Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (katikati) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya nne ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayowawezesha wateja wake kujipatia lita 40 za mafuta kwa kila mshindi wa droo hiyo kila wiki. Kulia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini, Bakari Maggid, na kushoto ni Meneja wa Fedha wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO Tanzania, Michael Chobu.
Pages
▼
Pages
▼
Thursday, December 31, 2015
Waraghabishi wilayani Kahama wapania Kumkomboa Mwanamke
Na
Krantz Mwantepele, Kahama
Wanawake ni nguzo
muhimu sana katika uchumi wa watanzania wengi. Mwanamke ana ushawishi mkubwa na
hasa pale anapoamua kuwa chachu ya maendeleo. Na hasa anapowezeshwa kufanya
hivyo.
Katika
kufanikisha hili waraghabishi wameamua kutoa mafunzo ya uraghabishi kwa makundi
mengine ya jamii. Mojawapo ya kundi hilo ni la wanawake. Waraghbishi wapya toka
katika kijiji cha Nyandekwa, kati ya hao wapo 9 ambao ni wanawake. Mmoja
wao ni Anna Alphonce, Mwenyekiti wa kitongoji cha Busolo, katika kijiji cha
Nyandekwa. Akielezea jinsi alivyoanza uraghbishi alisema. “Mi
niliona kuna kikundi wanakaaga humu karibu kila jioni. Na kila nilipokuwa
napita jirani na hapa naona watu wamejaa, basi nikapenda namimi nijiunge nao na
hasa baada ya kujua nini wanafanya. Na hapo ndipo nilipoanza uraghbishi,”
Anna Alphonce
(katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Busolo akifafanua jambo wakati
akielezea uraghbishi anaofanya.
Akiwa
kama mwenyekiti mwanamke wa kitongoji aliweza kutumia nafasi yake kufanya
uraghbishi kwa anaowaongoza. Kwa kuwa kilikuwa ni kipindi cha kampeni za
uchaguzi mkuu, aliitisha mikutano kwenye kitongoji chake kwa lengo la kutoa
hamasa ya wananchi kujitokeza kwa wingi. Kwa nafasi yake aliweza kuyafikia
makundi ya wazee, vijana na wanawake. Ingawa kati ya hawa wanawake ndio
walikuwa washiriki wazuri.
“Msisitizo
kwenye mikutano yangu ilikuwa ni kupiga kura kwa amani. Niliwasihi Vijana wetu
wasiwe chanzo cha vurugu na badala yake wawe walinzi na kuhakikisha uchaguzi
unafanyika katika mazingira ya utulivu,” Haya
ni maelezo ya mwenyekiti huyo akielezea jinsi alivyotumia nafasi yake kwenye
kufanya hamasa ya amani. Akaongeza,
“Kwangu
mimi haya ni mafanikio kwa sababu kweli uchaguzi umefanyika kwa amani katika
kitongoji change.” Mraghabishi
mwingine ni Matrida Peter toka katika kijiji cha Nyandekwa, yeye uraghbishi
wake alifundishwa na Elizabeth Ngaljalina toka kijiji hicho hicho. Baada ya
kufundishwa yeye alichoamua kufanya uraghbishi kwa vijana wa kijiji cha
Nyandekwa pamoja na wale waliokuwa mashuleni pia.
Wednesday, December 30, 2015
Rais Dr John Magufuli atangaza orodha ya Makatibu Wakuu wapya na Manaibu wao leo jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kulia ni Makamo wa Rais Mama Samiha Suluh Hassan wakisikiliza kwa makini.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.
Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1. Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi - Ombeni Sefue
2. Katibu Mkuu Ikulu
Peter Ilomo
3. Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
Dkt. Laurian Ndumbaro
4. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)
Dkt. Deo Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu - Afya)
Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu - Elimu)
5. Ofisi ya Makamu wa Rais
Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)
Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)
6. Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)
Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)
Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)
Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu - Sera)
7. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu - Kilimo)
Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)
Dkt. Budeba (Katibu Mkuu - Uvuvi)
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu atembelea ghala la kuhifadhia dawa Makao Makuu ya MSD
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea moja ya ghala la kuhifadhia dawa iliyopo makao makuu ya MSD,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laureane Bwanakunu na watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD Prof.Idris Mtulia.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuahidi kuwa balozi wa kuhakikisha deni la serikali linalipwa ili kuiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Waziri huyo ameeleza hayo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu kueleza kuwa ukosefu wa fedha na deni la serikali ni changamoto kubwa inayoathiri utekelezaji mzuri wa majukumu ya MSD. Mbali na hilo, Waziri wa Afya amesema mbali na deni hilo, hata kiasi cha fedha kinachotengwa na serikali kwaajili ya hospitali, vituo vya afya na zahanati na kununua dawa hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala hilo lifanyiwe kazi mapema, huku akisisitiza hata kiasi hicho kidogo kinachopatikana kitumike vizuri.
