Pages

Pages

Saturday, May 17, 2014

Harakati za kuuleta mwili wa marehemu Amina Ngaluma



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HATMA ya kuletwa kwa mwili wa marehemu Amina Ngaluma aliyefariki nchini Thailand, itajulikana kesho Jumatatu baada ya kufanikiwa kupata sahihi muhimu kwa baadhi ya barua za maombi ya kuuleta mwili wa mwanamuziki huyo nchini Tanzania.
Marehemu Amina Ngaluma, pichani, enzi za uhai wake.
Amina alifariki Thailand na kuibua simanzi nzito kwa wadau na mashabiki wa muziki wa dansi hapa nchini, kutokana na kifo cha mwimbaji huyo wa Mgumba namba mbili, akiwa ndani ya bendi ya Double M Sound, huku wadau mbalimbali wakiendelea kumlilia mkali huyo wa muziki wa dansi....

No comments:

Post a Comment