Mshindi wa mashindano maalum ya watoto yaliyoandaliwa na klabu ya Golf ya JWTZ ya Lugalo, Habiba Likuli akipiga mpira huku wachezaji wenzake wakimuangalia katika hekaheka za mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Luteni Selemani Semunyu)
Hayo yalisemwa na Mmoja wa Walimu wa Mchezo huo wa Klabu ya Lugalo Elias Chiundu mara baada ya mashindano ya Watoto yaliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Uwanja wa Golf wa Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waaandishi wa habari mwalimu huyo alisema yeye kama Mwalimu anafarijika kwa kuona viwango vya watoto hao vikikua na hivyo ni matarajio yake katika mwaka 2017 watafanya vyema Zaidi.
Mshindi wa pili wa mashindano maalum ya watoto yaliyoandaliwa na klabu ya Golf ya JWTZ ya Lugalo, Sophia Juma, akipiga mpira huku wachezaji wenzake wakimuangalia kwenye mashindano hayo.
Aliongeza kuwa kuna Faida kubwa kwa Wachezaji kuandaliwa wangali wadogo kwani wanakuwa na kipindi kirefu cha mafanikio iwapo wataweka jitihada sambamba na kuungwa mkono na wazazi.
Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza baada ya kucheza Viwanja 18 aliibuka Habiba Likuli baada ya kupata mikwaju ya jumla 89 kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 15 na hivyo kuibuka na Mikwaju ya Jumla 72 akifuatiwa na Sophia Juma aliyepiga Mikwaju ya Jumla 74.
Mbali na Viwanja 18 pia katika kundi la Watoto waliocheza viwanja Tisa mshindi ni Abra Bella aliyepiga mikwaju ya jumla 48 na katika viwanja vitatu mshindi ni Salehe Ramadhani aliyepiga mikwaju ya jumla 17.
Kwa upande wake mshindi wa mashindano hayo ya siku moja Habiba Likuli amesema mashindano yalikuwa mazuri licha ya changamoto ya jua kuwa kali na kuomba Wazazi kuwaruhusu watoto wao kuja kushiriki nao ili kuonyesha vipaji na kutumia muda wao vizuri. Jumla ya wachezaji 32 wameshiriki katika mashindano hayo yenye lengo la kupima ukuaji wa vipaji vyao.
No comments:
Post a Comment