Waziri Ummy akiuliza jambo kwa wafanyakazi wa bohari hiyo.
Viongozi wapya wa TAHLISO wala kiapo kulitumikia Shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu
Uongozi mpya wa
shirikisho la elimu ya vyuo vikuu nchini Tanzania TAHLISO umesema kuwa upo
tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kasi
aliyoanza nayo na kuhakikisha kuwa elimu ya Tanzania hasa elimu ya vyuo vikuu
inakuwa ya ubora unaofaa na inaheshimika nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti mpya wa TAHLISO Ndugu JUMA ALLY OMARI akila kiapo jijini Dar es salaam |
Akizungumza na
wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kuwasimika
viongozi wa shirikisho hilo wapya mwenyekiti mpya wa TAHLISO Tanzania Bw STANSLAUS
PETER amesema kuwa kwa miaka mingi elimu ya juu nchini Tanzania imekuwa haina
ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja na mitaala mibovu, ukosefu wa mokopo kwa
wanafunzi wengi jambo linalowakatisha tamaa wengi kusoma, ambapo amesema uongozi
wake umeona kasi nzuri ya serikali ya awamu ya tano na wapo tayari kushirikiana
na serikali kutatua changamoto za wanafunzi nchini.
Tuesday, December 29, 2015
KMKM na Mafunzo washindwa kutambiana Ligi Kuu Zanzibar
Mshambuliaji wa timu ya Mafunzo akijiandaa kupiga mpira huku beki wa timu ya KMKM akiwa tayari kumzuia wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1.
Beki wa Timu ya Mafunzo akiondoa mpira golini kwao.
Monday, December 28, 2015
Rais Dr John Magufuli aapisha Mawaziri na manaibu waliobaki leo Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha Prof. Jumanne Magembe kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, wakati wa hafla fupi ya kuwaapishwa Mawaziri wapya walioteuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Desemba 28, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, kuwa Waziri wa Ujenzi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapishwa Mawaziri wapya walioteuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Desemba 28, 2015. Picha zote na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, kuwa Waziri wa Ujenzi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapishwa Mawaziri wapya walioteuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Desemba 28, 2015. Picha zote na OMR
Saturday, December 26, 2015
Ridhiwani Kikwete avunja ukimya
RIDHIWANI KIKWETE AAMUA KUFUNGUKA ..
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Ndugu zangu waandishi wa habari, nimeamua kuwaita ili kuzungumza nanyi kuhusu baadhi ya mambo yaliyokuwa yanasemwa katika vyombo vya habari kuhusu mimi.
Ndugu zangu waandishi wa habari, nimeamua kuwaita ili kuzungumza nanyi kuhusu baadhi ya mambo yaliyokuwa yanasemwa katika vyombo vya habari kuhusu mimi.
Awali ya yote napenda kusema kuwa habari hizo ni UONGO mtupu, ni mambo yanayozushwa na waandishi wa habari hizo kwa nia ya kuchafua jina langu kwa sababu wanazozijua wanaoandika. UKWELI ni kwamba haya ni mambo yenye kufanywa kwa nia na dhamira mbaya dhidi yangu na hata familia yangu.
Hivi karibuni, kwa mfano, lipo gazeti moja liliandika na kutoa picha yangu na mtu mmoja waliyedai ni Mhe. Paul Makonda eti akinifunga kamba za viatu. Katika maelezo yake mwandishi akadai kuwa Mhe. Makonda alipata uteuzi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa sababu hiyo. Huu ni uongo usiokuwa na hata chembe ya ukweli. Napenda watanzania wajue kuwa hakuna wakati wowote Baba yangu alipokuwa Rais wa nchi yetu alinihusisha kwa namna yeyote ile katika uteuzi wa mtu yeyote katika Serikali. Hivyo basi kujaribu kunihusisha na uteuzi wa Mhe. Paul Makonda kuwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni ni jambo lisilokuwa na ukweli wowote.
Pili, Yule mtu anae onekana katika ile picha siyo Mhe. Paulo Makonda bali ni Bwana Deogratius Kessy anayefanya kazi katika kampuni ya ushonaji na mavazi ya Bwana Sheria Ngowi. Nilishona safari suti kwenye kampuni hiyo. Nilipokwenda kuchukua nguo yangu na nilipovaa ili kuona kama imeshonwa vizuri, Bwana Sheria Ngowi alitaka nivae viatu vya ngozi. Bahati mbaya nilikuwa nimevaa sandals hivyo akaamua kunipa viatu vya dukani kwake nivae. Wakati bwana Deogratius Kessy akinisaidia kuvaa viatu ndipo ile picha ikapigwa nampiga picha wa kampuni ya Bwana Sheria Ngowi , inashangaza na kusikitisha kuona picha hiyo inatumiwa kupotosha ukweli kwa kutoa maelezo ya uongo. Ni dhahiri kwamba mwandishi aliamua kufanya hivyo kwa maksudi mazima ya kutoa sifa mbaya kwangu na kwa Mheshimiwa Paul Makonda. Hivi ndivyo uhuru wa habari unavyostahili kutumika ?
