Pages

Pages

Saturday, October 04, 2014

Wait & Watch kutoka na filamu ya ‘Lifti’

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI inayokwenda kwa jina la Wait & Watch Film Company Ltd, ipo mbioni kukamilisha filamu yake ya kwanza itakayojulikana kama ‘Lifti’ inayotengenezwa kwa umakini wa hali ya juu.
Adam Mchomvu, mmoja  ya wasanii walioshiriki katika filamu ijulikanayo kwa jina la Lifti.

Filamu hiyo itakuwa ya kwanza tangu kampuni hiyo iliposajiliwa kwa ajili ya kujihusisha na kazi mbalimbali za sanaa, ikiwamo filamu hapa nchini, huku ikiwa na mipango lukuki.

Akizungumza leo asubuhi, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Athuman Kilo, maarufu kama 'Dr Kilo' alisema kuwa wamejipanga imara kuteka soko la filamu hapa nchini.

Alisema mashabiki wa filamu watapata burudani kamili pamoja na kujifunza kutoka kwenye filamu hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inaandaliwa kwa utulivu wa hali ya juu.

“Hii ni kazi ya kwanza ambayo tunaamini itaanza vyema kwasababu vichwa vimetulia na kuangalia namna gani akili zetu zinafanikisha kutoa kazi nzuri.

“Naomba wadau wote wakae mkao wa kula kuisubiri filamu hii ambayo kwa sasa ipo katika hatua za mwisho kabisa kukamilika na itakuwa moto wa kuotea mbali,” alisema Dr Kilo.

Baadhi ya watu walioshiriki katika filamu hiyo ni pamoja na Adam Mchomvu, Khamis Said, Sudi Ally ‘Akui’, Sadiki Manyeko, Jazzmin, Tatu Kingwande, Mzee Jengua na wengineo.

No comments:

Post a Comment