Pages

Pages

Tuesday, March 04, 2014

Chadema mkoani Tanga waonyesha makucha yao kwa mwekezeji


Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Tanga(Chadema) Jonathan Bawehje amemuagiza Katibu wa Chama hicho Jimbo la Korogwe Vijijini,Salim Sempori kumuandikia barua Mwekezaji wa Shamba la Mkonge la Kwashemshi Estate awalipe fidia wakazi wa kijiji cha Kwashemshi walioharibiwa mazao yao waliokuwa wamepanda kwenye shamba hilo ndani ya siku saba la sivyo watakwenda kumshtaki mahakamani.

Athumani Rashid, mkazi wa Kwashemshi akizungumza na uongozi wa Chadema Tanga
 Lakini viongozi hao walifika mbali zaidi na kutaka pia kumshtaki Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe Vijijini, Diwani wa kata hiyo, Rasuli Semahombwe na  Mtendaji wa Kata hiyo Kimweri Magogo kwa madai ya kushindwa kulipatia suala hilo ufumbuzi suala hilo.

Mkutano unaendelea.
Agizo la Katibu huyo alilitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi kwenye kijiji cha Kwashemshi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Korogwe,Dastan Mndolwa.


Hatua hiyo ilitokana na wananchi wanaoishi baadhi ya maendeleo yanayozunguka shamba hilo ambao walikuwa wakilima mahindi kila mwaka bila kuwepo kwa usumbufu wa aina yoyote lakini wakashangazwa na hatua ya mwekezaji huyo msimu huu kuharibu mahindi ambapo baada ya wao kupanda mahindi alikwenda kuyafyekea chini kitendo ambacho kimewapa wakati mgumu wakulima hao.

Mkutano ukiendelea.
Aidha Katibu huyo alilaani kitendo ambacho kilifanywa na mwekezaji huyo kwa kuharibu mazao ya wakulima ambao walijitolea kwa nguvu zao kwenda kulima wakitegemea watapata mazao badala yake wameharibiwa na kuzitaka mamlaka husika kulichukulia uzito suala hilo ili waweze kupata haki zao za msingi.

Alisema madhara yaliyopatikana ni makubwa sana na yanarudisha nyuma maendeleo ya wananchi hao na kuwataka kuwa imara kuweza kudai haki zao kwa kufuata utaratibu uliopo kwani wanawajibu wa msingi kufanya hivyo.


  “Diwani ameshindwa kuwatetea wananchi kwenye maeneo yenu nasema hivi sisi kama chadema hatutaki mchezo lazima tuwapeleke mahakamani wale wote wanaohusika na suala hilo ili iwe fundisho kwa vyama vyengine na kama noma na iweze noma “Alisema Bahweje.


Akizungumza kwenye mkutanoi huo,Mmoja wa wananchi wa eneo hilo,Mwanaidi Mussa alisema wao kama wakulima walifuata taratibu zozote zinazostahili lakini wanashangazwa na kitendo kilichofanywa na mwekezaji huyo ambacho wana kifananisha kama cha kinyama.
Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, mkoani Tanga, Jonathan Baweje, akijadiliana jambo na viongozi wa chama hicho Kata ya Kwashemshi, kabla ya kuanza mkutano wao wa hadhara.
“Mimi nimetoa fedha zangu kwenye shamba hilo lakini nashangaa kuja kukamatwa shambani na kuharibiwa mahindi yangu ,nimetoa fedha zangu lakini sijapewa kibali hivyo ninamuomba mh,Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutusaidia suala hili “Alisema Mwanaidi huku akionyesha hali ya masikitiko.
 

Akizungumzia suala hilo,Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mrisho Gambo alisema tatizo hilo wamelisikia kuhusiana na wananchi wao kuharibiwa maeneo yao kwa taarifa za awali walizozipata eneo hilo ni la mwekezaji ambapo wananchi wanapewa kwa ajili ya kulimo kwa kuchangia sh.10,000 kwa shughuli za kilimo kila msimu.


Gambo alisema wao kama serikali watamuita mwekezaji pamoja na viongozi wa kata ya Kwashemshi kuzungumza nao ili kuangalia namna gani wananchi wa eneo hilo wataweza kufaidika na maeneo hayo.


   “Tutamuita mwekezaji na viongozi wa kata ya kwashemshi  tuzungumze nao na  mwisho wa siku tuangalie tunafanya nini ili wananchi wanafaidika kwa kiwango kikubwa kwenye eneo hilo na kama mwekezaji anapaswa kufahama kuwa anapokuwa na wananchi lazima angalie namna ya kuhangaika nao lakini hawezi kumfukuza mtanzania kama anamfukuza mbwa “Alisema DC Gambo.

No comments:

Post a Comment