Bondia Thomas Mashali amsambaratisha Francis Cheka kwao Morogoro Mji kasoro bahari, usipime
Bondia Thomas Mashali kushoto akioneshana umwamba na Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika Morogoro Mashali alishinda kwa point mpambambano uho wa raundi kumi. |
Bondia Lulu Kayage kushoto akimtwanga ngumi Mwanne Haji wakati wa mpambano wao wa ubingwa Lulu alishinda kwa point katika mpambano huo wa raundi kumi. |
Wednesday, December 23, 2015
Mradi wa maji wa sh Milioni 343 wazinduliwa kijiji cha Mabogini, RC Makalla ataka vyanzo vya maji vitunzwe
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makalla mwenye miwani akizindua huduma ya maji katika kijiji cha Mabogini, mkoani Kilimanjaro wenye thamani ya Sh Milioni 343.
Akizungumza katika uzinduzi huo, RC Makalla aliwataka wananchi kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji, bila kusahau upandaji wa miti ili wasiharibu vyanzo vya maji. Alisema bila hivyo hali ya maji katika maeneo hayo itakuwa ngumu, hivyo kuna kila sababu ya wananchi hao kuielewa na kuiabudu sera ya utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti katika maeneo yao. “Naomba wananchi tulinde miundo mbinu ya maji ili kuhakikisha kwamba miradi ya maji inakuwa endelevu katika maeneo yetu tunayoishi, maana
Na Mwandishi Wetu,
Kilimanjaro
ZAIDI ya wananchi 3000
wa kijiji cha Mabogini, kitongoji cha Shabaha, mkoani Kilimanjaro, watanufaika
na huduma ya maji safi na salama, baada ya kupelekewa mradi wenye thamani ya Sh
Milioni 343. Mradi huo
uliozinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, umesimamiwa na
Mamlaka ya Maji Safi Moshi (MUASA), ukiwa na lengo la kuwapatia huduma bora ya
maji wakazi katika kijiji hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla akimtwishwa ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Mabogini baada ya uzinduzi wa mradi maji katika eneo hilo. Akizungumza katika uzinduzi huo, RC Makalla aliwataka wananchi kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji, bila kusahau upandaji wa miti ili wasiharibu vyanzo vya maji. Alisema bila hivyo hali ya maji katika maeneo hayo itakuwa ngumu, hivyo kuna kila sababu ya wananchi hao kuielewa na kuiabudu sera ya utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti katika maeneo yao. “Naomba wananchi tulinde miundo mbinu ya maji ili kuhakikisha kwamba miradi ya maji inakuwa endelevu katika maeneo yetu tunayoishi, maana
KADCO yaokoa madini yenye thamani bilioni 2 kwa wiki moja tu Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro
Tuesday, December 22, 2015
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akutana na mabalozi wa Kuwait na Rwanda ofisini kwake, jijini Dar es Salaam
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza
na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al Najem, alipofika Ofisini
kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 22, 2015 kwa mazungumzo. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea
zawadi kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al Najem, baada
ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo.
Washindi Kombe la Muungano Zanzibar wakabidhiwa Kombe lao
Mrajisi wa Vyama vya Michezo Zanzibar akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Michuano ya Muungano Kepteni wa Timu ya Uhamiaji Sofia Komba Baada ya timu yao kulinyakuwa Kombe hilo Mwaka huu katika Uwanja wa Gmykhana Zanzibar kwa kuifunga Timu ya JKU ya Zanzibar kwa mabao 38-25
Monday, December 21, 2015
Rais Dtk John Pombe Joseph Magufuli ashiriki mazishi ya dada wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, kijijini Msoga
Rais John Pombe Joseph Magufuli akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt JAkaya Kkikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015.
Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kkikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015.
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015
Washindi wa Kamati za kudhibiti Ukimwi Pangani wapewa zawadi zao
Meza kuu,wa kwanza kulia ni Meneja wa redio PANGANI FM Maimuna Msangi, wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA ambalo limeratibu tamasha hilo VERA PIEROTH,wa tatu ni Kaimu mgeni Rasmi ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya PANGANI Bi Patricia, na wanne ni Mratibu wa masuala ya UKIMWI wilaya ya PANGANI.
