Pages

Pages

Tuesday, April 15, 2014

Wagosi wa Kaya kuja na 'Bao na Gahawa'

Na Asifiwe George, Dar es Salaam
BAADA ya kimya cha muda mrefu wasanii wanaounda kundi la muziki wa kizazi kipya la Wagosi wa Kaya, limetoa vitu vipya vinavyokwenda kwa jina la 'Bao' na Gahawa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, mmoja wa wanaounda kundi hilo
Fred Maliki 'Mkoloni' alisema kutokana na deni kubwa walilonalo kwa mashabiki wao wameamua kurudi upya katika tasnia hiyo.
"Kuthibitisha kuwa ujio wetu sio wa kubahatisha tumejiandaa vizuri kukabiliana na soko gumu la muziki hata upande wa albamu ambao unakimbiwa na wasanii wengi kwa sasa," alisema.
Alisema nyimbo zote mbili zimerekodiwa katika studio ya Tongwe Records na video zake zimeshootiwa Tanga na kampuni ya Ngome video chini ya muongozaji Mecky Kaloka.
"Ujio wa kazi hizo mbili ni wa moja kwa moja na video bila ya kuwachelewesha wasanii kupata ladha tuliyoamua kuirudisha katika tasnia baada ya kimya cha muda mrefu," alisema.

No comments:

Post a Comment