Pages

Pages

Thursday, May 01, 2014

Kado: Viongozi Coastal kaeni mmalize tatizo



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KIPA wa timu ya Coastal Union ambaye kwa sasa mkataba wake umefikia ukingoni, Shaban Kado, amewataka viongozi wa klabu yake kukaa ili kumaliza tatizo la mgogoro liliojitokeza.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kado alisema kuwa mgogoro huo unazungumzika ili kuisuka upya timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi.

Alisema endapo uongozi utakaa chini kuangalia wapi wamekwama na kwanini kumeibuka mzozo utakaoifanya Coastal ipoteze mwelekeo.
“Nimeishi Tanga kwa mapenzi makubwa kwa timu ya Coastal Union, hivyo nadhani huu ni wakati wa kuzima mgogoro uliojitokeza kwakuwa hautakuwa na tija.

“Mzozo unazungumzika kwa maslahi ya klabu hii yenye kuungwa mkono na wadau wengi wa Tanga, jambo linalohitaji kuzimwa kwa mgogoro huu,” alisema.
Kwa mujibu wa Kado ambaye mkataba wake umekwisha, mgogoro huo ukiendelea inaweza kuleta tatizo kubwa katika mipango ya kimaendeleo ya klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment