Pages

Pages

Sunday, May 18, 2014

Taifa Stars yashinda bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe Uwanja wa Taifa



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mashabiki wa soka wa Tanzania, leo jioni wameondoka uwanjani kifua mbele baada ya kuishuhudia timu yao ya Taifa, Taifa Stars, ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbawe, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mechi ya Stars na Zimbabwe ni ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwaka 2015, ambapo Stars imejiweka katika nafasi nzuri kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa wiki mbili zijazo nchini Zimbabwe.

Bao la Stars lilifungwa dakika ya 13 na John Bocco, huku akilifunga kwa shuti kali nje ya 18, akitumia vyema pasi ya Thomas Ulimwengu.

Stars: Deogratius Munish, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Nadir Haroub Cannavaro, Kelvin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Jonh Bocco, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

Zimbabwe: George Chigova, Partson Jaure, Danny Phiri, Hardlife Zvirekwi, Stephen Alimenda, Tendai Ndoro, Milton Mkude, Kudakwashe Mahachi, Cuthbert Malajila, Peter Moyo na Eric Chipeta.
 

No comments:

Post a Comment