Pages

Pages

Friday, May 16, 2014

Waandishi wapewa mafunzo ya tiba asilia

Mlezi wa Chama Cha Utabibu wa Dawa Asilia Tanzania (ATME),Mzee Kingunge Ngombale Mwiru (kushoto), akifungua mafunzo kwa wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu tiba asilia, May 15,2014 katika ukumbi wa mikutano NIMR jijini Dar es Salaam,ambapo amewataka Watanzania kuondokana na imani potofu dhidi ya tiba asili na badala yake watumie ili kupona maradhi mbalimbali yanayowakabili (kulia),Mwenyekiti wa Chama cha Utabibu wa Dawa Asili Tanzania (ATME), Bw.Simba Abdulrahmani.
Lucey Samwel, kutoka kitengo cha Tiba asilia Wizara ya Afya akiwakilisha mada ya sera ya Afya, Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala, pamoja na taarifa mbalimbali zinazohusu Tiba Asilia na udhaifu katika usimamizi wa sheria ya TATM ya mwaka 2002.
Mkurugenzi kutoka Paseko T.H.P, Othman Shem.akielezea kuhusiana na Tiba Asili Tanzania na changamoto zake.
Mwanasheria kutoka AUDA, Onesimo Munuo (kushoto), akielezea mapungifu ya utekelezaji ya Tiba asili na mbadala.
Wahariri na waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali walihudhuria katika mafunzo hayo.
Mlezi wa Chama Cha Utabibu wa Dawa Asilia Tanzania (ATME), Kingunge Ngombale. Akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.

No comments:

Post a Comment