Pages

Pages

Thursday, March 05, 2015

Kwimba sasa kumekucha, hivi ndivyo ofisi mpya ya Bayport Financial Services inavyoonekana

Hivi ndivyo ofisi mpya ya tawi la 79 la Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services wilayani Kwimba, mkoani Mwanza inavyoonekana kwa mbele siku lilipozinduliwa rasmi mapema wiki hii, huku mgeni rasmi akiwa ni Vicent Emmanuel, Katibu Tawala wa wilaya ya Kwimba, hayupo pichani.
Katibu Tawala wa wilaya Mwanza, Vicent Emmanuel wa pili kutoka kulia, akiangalia matukio tofauti katika uzinduzi wa tawi la Bayport Financial Services, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. Kushoto kwake ni Meneja Mauzo wa Bayport Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Kulia kwa Katibu Tawala ni OCS Adam Amir, akiafutiwa na Meneja wa Bayport Mwanza, August Tesha. Bayport wamezindua tawi la 79 nchi nzima kwa ajili ya kusogeza huduma karibu na wananchi.

No comments:

Post a Comment