Pages

Pages

Wednesday, March 05, 2014

Wachezaji wa Lipuli mjini Iringa wapewa viatu

Na Revocatus Mathias, Dar es Salaam

MWENYEKITI  wa Soka Mkoa wa Iringa Sprian Kuamba amewapa viatu wachezaji wa timu ya Lipuli inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza,  ili kuwapa morali kuelekea mwishoni mwa Ligi hiyo.


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kuamba alisema kuwa amefikia hatua hiyo baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wake dhidi ya Majimaji ya Songea na kwmba zawadi hiyo iwe chachu ya ushindi katika mechi zote zilizobaki ili kuhakikisha timu yao inapanda na kuwa katika timu zitakazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.


“Ili timu yetu iweze kusonga mbele inahitaji jitihada ya hari ya juu hasa wakati huu tunapoelekea mwishoni mwa ligi hii ambapo mechi tulizobakiza ndizo zitakazo amua timu yetu inaingia katika ligi ya Vodacom au la, hivyo zawadi hizi ni chachu ya kuhakikisha tunashinda mechi zetu zote tulizo bakiza”,alisema.


Timu hiyo ilipoteza mechi yake mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa timu ya Majimaji ya Songea, na kusema kuwa  zawadi hizo ni kuwatia moyo wachezaji ili wacheze kwa kujituma katika mechi zao zote zilizobaki kabla ya Ligi hiyo kumalizika.


Lipuli FC inashuka dimbani leo katika uwanja wa Majimaji ili kuwania pointi tatu na timu ya JKT Mlale, na baada ya mechi hiyo watajiandaa kuikabili timu ya Pongezi kutoka Mafinga kabla ya kumalizia Ligi hiyo na timu ya Bukinafaso kutoka Morogoro.

No comments:

Post a Comment