Pages

Pages

Sunday, July 13, 2014

Sekeseke la upangaji matokeo ya kidato cha nne wilayani Handeni lafikia patamu



Na Mwandishi Wetu, Handeni
SEKESEKE la upangaji wa matokeo ya wanafunzi 138 wa sekondari wilayani Handeni, mkoani Tanga, limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa ni kweli wanafunzi hao walisaidiwa na walimu wao katika Mtihani wa kidato cha nne.
Habari kutoka wilayani Handeni, mkoani Tanga, zinasema kuwa wanafunzi hao wa shule za sekondari Kwaludege na Kwankonje, wamefutiwa matokeo yao.
Uamuzi huo umetokana na Tume iliyoundwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Handeni, Dr Khalfany Haule, umebaini kuwa wanafunzi hao walifanya udanganyifu kwenye mitihani yao kwa kusaidiwa na walimu wao.
Juzi Mkurugenzi wa Halmashuri ya wilaya ya Handeni Dk. Halfany Haule alitoa majibu ya tume hiyo kuwa ni kweli wanafunzi hao walisaidia katika mtihani.
Kwa mujibu wa matokeo ya Tume hiyo, serikali imeagizwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya walimu hao walioenda kinyume.

No comments:

Post a Comment