Shirika lisilo la kiserikali Wilayani Pangani la UZIKWASA linalojishughulisha na kuziwezesha kamati za kudhibiti Ukimwi, VMACK limezawadia kamati bora za kudhibiti ukimwi Wilayani humo. Sherehe hizo zimefanyika sanjari na kuwazawadia kijana bora mfano wa kuigwa na mama bora mfano wa kuigwa. Katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Jaira,K ata ya Madanga wilayani Pangani na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wananchi na viongozi kutoka halmashauri ya Wilaya ya Pangani mgeni rasmi alikuwa Kaimu Afisa Maendeleo Wilaya ya Pangani, Bi.Patricia Kinyange. Akizungumza katika hadhara hiyo Bi. Kinyange amelipongeza shirika hilo kwa kuzijengea uwezo kamati hizo ambazo zinafanya kazi kubwa kwa jamii. “Kwa kweli shirika la UZIKWASA nawapongeza sana, mnafanya kazi kubwa kwenye jamii ya Pangani na kwakweli watu wa Pangani wanapaswa kujivunia uwepo wenu. Nimeshangaa kuona mambo makubwa yanayofanywa na kamati kutokana na elimu mnayowapatia,mnastahili pongezi kubwa”alisema Bi.Kinyange.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifurahi jambo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga (kulia) wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya mwishoni mwa juma mkoa wa Lindi.Picha zote na Zainul Mzige.
Na Mwandishi wetu, Mtwara
NAIBU Waziri katika Wizari wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla ameagiza kubadilishwa kwa mifumo ya utawala, malipo na uendeshaji katika katika hospitali nchini ili kuleta ufanisi na tija. Akizungumza katika ziara yake ya kujifunza kuona katika hali ya kawaida huwa zinatolewaje katika hospitali za wilaya na mikoa alisema kukosekana kwa mifumo bora ya malipo na motisha kumedumaza utumishi.
Ziara yake hiyo ambayo aliifanya katika hospitali ya mkoa wa Lindi ya Sokoine na Ile ya Mtwara ya Ligula ililenga kuona masuala mbalimbali yanayohusiana na utoaji huduma ili kuwa na nafasi ya kutengeneza hali bora zaidi kimkakati.
Alisema tatizo la upungufu wa dawa na hata raslimali watu linasababishwa na kukosekana kwa mfumo waukusanyaji mapato ulio sahihi na wenye salama ambao utawezesha pia kutoa motisha mbalimbali kwa watumishi ili kuwavutia kufanyakazi katika mikoa ya pembezoni.
Aidha alisema malipo yanayofanyika katika hospitali hizo yanatakiwa kuwa ya kielektroniki kwa kuwa imethibitishwa kila kunapokuwapo na mfumo wa malipo kielektroniki unaboresha mapato na hatimaye kuboresha ufanisi katika uendeshaji wa hospitali pamoja na kuwapo kwa huduma bora za dawa.
Tanzania yajikita mstari wa mbele kushughulikia mgogoro wa nchini Burundi
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk Augustine Mahiga amesema Tanzania iko mstari wa mbele kushughulikia mgogoro unaoendelea nchini Burundi.
Balozi Mahiga alisema sio kweli kuwa Tanzania imekaa kimya na haijishughulishi na mgogoro huo, bali ilikuwa imekasimu kazi hiyo kwa Serikali ya Uganda kutokana na majukumu mazito yaliyokuwa yakiikabili nchi hususan Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba mwaka huu.
Alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza na vyombo vya habari Arusha wakati wa ziara ya kujitambulisha kwa Bodi mpya ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) na kutembelea miradi mbalimbali ya kituo hicho.
Alisema Tanzania kutokana na kukabiliwa na mambo mbalimbali likiwemo la uchaguzi, kuchelewa kutangazwa kwa Baraza la Mawaziri ndipo ilipoamua kukasimu uongozi wake wa Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa Uganda ili kuanzisha mazungumzo kuhusu mgogoro huo.
Aliongeza kuwa baada ya Tanzania kuwa katika hali nzuri ya kujikita katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo, ndipo yeye kama waziri wa masuala hayo, alipopokea maagizo kutoka kwa Rais John Magufuli ya kutakiwa kufanya maandalizi yote kwa ajili ya kuanza kwa mazungumzo hayo.
WAZIRI wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk Augustine Mahiga amesema Tanzania iko mstari wa mbele kushughulikia mgogoro unaoendelea nchini Burundi.
Balozi Mahiga alisema sio kweli kuwa Tanzania imekaa kimya na haijishughulishi na mgogoro huo, bali ilikuwa imekasimu kazi hiyo kwa Serikali ya Uganda kutokana na majukumu mazito yaliyokuwa yakiikabili nchi hususan Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba mwaka huu.
Alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza na vyombo vya habari Arusha wakati wa ziara ya kujitambulisha kwa Bodi mpya ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) na kutembelea miradi mbalimbali ya kituo hicho.
Alisema Tanzania kutokana na kukabiliwa na mambo mbalimbali likiwemo la uchaguzi, kuchelewa kutangazwa kwa Baraza la Mawaziri ndipo ilipoamua kukasimu uongozi wake wa Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa Uganda ili kuanzisha mazungumzo kuhusu mgogoro huo.
Aliongeza kuwa baada ya Tanzania kuwa katika hali nzuri ya kujikita katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo, ndipo yeye kama waziri wa masuala hayo, alipopokea maagizo kutoka kwa Rais John Magufuli ya kutakiwa kufanya maandalizi yote kwa ajili ya kuanza kwa mazungumzo hayo.
Saturday, December 19, 2015
Ligi Kuu ya Muungano ya Netiboli Kati ya Polisi Moro na TTPL Uwanja wa Gymkhana. Timu ya Polisi Moro imeshinda 36-33.
Wachezaji wa Timu ya TTPL na Polisi Moro wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Muungano zinazofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar timu ya Polisi Moro imeshinda 36-33.
Mchezaji wa timu ya TTPL Mwanaasha Ali ( GS) akiwa na mpira huku mchezaji wa timu ya Polisi Moro Jawa Iddi (GD) akijiandaa kumzuiya katika mchezo wao wa kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu ya Muungano ya Mchezo wa Netiboli yanayofanyika katika viwanja vya Gmykhana Zanzibar Timu ya Polisi Moro imeshinda 36--33.
Jeshi la Polisi lakanusha madai ya kufanya chujio la vyeti feki kwenye jeshi lao
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa za uzushi na uongo kutumia majina ya taasisi, mashirika ya umma na ofisi za Serikali na kueneza taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kupotosha wananchi.
Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa za uzushi na uongo kutumia majina ya taasisi, mashirika ya umma na ofisi za Serikali na kueneza taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kupotosha wananchi.
Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na taarifa kuhusu Jeshi la Polisi iliyosambazwa jana katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari ‘chujio Jesho la polisi, vyeti feki vyawaonndoa askari kazini’ Taarifa hiyo ni uzushi na hajatolewa na Jeshi la Polisi.
Kufutia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapenda kukanusha taarifa hiyo ya uzushi ambayo haina ukweli wowote na inalengo la kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi kwa jamii.
Jeshi la Polisi nchini limeanza upelelezi wa kuwatafuta watu wote waliohusika kueneza taarifa hiyo na kujifanya wao ni Jeshi la Polisi. Aidha, Tunatoa onyo kali kwa watu wote kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kufanya uposhaji na badala yake watumia mitandao hiyo kwa ajili ya ustawi wa jamii.
Imetolewa na:
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
Wizi wa simu za mikononi, simu feki wafikia tamati, TCRA waja na mwarobaini wake nchini Tanzania
TAARIFA KWA UMMA
MFUMO WA RAJISI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO WA SIMU ZA KIGANJANI (CENTRAL EQUIPMENT IDENTIFICATION REGISTER (CEIR)
UTANGULIZI:
Vifaa vya mawasiliano vya mkononi – hususan simu za kiganjani na vifaa vya mawasiliano vya kiganjani (tablets) – vina namba maalum inayovitambulisha. Namba hiyo inajulikana kama IMEI ambacho ni kifupi cha International Mobile Equipment Identity.
Kifungu cha 84 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 kinataka kuwepo kwa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi. Rajisi hii inajulikana kwa kiingereza kama Central Equipment Identification Register, kwa kifupi CEIR. Sheria inataka rajisi hiyo ihifadhiwe na kuendeshwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Vifaa vya mawasiliano vya mkononi – hususan simu za kiganjani na vifaa vya mawasiliano vya kiganjani (tablets) – vina namba maalum inayovitambulisha. Namba hiyo inajulikana kama IMEI ambacho ni kifupi cha International Mobile Equipment Identity.
Kifungu cha 84 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 kinataka kuwepo kwa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi. Rajisi hii inajulikana kwa kiingereza kama Central Equipment Identification Register, kwa kifupi CEIR. Sheria inataka rajisi hiyo ihifadhiwe na kuendeshwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Aidha Kanuni za mwaka 2011 za EPOCA kuhusu mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi inawataka watoa huduma wa mawasiliano yanayotumia vifaa vya mkononi kuweka mfumo wa kudumu wa kumbukumbu za namba tambulishi (Equipment Identity Register – EIR) za vifaa vya mkononi vinavyotumika kwenye mitandao yao. Mfumo huu wa kielektroniki ambao utahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi una lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vinavyoibiwa, kuharibika, kupotea au ambavyo havikidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano. Vifaa vyote vya mawasiliano vya mkononi ambavyo vimeibiwa, vimeharibika, kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaweza kufanya kazi kwenye mitandao ya mawasiliano kutumia vifaa vya mkononi.
