Pages

Pages

Thursday, May 15, 2014

CCM Kinondoni kuwapa makali viongozi wao mjini Dodoma kwa siku mbili



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, kinaendelea na juhudi zake za kuwafunza viongozi wake ili waweze kwenda na wakati na kufanya siasa zenye ushindani kwa maslahi ya chama na Tanzania kwa ujumla, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2015 nchini kote kwa kushirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu.
Mwenyekiti wa CCM, wilaya Kinondoni, Salum Madenge, pichani.
CCM wilaya ya Kinondoni, leo imewapeleka Makatibu wa Uchumi na Fedha mkoani Dodoma watakaofanya semina ya mafunzo ya siku mbili mkoani humo, wakiamini kuwa ni njia ya kuwapa makali ya kukijenga chama chao kilichofanikiwa kujenga misingi na imani kubwa kwa wanachama wao na Watanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment