Pages
▼
Pages
▼
Thursday, December 15, 2016
Kada wa CCM Emmanuel Shilatu ampongeza Dr Magufuli
CCM MPYA YA HAPA KAZI TU
Napenda kuungana na mamilioni ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kumpongeza Mwenyekiti wa chama Taifa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuja na CCM mpya yenye dira na maboresho zaidi ya kurudi kwenye misingi ya uasisi wa CCM. Ni CCM ya "Hapa Kazi Tu".
Kila mtu amefurahia kwa namna Mwenyekiti Dk. Magufuli alivyoibuka na mikakati ya Mwanachama kukifuata chama na sio mtu, kupunguza idadi ya vikao, kuja na utaratibu wa kadi za kielektroniki utakaondoa utitiri wa kadi feki, kupunguza kitendo cha mtu kumiliki cheo zaidi ya kimoja, kupunguza idadi ya wajumbe kamati kuu na wajumbe wa NEC.
Maboresho hayo yamekisogeza chama kwa wanachama jambo litakalotoa fursa kukua kwa chama kimuonekano, kivitendo, kimtazamo kutokana na chama kuwa mali ya wanachama wote.
Halikadhalika nampongeza Mwenyekiti wa CCM Dk. Magufuli kuja na uteuzi makini wa Ndugu Rodrick Mpogoro (Naibu Katibu Mkuu - Bara) Humphrey Polepole (Katibu Itikadi na uenezi), na Kanali Ngemela Lubinga ( Katibu wa NEC siasa na uhusiano wa kimataifa. Hawa wote walioteuliwa ni watu makini, weledi, sahihi kabisa waliokuja kwa wakati sahihi. Kiukweli wametosha katika nafasi zao.
Rai yangu kwa wanachama ni wakati sasa kuacha kutafuta vyeo kwa njia za kutoa rushwa, mwanachama kukifuata chama na si mtu, uwekezaji kufanywa kwa chama na si wanachama, wanachama kufanya kazi ya kukijenga chama na kuhakikisha chama kinarudi katika misingi yake iliyojengwa na waasisi wa chama chetu ambacho ni kimbilio kwa wafanyakazi na wakulima.
Kiukweli tarehe 13/12/2016 CCM ilizaliwa upya tena. Hongera sana Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli, wajumbe wa Kamati kuu, wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kuja na CCM mpya, CCM ya hapa kazi tu.
No comments:
Post a Comment