UFAFANUZI
Taarifa kwenye mfumo huu wa rajisi zitakuwa na aina tatu za kumbukumbu; ambazo ni orodha ya namba tambulishi ambazo vifaa vyake vinaruhusiwa, orodha ya namba tambulishi ambazo zimetolewa taarifa kuwa zimefungiwa na namba tambulishi ambazo zimefungiwa kwa muda au kuruhusiwa kwa muda.
Orodha Nyeupe: Orodha ya vifaa vya mkononi vya mawasiliano vinavyoruhusiwa kutumika katika mitandao ya huduma za simu za kiganjani
Orodha Nyeusi: Orodha hii ni ya namba tambulishi ambazo zimefungiwa na mtoa huduma kwenye mfumo wao wa EIR na kutumwa kwenye mfumo wa CEIR kwa ajili ya kufungiwa ili zisitumike kwenye mitandao mingine ya simu za kiganjani kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na kukubaliwa miongoni mwa watoa huduma. Simu zote za mkononi zilizoibiwa au kupotea zitafungiwa ndani ya saa 24 ili zisitumike kwenye mtandao wowote wa simu za mkononi Tanzania. Ikitokea simu ya mtumiaji ikafungiwa kinamosa, anatakiwa kutoa taarifa mara moja kwa mtoa huduma wako kwa ajili ya kuifungua. Watoa huduma wanatakiwa wafungulie, ndani ya saa 24, simu zote zilizofungwa kimakosa.
Friday, December 18, 2015
Droo ya tatu ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" ya GAPCO yafanyika jijini Dar es Salaam
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa kampuni ya GAPCO Tanzania, Jane Mwita (kati) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayoendeshwa na Kampuni hiyo kwa Wateja wake wa jijini Dar es Salaam,ambapo zaidi ya wateja 25 huibuka kidedea kila wiki. Kulia anaeshuhudia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini, Chiku Saleh na Kushoto ni Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi.
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa kampuni ya GAPCO Tanzania, Jane Mwita (kati) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayoendeshwa na Kampuni hiyo kwa Wateja wake wa jijini Dar es Salaam,ambapo zaidi ya wateja 20 huibuka kidedea kila wiki. Kulia anaeshuhudia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini, Chiku Saleh na Kushoto ni Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi.
Thursday, December 17, 2015
TFF yasema wachezaji wapya wenye ITC ruksa kutumika kwa kutumia mtandao wa TMS
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya marekebisho ya kanuni za usajili ambapo sasa mchezaji ambaye usajili wake utakuwa umepita kwenye mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS) atapewa leseni na kuitumikia moja kwa moja timu yake mpya.
TFF itatoa leseni ya usajili wa mchezaji ambaye amethibitishwa kupitia mtandao wa TMS baada ya kuwepo nyaraka zote; mkataba uliomalizika, barua ya kuvunja mkataba, barua ya kuachwa (release letter), mkataba mpya na uthibitisho wa makubaliano kati ya klabu zinazohusika.
Licha ya mchezaji kupata leseni, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji bado itakuwa na mamlaka ya kushughulia upungufu, malalamiko ya kiusajili, pingamizi na uhalali wa kimkataba kati ya pande mbili (mchezaji na klabu).
Wachezaji wote wa kigeni waliosajiliwa kwa ajili ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) wanapaswa kulipiwa dola za kimarekani U$ 2,000 kwa kila mmoja kabla ya kupatiwa leseni na kuanza kuzitumikia klabu zao katika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho.
Wednesday, December 16, 2015
Kwa hili la shamba la mkonge la Kwamdulu Estate, nakubaliana na wanaosema kwamba masikini hana haki
Na Kambi Mbwana, Handeni
Wakati mwingine viongozi wetu wanashindwa kutumia busara kufanya uamuzi wenye tija kwa Taifa na wananchi wake. Angalia, nimekuja Kata ya Segera, Kitongoji cha Kwedihangala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, nilipopata taarifa kwamba wananchi wamevunjiwa nyumba zao na wawekezaji wa shamba la Mkonge la Kwamdulu Estate, linalopita katika vijiji kadhaa vya Korogwe na Handeni. Wananchi hao waliovunjiwa nyumba zao wameishi hapo tangu mwaka 1982. Shamba lenyewe halilimwi.
Kampuni yenyewe imevunja mkataba, maana shamba ni la mkonge na wao eti wanataka walime mitiki. Kwa jinsi shamba lilivyokuwa kubwa, kampuni haitaweza kulilima lote hadi walipokuwa wananchi hao. Mwekezaji anaamuru wananchi wahame ndani ya siku 90 kwa madai wanataka kulima mitiki, wakiogopa kauli ya serikali ya kutaifisha mashamba yasiyolimwa na wawekezaji uchwara. Siku 90 zinaisha, wanatumwa vijana kuanza kuvunja nyumba za walalahoi hawa, masikini wanaoishi kwa kutumia jembe la mkono.
