Pages

Pages

Sunday, March 01, 2015

Wakuu wa wilaya za Handeni na Lushoto watakiwa kushupalia migogoro ya ardhi

      
               Na Mwandishi Wetu, Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula pichani juu, amewataka wakuu wa wilaya mpya za Handeni na Lushoto mkoani hapa kuhakikisha wanawajibika ipasavyo kwenye maeneo yao ikiwemo kuipatia ufumbuzi migogoro ya ardhi na viwanja ambayo imeonekana kuleta manunguniko kwa wananchi.

Badala yake amewataka kuhakikisha wanasimamia haki kwa usawa ili kuweza kuondoa migogoro hiyo kwenye maeneo husika ikiwemo kuzipatia ufumbuzi changamoto nyengine ambazo.

Mkuu Mpya wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab Msangi, Mkoani,  akiapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Said Magalula.
Alitoa wito huo jana wakati akiwaapisha wakuu hao wa wilaya ya Handeni,Husna  Rajabu na Mariam Juma wa Lushoto ambao waliteulwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kushika nafasi hizo katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Alisema kuwa kimsingi wakuu hao wapya wanapaswa kwenda kufanya kazi kubwa kwenye wilaya walizopangiwa ili kuweza kuonyesha namna ya uwajibikaji wao katika jukumu hilo kubwa ambalo walipewa na Mkuu wa nchi.

   “Naombeni msimuangushe Rais akawa na maswali mengi kwa uteuzi aliowapa hakikisheni mnatimiza majukumu yenu kwa kusimamia shughuli za maendeleo kwenye wilaya zenu lengo likiwa kuzipa maendeleo “Alisema RC Magalula.
Aidha aliwataka kwenda kushirikiana na wananchi katika maeneo wanayokuwa wakiongoza ili kuweza kuchangia harakati za maendeleo kwa jamii zinazowazunguka.
 
Mkuu mpya wa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Mariam Juma, akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula jana,
Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka kuacha kukaa maofisini badala yake watoke na kwenda kukaa vijijini ili kuweza kubaini changamoto ambazo zinawakabili wananchi ili kuangalia namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Hata aliwataka waweke mikakati mazuri ya kutenda haki kwa wananchi bila ubaguzi wa aina yoyote pamoja na kuangalia jinsi ya kutatua migogoro iliyopo maeneo yao kwa kufuata sheria zilizopo.

   “Acheni kukaa maofisini kusubiria kuletewa taarifa badala yake tokeni mkaangalie changamoto zinazowakabili wananchi lengo likiwa kuangalia namna ya kuzipatia ufumbuzi haraka lakini pia jiepusheni na tabia ya umangi meza“Alisema RC Magalula.

Awali akizungumza baada ya kuapisha Mkuu Mpya wa wilaya ya Handeni,Husna Rajabu Msangi alisema kuwa atahakikisha anatenda haki wakati akifuatilia na kushughulikia masuala ya migogoro ya ardhi kwa kutafuta ukweli ili kuweza kutenda haki kwa kushirikiana na viongozi wenzake.

No comments:

Post a Comment