Pages

Pages

Thursday, May 15, 2014

Shule ya Sekondari Azania yapigwa jeki, yapata msaada wa kompyuta

Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko (kulia) akimkabidhi moja ya kompyuta Mkuu wa Shule ya Sekondari Azania, Mwl. Benald Ngonzie (kushoto), wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni wanafunzi wa shule hiyo. Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta 10 kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. 
Shule ya sekondari ya Azania inakabiliwa na uchakavu wa miundombinu ikiwamo majengo na ubovu wa vyoo, hali inayohatarisha afya za wanafunzi hao kutokana na kuwapo kwa majimaji anayoweza kuzalisha mbu waenezao ugonjwa wa Malaria na Dengue.
Akizungumza jana baada ya kupokea msaada wa kompyuta 10 kutoka katika benki ya Access, Makamu Mkuu wa shule hiyo Elizabeth Ngoda alisema shule hiyo ni kongwe kwa sasa kutokana na kujengwa muda mrefu hivyo inahitajika ukarabati wa kina.
Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko (kulia) akimkabidhi moja ya kompyuta kwa wanafunzi waliowawakilisha wenzao, anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwl. Benald Ngonzie. Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta 10 kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
  Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko (kulia) akimkabidhi moja ya kompyuta makamu wa rais wa shule ya sekondari ya Azania, Johnson Kaaya, wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa shule hiyo, Mwl. Benald Ngonzie. Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta 10 kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
  Mkuu wa shule ya Sekondari ya Azania, Mwl. Benald Ngonzie akiongea na wanafunzi mara baada ya makabidhiano ya kompyuta kwa shule hiyo iliyotolewa na  Access Bank. Benki hiyo jana ilitoa msaada wa kompyuta 10 kwa shule hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
Ofisa Masoko Mwandamizi Access Bank, Muganyizi Bisheko akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi kompyuta kwa shule hiyo. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
---
"Shule ni kongwe na imezalisha viongozi mbalimbali na sasa imechakaa, majengo yanahitajikukarabatiwa na vyoo havitoshi, lakini tunawashukuru Access Bank kwa kutuletea kompyuta hizi, kwani tulikuwa na kompyuta 25 awali ambazo hazikukidhi mahitaji kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi," alisema Ngoda na kubainisha kwamba shule ina wanafunzi 2000 na wafanyakazi 115.
Ngoda alitoa wito kwa wadau wengine pamoja na wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo,kujitolea kwa hali na mali ili kuirudisha Azania katika hali nzuri ya kimazingira.
Makamu wa rais wa shule hiyo Johnson Kaaya aliwashukuru wadau hao huku akitoa wito kwa makampuni mengine kuchangia katika kurekebisha kasoro kadhaa zilizopo shuleni hapo hasa miundombinu.
"Tunaahidi kuzitumia kompyuta hizi katika kuleta ufanisi na si vinginevyo, tunaomba hii iwe chachu kwa makampuni mengine kusaidia zaidi kwani changamoto kubwa hapa shuleni kwetu ni uchakavu wa majengo, hatuna viti, vyoo vibovu na pia tunapata taabu kipindi cha joto kwani hakuna feni," alisema Kaaya.
Naye Ofisa Masoko Mwandamizi wa Access Bank, Muganyizi Bisheko alisema msaada huo ni katika mwendelezo wa mchakato wa kusaidia sekta ya elimu nchini hasa katika upane wa teknolojia ya abari na mawasiliano ambayo imeonekana kuwa kikwazo kikubwa katika utafutaji wa ajira kwa vijana ambao humaliza shule bila kuwa na utaalamu wa kompyuta.
"Tunaamini kupitia kompyuta hizi wanafunzi wataweza kujifunza programu mbalimbali ambazo zitawasaidia katika kukuza elimu yao hapa shuleni na katika maisha yao," alisema Bisheko.

No comments:

Post a Comment