Pages

Pages

Sunday, April 06, 2014

Yanga yaikandamiza JKT Ruvu bao 5-1 Uwanja wa Taifa



Timu ya Yanga SC leo imezinduka tena kwa kuwachabanga kwa jumla ya mabao 5-1 timu ya JKT Ruvu, mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Yanga wakionekana kuwa wachache zaidi katika mchezo wa leo dhidi ya JKT Ruvu ambapo walishinda bao 5-1.

Katika mchezo huo, winga wa Yanga, Mrisho Ngassa alifunga bao tatu kwa dakika ya 8, 15 na 48, wakati goli la nne la Yanga lilifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 40, huku lile la tano likifungwa dakika ya 51 na Hussein Javu, wakati bao la kufutia machozi la JKT likifungwa na Idd Mbaga dakika ya 83.

Mechi ilianza kwa kasi, ila JKT walipunguza umakini na kuwapa nafasi Yanga kulishambulia lango lao mara nyingi na kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono ambao pia umeibua matumaini ya kutetea ubingwa wao.


No comments:

Post a Comment