Pages

Pages

Friday, May 02, 2014

Yanga yaufyata kukimbiwa na wachezaji wake



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya  Yanga, umesema hautasema lolote kwa sasa, licha ya kuandamwa na wimbi la wachezaji wake wanaodaiwa kukimbilia Azam FC.

Baada ya kusajiliwa kwa Didier Kavumbagu, Azam haikutosheka na kufanikiwa kuinasa saini ya Frank Domayo, hivyo kuongeza machungu kwa mashabiki wake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kwamba hawatafungua mdomo wao kuzungumzia sakata la kuondoka kwa wachezaji hao, badala yake wanaendelea na taratibu nyingine za kuijenga klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya twiga na jangwani.

Alisema suala la wachezaji kusajiliwa kwa klabu nyingine ni jambo la kaiwada, hivyo si lazima wakurupuke kutoa msimamo wao kwa kushinikizwa na watu.

“Hatuwezi kuzungumzia chochote kwa sasa wasababu ya kuondoka kwa wachezaji hao, maana Yanga ni klabu kubwa na yenye mipango endelevu.

“Tutazungumzia mambo yetu kwa utaratibu tuliojiwekea, ukizingatia kuwa kuna wachezaji wengi wazuri na vipenzi vya Yanga waliondoka nab ado timu ikaendelea kuwa imara,” alisema Kizuguto.

No comments:

Post a Comment