Nimekuja hapa, nimeumia, haswa baada ya kusikia kwamba viongozi wa wilaya ya Handeni wamewataka wananchi hao wahame kama walivyohamia hapo. Huu ni ujinga wa karne. Ningekuwa mimi ni Mkuu wa wilaya ya Handeni, ningezungumza na mwekezaji huyo badala ya kuhamisha wakulima hao, wangewamilikisha heka japo mbili au tatu ili waendelee kulima na kujenga Taifa lao. Kitendo cha kuwataka wahame, wakiwa na mazao yao, mihogo au msimu huu wa kilimo ni kuwasumbua na kuwadhalilisha wananchi hawa.
Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi, Diwani na viongozi wengine wa chama na serikali wanashindwa kuwa upande wa wananchi badala yao wapo upande wa mwekezaji aliyeshindwa kuilima ardhi yetu. Hii si haki. Serikali iliangalie upya suala hili. Wananchi hawa wapewe japo mwaka mmoja au miwili ili wajiandae kuhama sanjari na kuhamisha rasilimali zao. Wana watoto wanasomesha. Wameshiriki mengi ya kimaendeleo kama michango ya zahanati, shule, maabara za sekondari wakitambuliwa kama wananchi halali katika eneo hilo hilo moja. Je, serikali haikujua udhaifu huo?
Hivi msimu huu wa kilimo, hata kama wananchi hao wakihama, watakwenda wapi? Watalima wapi? Na je mwekezaji anaweza kuwafikia mwaka huu au anataka kulima vibarabara ili waonekane wanalilima shamba lote? Wahanga wananiuliza. Je, ungekuwa ni mwaka wa uchaguzi wangenyanyaswa? Nimewaambia nitawajibu siku nyingine.
By Kambi Mbwana, Mwananchi wa kawaida
By Kambi Mbwana, Mwananchi wa kawaida
0712 053949
kambimbwana@yahoo.com
Mungu ibariki Tanzania.
kambimbwana@yahoo.com
Mungu ibariki Tanzania.
Wataalamu wajadili mbinu za kupambana na magonjwa ya milipuko jijini Arusha
Dokta Mwele Malecela wa Kituo cha Utafiti wa Madawa (NIMR) Tanzania akifanya mahojiano jana na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoshiriki katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama ukiwemo ugonjwa wa Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani.Warsha hiyoimeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za barani Afrika na Ulaya wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani. Warsha hiyo imeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za barani Afrika na Ulaya wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani. Warsha hiyo imeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.
Monday, December 14, 2015
Waziri Januari Makamba amtembelea ofisini kwake Makamu wa Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari
Makamba, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba
14, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa
katika mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira, Mhe. Januari Makamba, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini
Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha baada ya
kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Filamu Nne Kutoka Proin Promotions zaingia kwenye kinyanganyiro cha Africa Magic Viewers Choice Awards 2016
Proin Promotions Ltd imefanikiwa kuingiza filamu zake nne katika Shindano la Africa Magic Viewers Choice Awards 2016 (AMVCA 2016) katika vipengele viwili huku Filamu zote nne zikiingia katika Kipengele Kimoja cha BEST MOVIE - EAST AFRICA filamu zilizoingia katika kipengele hiko ni MAPENZI YA MUNGU, KITENDAWALI, MPANGO MBAYA, DADDY’S WEDDING huku filamu ya KITENDAWILI ikiingia katika Kipengele kingine cha BEST INDIGENOUS LANGUAGE MOVIE/TV SERIES – SWAHILI.
Filamu zote nne zimeingia katika kipengele kimoja zikichuana zenyewe huku mbili zikitokea nchini nyingine.
Tunawaomba watanzania kuweza kuzipigia kura filamu hizi ili kuweza kuibuka mshindi. Jinsi ya Kupiga kura fuata tovuti hii www.africamagic.tv
Washindi wa shindano hii wanatarajiwa kutangazwa Mwakani 2016 mwezi wa 3.
Sunday, December 13, 2015
Kozi ya awali ya mafunzo ya zimamoto na uokoaji yafungwa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji, jijini Dar es Salaam
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiwa wamebeba mfano wa majeruhi wa ajali, mara baada ya kumuokoa kutoka eneo la tukio wakati wa maonyesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi hilo,yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakionyesha jinsi ya kuzima moto wakati wa maonyesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi hilo,yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.
