Pages

Pages

Sunday, May 14, 2017

Bia ya Serengeti kuidhamini Taifa Stars kwa Sh Bilioni 2.1

Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (kulia ) akipeana mkono na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) mara baada ya kukabidhiana mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 2.1,ambao ni udhamini  kwa timu ya Taifa kwa miaka mitatu .Pichani kati anaeshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

 Rais wa TFF, Jamal Malinzi  akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba na SBL wa kuwa mdhamini mkuu wa Taifa Stars anaefuatia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  na mwishoni Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  akifurahi jambo na Rais wa TFF Jamal Malinzi wakati wa mkutano  na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba wa kuidhamini Taifa stars


Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba wa kuidhamini Taifa stars kwa miaka mitatu ambapo SBL imetoa kiasi cha Bilion 2.1 na kuwa mdhamini mkuu wa Taifa stars .


Wadau mbali mbali wakishuhudia tukio la kusaini mkataba wa kudhamini Taifa stars 


Waandishi wa habari wakichukua matukio 


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  akiongea na mwandishi wa habari mara baada ya SBL na TFF kusaini mkataba wa kudhamini Taifa stars  kwa kipindi cha miaka mitatu kwa mkataba wa kiasi cha Bilioni 2.1 

 Kampuni /- kama mdhamini mkuu wa timu ya taifa
Dar es Salaam, Mei 12, 2017. Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) leo imeingia mkataba wa mitatu na Shirikisho la Mipira wa Miguu Tanzania (TFF)  wa thamani ya shilingi bilioni 2.1  ambao unaifanya kuwa mdhamini  mkuu wa timu ya taifa -Taifa Stars.
 Hii ni mara ya pili kwa SBL kuiunga mkono timu ya taifa baada ya kampuni hiyo kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu ilipoidhamini timu hiyo kati ya mwaka 2008 hadi 2011.
Katika makubaliano hayo ambayo yalisainiwa leo na pande hizo mbili na Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie na Rais wa TFF Jamal Malinzi, kampuni ya SBL itapata fursa ya kutanga biashara yake wakati wa mechi zote za Taifa Stars za nyumbani na ugenini.
 Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo Bi Weesie alisema uamuzi wa kampuni hiyo wa kuidhamini timu ya taifa unatokana na sera ya SBL ya kusaidia kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo.
ga mkono sekta ya michezo nchini na kubainisha kwamba  michezo sio tu inaburudisha bali pia inaunganisha mashabiki na pia ni chanzo cha kipato kwa vijana.
“SBL inaona fahari kuidhamini timu yetu ya taifa kwa mara nyingine. Tumechukua hatua hiii kwa kuwa tunaelewa mchango wa sekta michezo katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Aidha tunaamini kuwa udhamini wetu utachangia kukuza vipaji vya vijana wetu pamoja na kuleta hamasa kubwa kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya taifa,” alisema Weesie.
Kwa upande wake, Rais wa TFF aliishukuru SBL kwa kukubali kuidhamini Taifa Stars jambo ambalo alisema litasaidia katika kufanikisha maandalizi mazuri na ushiriki kikamilifu wa timu hiyo katika mashindano mbalimbali, ndani nan je ya nchi.
 “Udhamini wa SBL umekuja kwa wakati mwafaka, wakati ambapo timu yetu ya taifa ipo katika hatua za  maandalizi kwa mashindano ya kikanda na kimataifa,” alisema Malinzi.
Hafla ya kusainiwa kwa udhamini huo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe ambaye  alitoa wito kwa  kampuni zingine na watu binafsi wenye mapenzi na michezo kujitokeza na kutoa michango ya hali na mali ili kuendeleza sekta hiyo.

No comments:

Post a Comment