Pages

Pages

Sunday, June 08, 2014

Kaseba awataka mabondia wa Kimataifa



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa, Japhet Kaseba, amesema kwamba amekuwa na matamanio ya kupata mapambano ya Kimataifa, kama alivyowika kwenye ulimwengu wa Kick Boxing.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema hata ziara ya nchini Ujerumani na Hispania ina lengo la kutafuta mtandao wa masumbwi kona za Kimataifa.

Alisema alipokuwa katika ulingo wa ngumi na mateke (Kick Boxing), aliweza kuonyesha kiwango cha juu kiasi cha kumfanya aibuke na Ubingwa wa Dunia.

“Bado sijakata tama, maana ndoto zangu ni kuhakikisha nafanya vizuri kwa kupata mapambano makubwa nje ya nchi yetu.

“Naamini nikifanikiwa kufanya zafari zangu mwishoni mwa mwezi huu, basi mipango hiyo itafanikiwa,” alisema.

Kaseba ni miongoni mwa mabondia wenye mipango kabambe ya kuonyesha kiwango cha juu katika sekta ya masumbwi nchini.

No comments:

Post a Comment