Pages

Pages

Saturday, December 19, 2015

Jeshi la Polisi lakanusha madai ya kufanya chujio la vyeti feki kwenye jeshi lao

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa za uzushi na uongo kutumia majina ya taasisi, mashirika ya umma na ofisi za Serikali na kueneza taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kupotosha wananchi.
Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na taarifa kuhusu Jeshi la Polisi iliyosambazwa jana katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari ‘chujio Jesho la polisi, vyeti feki vyawaonndoa askari kazini’ Taarifa hiyo ni uzushi na hajatolewa na Jeshi la Polisi.
Kufutia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapenda kukanusha taarifa hiyo ya uzushi ambayo haina ukweli wowote na inalengo la kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi kwa jamii.
Jeshi la Polisi nchini limeanza upelelezi wa kuwatafuta watu wote waliohusika kueneza taarifa hiyo na kujifanya wao ni Jeshi la Polisi. Aidha, Tunatoa onyo kali kwa watu wote kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kufanya uposhaji na badala yake watumia mitandao hiyo kwa ajili ya ustawi wa jamii.
Imetolewa na:

Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.

No comments:

Post a Comment