Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BEKI wa zamani wa klabu ya Simba, Boniface Pawasa
amesema kwamba ndoto zake sasa ni kuwa kocha wa Kimataifa, baada ya kustaafu
kucheza soka la ushindani uwanjani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Pawasa alisema
kwamba dhamira hiyo itatimia kwasababu ameshaweka mipango kabambe.
Alisema mara baada ya kustaafu kucheza soka, aliamua
kuingia kwenye hatua hiyo ya kuwa kocha mwenye mafanikio makubwa.
“Mipango yangu mikubwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa nakuwa
kocha, hivyo naamini kwa mikakati hii kila kitu kitakuwa sawa.
“Nimekuwa nikipangilia mipango hii kwasababu ndio malengo
yangu makubwa kuhakikisha kuwa nakuwa kocha wa mpira wa miguu,” alisema Pawasa.
Pawasa ni miongoni mwa wachezaji wa soka waliokuwa na
mafanikio makubwa katika soka la Tanzania, huku akiwika kwenye klabu ya Simba
na timu ya Taifa (Taifa Stars).
No comments:
Post a Comment