Pages

Pages

Sunday, July 13, 2014

Coastal Union yamng’ang’ania Aurora



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam


UONGOZI wa klabu ya soka ya Coastal Union yenye maskani yake jijini Tanga, Tanzania umesema kwamba hauwezi kuridhia kujiuzulu kwa Mwenyekiti wao Ahmed Aurora, kama inavyodaiwa na baadhi ya wadau wa michezo kuwa mwenyekiti  si za kweli.

Akizungumza jana kwa njia ya simu, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Oscar Assenga, alisema kwa Aurola bado ni mwenyekiti wao na hakuna mpango wowote wa kujiuzulu kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Alisema kuwa mwenyekiti wao hana mpango wa kujiuzulu zaidi ya kuwa na fikra za kuijenga klabu yao kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi ya Tanzania Bara utakaoanza Septemba.

“Hakuna mpango wowote wa kujiuzulu kwa mwenyekiti wetu, maana anachokifanya kwa sasa ni kushirikiana na viongozi wenzake kwa ajili ya kuiongoza timu kwa mafanikio.

“Naamini huu ni wakati muafaka kwa uongozi wetu kutulia na kuhakikisha kuwa Coastal inakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ndani ya Tanga na nje pia, ukizingatia kuwa ligi ijayo itakuwa na ushindani wa aina yake,” alisema.

Taarifa ya kujiuzulu kwa Aurora zimekuja wakati ambao klabu hiyo bado haijatulia mara baada ya Mkurugenzi wa Ufundi na aliyekuwa mdhamini wao Nassor BinSlum kujiuzulu, sanjari na Msemaji wao Hafidh Kido.




No comments:

Post a Comment