Pages

Pages

Monday, March 02, 2015

Othuman Michuzi asherehekea kuzaliwa kwake kwa ujumbe moto moto

Napenda Kuchukua Fursa hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma na Mwenye Kurehemu kwa kunijaalia Uhai na afya njema hadi kufikia siku hii ya leo,ambapo ninayo furaha kubwa sana kwa kuongeza namba moja katika umri wangu,kwani bila yeye hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika.

pia nitakuwa ni mchoyo wa Fadhila iwapo sitotoa shukrani za kipekee kwa ndugu zangu woote (wakiwemo wazazi wangu wawili, Ankal Issa Michuzi, Ahmad Michuzi, Karim Michuzi, Ramadhan Michuzi, Ismail Michuzi, Ankal Macheka, Ai Michuzi, Zahra, Tatu, Sellah, Bobby, Noreen, Adam, Saleh na wengine wengi ambao sijawataja majina yenu hapa ila moyoni ninayo,na bila kumsahau mtarajiwa wangu wa ubani bi. Farida) kwa kuwa pamoja nami katika makuzi yaliyo mema hadi leo hii kufikia hapa nilipo.



Tanzania Bloggers Network (TBN) pia naomba mpokee shukrani zangu za dhati kwa kuwa pamoja nami kama mwanachama hai siku zote na bila kunitupa,pia nichukue fursa hii kutoa pongezi kwa uongozi wa TBN na wanachama wenzangu kwa kuungana pamoja katika tafrija ya kihistoria  iliyotukutanisha pamoja,kiukweli ile ilikuwa ni siku muhimu sana kwetu kwa kutukutanisha pamoja na kufahamiana zaidi,ile ilikuwa ni bonge la heko kwani kuna wengine walitamani kuwa na umoja kama wetu lakini hawafanikiwi.

pia nawashukuru marafiki,jamaa zangu pamoja na Wadau woote popote pale mlipo ambao kwa namna moja ama nyingine mmekuwa ni mchango mkubwa katika maisha yangu na kunifanya kila siku niwe bize kuhakikisha libeneke halilali mpaka kieleweke.Nawashukuruni sana tena sana na Mungu awabariki nyoote. Nawapenda sana wote na tuko pamoja sana.


TEMBELEA BLOG YA MTAA KWA MTAA Inayomilikiwa na Besdei boy Othman Michuzi kwa kufuata link hii.
http://othmanmichuzi.blogspot.com
 
Hapa ni dole tupi,nikiwa na wadau wangu Anganile na Hellen Kiwia.

No comments:

Post a Comment