Pages

Pages

Friday, July 11, 2014

Mdau wa Handeni, John Kida afiwa na kaka yake Charles Kida jijini Tanga

MDAU mkubwa wa Handeni, Bwana John Kida, amefiwa na kaka yake, Charles Kida, jijini Tanga, huku maziko yake yakitarajiwa kufanyika Handeni siku ya Jumapili. Mchana huu mwili wa marehemu ulitarajiwa kusafirishwa wilayani Handeni kwa maziko ya Jumapili ya Julai 13.

Akizungumzia hilo, John Kida, alisema kuwa kaka yake alikuwa anasumbuliwa kwa maradhi, ambapo alikuwa akiishi jijini Dar es Salaam, kabla ya kumsafirisha jijini Tanga kwa matibabu, ambapo kifo chake kilimkuta akiwa jijini Tanga.

"Tunatarajia kufanya mazishi ya kaka Jumapili hii saa nane mchana, baada ya kufariki Dunia usiku wa kumkia leo jijini Tanga, Tanzania," alisema Kida.

No comments:

Post a Comment