Pages

Pages

Sunday, April 06, 2014

Super D apongeza pambano la ngumi Chalinze



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA wa mchezo wa masumbwi wa klabu ya Ashanti Boxing, yenye maskani yake Ilala, jijini Dar es Salaam, Rajabu Mhamila ‘Super D’, amesema kwamba kufanyika kwa pambano la Erick Magana na Mwaite Juma wilayani Chalinze ni sehemu ya kuendeleza mchezo huo na kuupatia mafanikio.

Pambano hilo limepangwa kufanyika Aprili 15 katika Ukumbi wa Ndelema Inn, mjini Chalinze, ambalo halitakuwa la ubingwa, huku ikiwa ni njia za kuweka harakati ya kuutangaza vizuri na kuurudisha kwenye hadhi yake ya siku zote.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Super D alisema kwamba wadau wa ngumi wamekuwa wakishirikiana kwa mambo mengi, ikiwamo mbinu nzuri za kuuletea mafanikio makubwa mchezo wa masumbwi.

Alisema mapambano kadhaa ya utangulizi yatakuwapo likiwapo la Biglee Juma, Godfrey Sadick, Hussein Pendeza nao wakitarajiwa kupanda ulingoni kwenye patashika hiyo itakayokuwa na faida kubwa kwa wakazi wa Chalinze na Tanzania kwa ujumla.

“Tuna mipango kabambe ya kutangaza mchezo wa masumbwi katika nchi yetu, hivyo tunaamini kwa pamoja Chalinze watapata burudani kamili kutoka kwa vijana wao,” alisema.

Pambano limeandaliwa kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huo nchini, ambapo kwa siku  hivi karibuni unaonekana kusua sua, hivyo hizi ni juhudi za kuuweka juu,” alisema.

Mchezo wa masumbwi umeendelea kuwekewa mikakati ya kuuweka kileleni baada ya kuonekana kuwa umeanza kusua sua katika kona ya ngumi nchini.

No comments:

Post a Comment