka kwa siku za hivi karibuni na kufanikiwa kujizolea umaarufu mkubwa kutokana na utaratibu wake wa upatikanaji wa washindi na kugawa zawadi kwa wakati jambo linalotafsiriwa kama fursa za kiuchumi kwa wachezaji wake na Watanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment