Pages

Pages

Friday, May 16, 2014

Video mpya ya wimbo wa Mb Dog 'Baby Mbona Umenuna' ni balaa


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, pichani chini, amekamilisha video ya wimbo wake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Baby Mbona Umenuna’.
Video ya wimbo huo imetengenezwa chini ya Abby Kazi, ambaye ameikamilisha mapema wiki hii, huku akijiandaa kuisambaza katika vituo vya televisheni sanjari na kuingizwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Qs Mhonda J Entertainment, Joseph Mhonda, alisema kwamba video ya wimbo huo imeandaliwa kwa kiwango cha juu ili kuwapatia burudani kamili wadau na mashabiki wa Bongo Fleva.

Alisema mashabiki watakaobahatika kuitazama video hiyo watapata burudani kamili kutoka kwa msanii huyo mwenye uwezo wa juu katika kona ya muziki wa kizazi kipya.

“Hii ni moja ya video nzuri za msanii Mb Dog ambaye kwa sasa anajiandaa kuteka tena soko la muziki wa Bongo Fleva, akikumbukia nyimbo zake za zamani zilizomuweka juu, ikiwamo Latifa, Si Uliniambia na nyinginezo.

“Naamini kwa pamoja mashabiki wa msanii huyu watashuhudia uwezo wa Mb Dog ambaye kwa kiasi fulani ni mmoja ya watu wenye ubora wa sauti na ujuzi wa kuandika nyimbo nzurim,” alisema.

Mb Dog aliachia wimbo wa Baby Mbona umenuna mapema mwezi uliopita, ambapo sasa amefanikiwa kutengeneza video yake iliyoandaliwa kwa kiwango cha juu kwa ajili ya kumuweka katika mazingira mazuri.

No comments:

Post a Comment