Picha kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Ndani
Ziara za kushtukiza zashika kasi, Waziri wa Afya na Naibu wake wavaa vibwebwe
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika Hospitali ya rufaa ya Amana iliyopo Ilala, Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza baada ya sherehe za kuapishwa.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala ikiwa ni masaa machache tangu kutoka kuapishwa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Wizara hiyo. Mhe. Ummy aliwasili katika hospitali ya Mwananyamala, majira ya saa 8 mchana na kuanza kuzungumza na wananchi mbalimbali waliokuwa wamekaa eneo la hospitali hiyo kuhusu matatizo yanayowakabili pindi wanapofika hospitali hapo kupatiwa huduma ambao wengi wao walionekana kutoridhishwa na huduma wanazopatiwa wanazozihitaji.
Mmoja wa wananchi ambao alielezea kwa masikitiko yaliyomkuta pindi alipofika hospitalini hapo ni, Bi. Khadija Meso ambaye alisema kuwa walikuwa na siku tatu tangu wamefika hospitalini hapo ambapo walikuwa wamempeleka mtoto wao ambae alikuwa anaumwa lakini alikuwa hapatiwi huduma hali imeyopelekea kupoteza maisha kwa mtoto huyo. Mwingine aliyezungumza aliyejitambulisha kwa jina la Mama Madohoro alisema kuwa anashangazwa na hospitali ya rufaa kuwatoza wazee pesa licha ya sera ya afya kusema wazee na watoto chini ya miaka 5 kupatiwa bure huduma za kiafya.
Saturday, December 12, 2015
Profesa Muhongo awakalia kooni Tanesco
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Serikali imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuacha mara moja tabia ya kukata umeme bila sababu ya msingi.
Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani walipofanya ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya shirika hilo.
Mara tu baada ya kuapishwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani walifanya ziara hiyo ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuzungumza na Menejimenti ya Shirika hilo.
Profesa Muhongo alisema wananchi wamechoshwa na tabia ya shirika hilo ya kukatakata umeme bila kuwepo na sababu ya msingi ya kufanya hivyo.
“Haiwezekani kila mwaka matatizo ni yaleyale na nyie bado mpo ofisini, hili halikubaliki na halivumiliki. Ninataka tutengeneze historia ya kutatua matatizo ya umeme nchini. Umeme ukiendelea kukatikakatika lazima muondoke,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema wananchi wanahitaji umeme wa bei nafuu ili waweze kujikwamua na umasikini huku akieleza kwamba ni wakati mwafaka suala hilo likatazamwa kwani bei ya huduma ya umeme ikishuka bidhaa nyingine pia zitashuka.
Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliwataka watendaji hao kujieleza ni kwanini umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwataka waeleze wao kama Menejimenti ya Shirika hilo ni hatua zipi ambazo tayari wamezichukua kuhakikisha hali hiyo haijirudii.
Alisema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na hivyo inatakiwa kuwa na umeme wa uhakika.
Vilevile aliwataka waeleze ni kwa nini huwa wanachelewa kufika maeneo ambayo kumetokea hitilafu hali yakuwa wananchi wanatoa taarifa mara tu wanavyoona hitilafu husika.
Dj Bon Love alivyochengua jijini Dar es Salaam
Mkali wa magoma hapa nchini na nje, Dj Bon Love akifanya yake katika Usiku wa Heart & Soul uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye kiota kinachobamba zaidi hapa mjini cha Raphsody, ndani ya Jengo la Viva Towers katikati ya Jiji la Dar. Dj Bon Love na maDJ wengine wakali hukutana pamoja kwenye kiota hicho ili kukonga nyoyo za wapenda Burudani kutoka maeneo mbalimbali.Usiku huo uliwezeswa kwa Udhanimi Mkubwa wa Kilaji ya Heineken.
Baadhi ya Wadua wa Burudani wakiwepo DJ. Venture na Mwanalibeneke Haki Ngowi wakiwakilisha katika Usiku wa Heart & Soul.
Friday, December 11, 2015
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akutana na mabalozi wa Norway na Malawi
Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amekutana na Balozi wa Malawi nchini Tanzania na kufanya naye mazungumzo yaliyolenga kukuza uhusiano wa nchi hizi mbili, sambamba na kuongeza tija ya maendeleo huku wakifahamishana nia ya kuwa na miradi ya pamoja itakayolenga kuongeza uhusiano wa pamoja na kupunguza changamoto zinazozikabili nchi hizi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 11, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais leo Desemba 11, 2015 amekutana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne-Marie Kaarstad ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo walizungumzia kuhusu uongezaji wa mahusiani na ushirikiano hasa katika suala la mazingira. Balozi Kaarstad ni mpya nchini Tanzania na ujio wake ameelezea kuwa unalenga katika kuongeza tija kwa nchi hizi mbili na kwamba Norway itabakia kuwa rafiki wa karibu wa Tanzania.