Pages

Pages

Tuesday, March 04, 2014

Ridhiwani Kikwete aibuka kidedea kura za maoni jimbo la Chalinze, mkoani Pwani?



HABARI ambazo hazijathibitishwa kutoka Chalinze mkoani Pwani, zinasema kuwa Ridhiwani Kikwete, mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ameshinda katika kura za maoni za kuwania ubunge wa jimbo la Chalinze.
Ridhiwani Kikwete, akiwa amepanga foleni kijiji cha Msoga kwa ajili ya kujipigia kura,leo asubuhi.
Ridhiwani amewashinda wagombea wenzake, akiwamo mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Imani Madega, ambao kwa sasa Ridhiwani ndiye atakayeiwakilisha Chama Cha Mapinduzi CCM, kuelekea katika Uchaguzi wa jimbo hilo.

Mwandishi wetu mkoani Pwani anaendelea kufuatilia matokeo ya uchaguzi huo, ambao tangu awali ulibashiri kuwa huenda Ridhiwani akaibuka na ushindi kutokana na siasa za Tanzania kuwa upande wake, sanjari na nguvu zake kisiasa.

Uchaguzi huo unafanyika kujaza nafasi ya mbunge wake wa zamani, Said Mwanamdogo, aliyefariki Dunia, hivyo jimbo hilo kuwa wazi.

No comments:

Post a Comment