Pages

Pages

Monday, December 19, 2016

Mashindano ya Mamlaka ya Bandari Tanga yafikia tamati


Kapteni wa timu ya Bandari Tanga, Abdalla Abdulla, akipokea Kombe la Ubingwa wa jumla na Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana mara baada ya kumalizika michezo hiyo iliyoshirikisha timu za Tanga, Dar Makao Makuu, Mtwara na Bandari za Maziwa.

Na Mwandishi Wetu, Tanga
Tanga, MICHEZO ya tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS GAMES) yamemalizika kwa timu ya Bandari ya Tanga kuibuka Mabingwa wa jumla.
Timu ya Bandari ya Tanga imeibuka kwa kunyakua vikombe 7 ikifuatiwa na Bandari Makao Makuu Dar es Salaam kwa kujinyakualia vikombe 7 ambapo Bandari Mtwara na Bandari za Maziwa kila mmoja kujinyakulia kikombe kimoja kimoja.

Akikabidhi vikombe na zawadi mbalimbali kwa washindi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana ,aliwapongeza washiriki hao kwa kuonyesha umahiri katika michezo mbalimbali. Alisema mbali ya umri wao kwenda juu lakini walikuwa wakionekana kama vijana ambao wanaweza kucheza timu yoyote inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.

“Nimefarijika kuwaoma wafanyakazi wenzangu umri tofauti mukicheza mpira na kushindwa kutofautisha kijana na mzee, munakimbia uwanjani kama Messi na Ronaldo” alisema Msabimana. Aliwataka wanamichezo hao ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kuwa wamoja na kuwa na mshikamano ili kuweza kuyafikia malengo waliojiwekea.
                                   

Mshindi wa bao kutoka Bandari Makao Makuu Dar es Salaam, Mwinyi Sultan, akikabidhiwa kombe na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa  Msabimana baada ya kuibuka msindi wa mchezo huo wakati wa michezo iliyofanyika Tanga kwa siku 4 viwanja mbalimbali mkoani humo.

 Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, Netboll, kurusha Tufe, kuvuta kamba na riadha wakishangilia ushindi wa jumla mara baada ya kukabidhiwa kombe lao na Kaimu  Mkurugenzi Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mussa Msabimana. Bandari Tanga imeibuka mshindi wa jumla na kunyakua vikombe 6.


 Wachezaji wa timu ya Bandari Makao Makuu Dar es Salaam wakishangilia ushindi mara baada ya kukabidhiwa vikombe vyao kwa michezo mbalimbali, Bandari Makao Makuu walinyakua vikombe 7.
Raha ya Ushindi Bandari Mkao Makuu.Dar es Salaam.
Picha zote kwa hisani ya Tanga Kumekucha Blog

No comments:

Post a Comment