Pages

Pages

Tuesday, March 04, 2014

Wilaya ya Muheza waanzisha doria kukabiliana na uharibifu wa mazingira



Na Mwandishi Wetu, Muheza

MKUU wa wilaya ya Muheza ,Subira Mgalu, pichani, amesema wilaya hiyo imeanzisha doria za mara kwa mara kwenye maeneo ya misitu na ukanda wa bahari kwenye kata za Kigombe ili kuweza kukabiliana na wimbi la uharibifu wa mazingira hususani ukataji wa miti.
 

Mgalu alitoa kauli hiyo wakati akisoma taarifa fupi ya wilaya hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati alipofanya ziara wilayani humo kwa kuzindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.


Alisema wilaya hiyo pia imewaondoa wavamizi waliovamia misitu ya Kwani na Tongwe ikiwemo kupandwa miti ipatayo 1,500,000 ya matunda ,kuni,kivuli na viungo iliyopandwa kuwa kushirikiana na wadau mbalimbali hususani shule,mashirika binafasi kwa ajili ya kuendeleza hifadhi ya mazingira.


Aidha aliongeza kuwa kumekuwa na uharibifu wa tatizo la uharibifu wa mazingira na ukataji miti unaochochewa na mahitaji ya ardhi kwa ajili ya kilimo,mbao kwa ajili ya samani na maeneo ya kulishia mifugo.



Alieleza kuwa licha ya kulishia mifugo kumekuwa na uchimbaji haramu wa madini katika msitu wa asili wa amani ambapo serikali imechukua hatua mbalimbali ili kudhibiti tatizo hilo la uharibifu wa mazingira.


Mkuu huyo wa wilaya alisema wameanzisha kampeni dhidi ya athari za moto na kufanyika vijiji 32 vilivyo karibu na misitu ili kunusuru bionuai ikiwemo kuhamasishwa wananchi kufanya shughuli za ufugaji wa nyuki na upepo ambazo ni rafiki wa mazingira pamoja na kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa misitu na athari za uharibifu wa mazingira.


Hata hivo,Mgalu alizungumzia suala la migogoro ya ardhi kwenye wilaya hiyo alisema mingi kati ya hiyo inahusu uvamizi wa mashamba makubwa ya mkonge ambayo hayaendelezwi ipasavyo pamoja na mipaka ya wilaya inayohusiana na vijiji vilivyopo mipakai ikiwemo mashamba saba ya mkonge,shamba la mifugo lililopo Azimio na shamba la mifugo Mivumoni.


Aliongeza kuwa mgogoro uliopo kati ya Muheza ,Tanga na wilaya ya Pangani hatua za kuuupatia ufumbuzi unaendelea kushughulikiwa katika ngazi ya mkoa na ule kati ya wilaya ya Muheza na Pangani mazungumzo kati ya uongozi wa wilaya hizo mbili bado yanaendelea ili kufikia muafaka.

No comments:

Post a Comment