Pages

Pages

Wednesday, May 24, 2017

Mkazi Tabata Daniel Mwakaboko aibuka na mkwanja wa Biko

Picha tofauti tofauti Balozi wa Biko Kajala Masanja akimkaribisha mgeni wake mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe katika droo ya nane ya Sh Milioni inayoondeshwa na Biko Tanzania ambapo mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Daniel Dancan Mwakaboko alifanikiwa kutangazwa mshindi katika droo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha wetu. 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya nane iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam na waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ imefanyika huku mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Daniel Dancan Mwakaboko akifanikiwa kuibuka na mkwanja wa Sh Milioni 10. 
 
Hiyo ni siku chache baada ya wakazi wa Ubungo, Sospeter Muchunguzi na Stanley Kapondo, mfanyakazi wa TANESCO nao kuibuka na mamilioni ya Biko kwa siku tofauti ndani ya wiki moja.


Akizungumza katika droo hiyo, Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema kwamba siri kubwa ya ushindi ni kucheza Biko mara nyingi zaidi, akiamini kuwa kila anayecheza ana nafasi kubwa ya kuibuka kidedea na ushindi huo.

Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe kushoto akiwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja wakati wanamtafuta mshindi wa droo ya nane wa Biko ambaye mkazi wa Tabata, Daniel Mwakaboko alitangazwa mshindi na kuzoa jumla ya Sh Milioni 10 atakazokabidhiwa jijini Dar es Salaam.

Alisema mchezo wa Biko ni mzuri na rahisi kucheza kwake, hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kutumia nafasi yake vizuri kwa kucheza bahati nasibu hiyo iliyojizolea umaarufu katika kipindi kifupi baada ya kuanzishwa kwake.


“Hakuna njia ya mkato ya kuweza kushinda donge nono la Biko badala yake dawa ni kucheza kwa wingi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Kajala.


Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka Watanzania kuingia kwa wingi katika mchezo wa Biko hususan wakazi wa mikoa mbalimbali ya Tanzania nao wakiwa kwenye nafasi kubwa ya ushindi.

“Tumetoa zawadi kwa washindi zaidi ya 30,000 nchi nzima kwa zawadi kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja nchini kote, hivyo tunawaomba watu wa mikoani nao kuongeza mwendo kuwania mamilioni ya Biko yanatotoka kila siku, huku droo kubwa ya Sh Milioni 10 ikifanyika siku mbili kwa wiki, yani Jumatano na Jumapili,” Alisema Heaven. 
 
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Chiku Salehe, alisema anajisikia faraja kuwa mwangalizi katika droo iliyompa ushindi mkazi wa Tabata, Mwakaboko, akiamini kuwa kila Mtanzania anaweza kuzoa mamilioni ya Biko.


“Mchezo wa Biko ni rahisi kucheza, ni salama na tunaangalia kwa kina ili kila Mtanzania aweze kushinda kihalali na kuongeza kipato chake kama walivyokusudia, ukizingatia kuwa endapo mtu anaibuka na mamilioni ya Biko anaweza kufika mbali kiuchumi,” Alisema Chiku. 
 
Mshindi wa droo hiyo, Mwakaboko hakusita kuonyesha furaha yake kwa kutangazwa mshindi, huku akisema licha ya kuchelewa kushinda, lakini hakuvunjika moyo akiamini kuwa siku moja bahati inaweza kuwa yake.


“Nashukuru sana kwa kutangazwa mshindi wa Biko wa Sh Milioni 10, sasa nitaipata lini,” Alihoji Mwakaboko kwa kupitia simu wakati anahojiana na balozi wa Biko, Kajala.


Kwa ushindi huo, Mwakaboko anatarajiwa kukabidhiwa fedha zake mapema ili aweze kuziingiza katika matumizi yake ya kimaisha hususan ya kumkwamua kiuchumi kwa kupitia mchezo wa Biko uliojizolea umaarufu mkubwa ukitambulika kama nguvu ya Buku.

No comments:

Post a Comment