Pages

Pages

Monday, October 06, 2014

Kitabu cha ‘Ni Wakati wako wa kung’aa’ chadhamini tamasha la Handeni Kwetu 2014



Na Mwandishi Wetu, Handeni
KAMPUNI ya SmartMind & Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd, imejitosa kudhamini tamasha la Handeni Kwetu 2014, litakalofanyika Desemba 13, wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Kitabu cha Ni Wakati wako wa kung'aa kinavyoonekana kwa nje
Ni mara ya pili kwa kampuni hiyo kudhamini tamasha hilo, kwa kupitia Kitabu chao kijulikanacho kama ‘Ni wakati wako wa kung’aa’, kilichoandikwa na Albert Sanga.

Akizungumza jana mjini hapa, Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kwamba kwa kudhamini tamasha hilo, kampuni hiyo itakuwa na haki zote za kuuza kitabu chao sambamba na kutangaza bidhaa zao kwa kupitia tamasha hilo.

Alisema Sanga ni mjasiriamali mzalendo na mdau wa maendeleo ya Tanzania, hivyo anaamini wadau wa tamasha hili na Watanzania wote wananufaika kwa kiasi kikubwa mno.

“Tunashukuru kwa kupokea taarifa nzuri za udhamini kutoka kwa SmartMind&Patners kwa kupitia kitabu chao cha Ni wakati wako wa kung’aa, kikiandikwa na Sanga, ambaye ndio Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo.

“Mbali na hao, wengine walionyesha moyo wa kulisaidia tamasha hilo msimu huu kwa wakati huu ni pamoja na Phed Trans, chini ya Yusuphed Mhandeni, Handeni Kwetu Foundation, Wait & Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt Ltd,” alisema.

Mbwana alimaliza kwa kuwataka wadhamini wengine kujitokeza kwa wingi yakiwamo mashirika na taasisi za kiserikali kuingia kwenye udhamini ili waliwezeshe tamasha hilo sambamba na kutangaza biashara zao.

No comments:

Post a Comment